Saturday, July 21, 2012

Mtoto wa kambo wa msanii Usher Rymond afariki dunia


Tumepata habari ya kustusha kua mtoto wa kiume wa Tameka Raymond ambae ni mtoto wa kambo wa Msanii usher rymond amefarki dunia siku ya leo.Mtoto huyo aliekua na miaka 11 amefariki kutokan kufatia majeraha aliyokua nayo mtoto huyo yaliyotokana na ajali mbaya aliypiapata mapema mwezi huu.

Daktari aliekua anamtibia mtoto huyo aliamua kuondoa mchine maalum iliyokua inamsaidia kupumua mtoto huyo baada ya daktari kuona majeraha hayo yalikua makubwa sana kwa mtoto huyo kuweza kupona

Glover alipata ajali ya piki piki za majini siku ya tarehe 8 mwezi huu kufuatia kugongana na mwenzie ambae alipoteza muelekeo wa piki piki yake.

Jana Tameka alitweet single moja ya mtoto huyo akiwa na mdogo wake cinco ambae ni mtoto wa usher rymond.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...