Wednesday, August 8, 2012

MKAPA NA SIRI ZA FREEMASON


                             Benjamin Mkapa akiwa na Sir Andy Chande mwaka 1989.
                                                                    Mwaka 2002
                                                                         Mwaka 2003
                                                                       Mwaka 2003
                                                                Mwaka 2003

Na Elvan Stambuli
RAIS Mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa anaongozwa kwa kualikwa katika hafla mbalimbali zinazofanywa na jamii ya siri (secret society) ya Freemasons, hali inayoonesha kuwa huenda ana siri nyingi za taasisi hiyo, Uwazi limegundua.

Kwa mujibu wa mtandao wa kiongozi wa muda mrefu wa jamii hiyo, Jayantilal Kashavji Chande almaarufu Sir Andy Chande, picha nyingi za Mkapa zimewekwa katika mtandao huo na kuelezwa kile alichokuwa akifanya akiwa na kinara huyo wa Freemasons Afrika Mashariki.

MIAKA 100 YA FREEMASONS
Katika sherehe ya jamii hiyo ya kutimiza miaka 100 tangu waingie Afrika Mashariki iliyofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 9, 2004, Mkapa alialikwa na kuwa mgeni rasmi na sherehe hiyo ilifanywa kwa siri kubwa.

Gazeti hili limegundua kuwa Sir Andy Chande katika mahojiano yake na mwandishi mkongwe nchini, Ernest C. Ambali aliyekuwa akiandikia Gazeti la The Guardian, lililokuwa mitaani Oktoba 8, 2004 hakueleza mahali patakapofanyika sherehe hizo jijini Dar es Salaam lakini alitaja waziwazi kuwa mgeni rasmi angekuwa Rais (wakati huo) Benjamin Mkapa ambaye angefuatana na mkewe mama Anna Mkapa.

Hata hivyo, wakati anasimikwa Chaim Henry Gehl kuwa kiongozi wa Freemasons Israel, ilitajwa kuwa sherehe hizo zingefanyika katika Hoteli ya Royal Palm jijini Dar es Salaam ambapo wageni 350 walihudhuria.

MKAPA, SIR CHANDE UGANDA
Mkapa ameonekana katika picha akiwa na Sir Chande nchini Uganda walipotembelea Kiwanda cha Sukari cha Kakira wakati huo akiwa madarakani mwaka 2005. Haikuelezwa kwa nini walitembelea kiwanda hicho.

Sir Andy Chande katika kudhihirisha kuwa ni marafiki na Mkapa, alimpa nafasi katika kitabu chake kuandika utangulizi ambapo rais huyo mstaafu amesema kazi anazofanya mfuasi huyo wa Freemason kwa jamii ni nzuri.

Aidha, Mkapa amebainisha kuwa mara baada ya kufahamiana na mzee Chande, alimteua kuwa mjumbe wa bodi ya Shule ya Shaaban Robert jijini Dar es Salaam na kufanya naye kazi kwa karibu na ndipo alipoelewa zaidi shughuli za Freemasons ambazo ni za kusaidia jamii.
“Mkapa amekuwa akihudhuria hafla nyingi za Freemasons tangu akiwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere,” alisema Mnajimu Maalim Hassan Yahya Hussein aliyehojiwa na gazeti hili.

Aliongeza kuwa shughuli za Freemasons nyingi huwa ni za kijamii na zinafahamika na karibu viongozi wote wa kitaifa waliopo madarakani na hata wale ambao waliongoza nchi.
“Kama kuna siri, basi Mkapa atakuwa anajua maana amekuwa karibu na Sir Andy Chande kwa muda mrefu, tangu enzi za Mwalimu Nyerere” alisema.
Katika mtandao huo, kiongozi wa pili ambaye anaonekana kuhudhuria hafla za jamii hiyo ni rais wa awamu ya pili, Mzee Ally Hassani Mwinyi akifuatiwa na Rais Jakaya Kikwete na hata aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye.

MWALIMU NYERERE
Mwalimu Julius Nyerere naye ana picha mbalimbali mtandaoni humo akiwa na Sir Andy Chande na alikuwa akifuatana na Mkapa katika shughuli za kiserikali kwani imeelezwa kuwa kigogo huyo wa Freemasons alikuwa akiaminiwa sana na baba wa taifa kiasi cha kumfanya kuwa mwenyekiti wa bodi mbalimbali za mashirika ya umma aliyoyaongoza vyema.
Miongoni mwa bodi alizozisimamia kwa umakini mkubwa ni Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Shirika la Usagaji la Taifa (NMC), mashirika ambayo baada ya uongozi wake yalizorota na hatimaye kufa. Sir Andy Chande pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Gazeti la UWAZI hivi karibuni lilimtafuta Sir Andy Chande kwa njia ya simu ili kuhojiana naye lakini mmoja wa wasaidizi wake, Ramji Suryakanti alisema kiongozi huyo amekwenda nchini India kwa ajili ya kupata matibabu.


 Source:Globalpublisher

SERIKALI YATANGAZA AJIRA 800,000

na Tamali Vullu, Dodoma
SERIKALI imesema katika mwaka huu wa fedha, itatengeneza ajira 800,000 katika fani mbalimbali nchini.
Kauli hiyo ya serikali ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara yake kwa mwaka 2012/2013.
Alisema fursa za ajira hizo mpya zitapatikana kupitia miradi ya maendeleo chini ya mpango wa taifa wa miaka mitano unaotekelezwa na wizara na taasisi mbalimbali ((FYDP I).
“Takwimu hizi ni mbali na ajira za watumishi 56,678 watakaoajiriwa na serikali kama ilivyobainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ” alisema.
Waziri Kabaka alisema ajira hizo zitapatikana katika sekta za kilimo, ujenzi, mawasiliano na viwanda.
“Ajira zitakazozalishwa katika Kilimo ni 169,189, ujenzi wa miundombinu ya barabara 646,615, mawasiliano 27,600 na katika sekta ya viwanda na biashara zitazalishwa ajira 5,000,” alisema.
Alibainisha kuwa katika mpango huo wa kuongeza ajira, halmashauri za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zitazalisha ajira 6,885.
Alieleza kuwa katika mwaka wa fedha ulioisha, jumla ya ajira 250,678 zilipatikana kutokana na miradi ya maendeleo.
Alisema ajira zilizopatikana katika miradi mbalimbali ikiwemo Tasaf (34,516), ujenzi wa barabara (42,107) na ujenzi wa majengo ya serikali (17,685).
Miradi mingine kituo cha taifa cha uwekezaji (TIC) ajira 82,834, mamlaka ya ukanda wa kiuchumi (EPZA) 15,100 na serikali ilitengeneza ajira 38,289.
Source: Tanzania Daima

KIPIGO CHA DK. ULIMBOKA CHAZUA BALAA TIGO, WAFANYAKAZI 30 WATIMULIWA WAKIDAIWA KUTOA MAWASILIANO YA SIRI KWA GAZETI LA MWANAHALISI

na Betty Kangonga
KUTEKWA, kupigwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama cha Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka na hatimaye kufungiwa kwa Gazeti la MwanaHalisi kwa muda usiojulikana, kumeleta kizaazaa katika kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Habari kutoka ndani ya kampuni hiyo ya simu yenye mtandao mpana nchini, zinasema kuwa zaidi ya wafanyakazi 30 wamefukuzwa kazi na wengine wako kwenye uchunguzi wakituhumiwa kuvujisha mawasilino ya siri ya simu za wateja kwa Gazeti la MwanaHalisi.
Kwa mujibu wa habari hizo, taarifa za mawasiliano za simu zinazodaiwa kuvujishwa na wafanyakazi hao, zilikuwa kati ya Dk. Ulimboka, Afisa Usalama wa Ikulu na watu aliowasiliana nao kabla ya kutekwa.
Rais Jakaya Kikwete amepata kuliambia taifa mara mbili kwa njia ya televisheni, mwishoni mwa Juni na alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari wiki iliyopita, kwamba serikali yake haihusiki kuteka, kutesa na kumtupa daktari huyo porini.
Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda amepata kuliambia Bunge kuwa, serikali yake haihusiki na utekaji, utesaji na kuhoji, “...serikali imteke ili iweje?”
Hivi karibuni serikali ililifungia Gazeti la MwanaHalisi baada ya kuandika habari iliyomtaja ofisa mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu (TISS), kuwa ndiye aliyetekeleza mpango wa kumteka, kumpiga na kumtesa hadi kumjeruhi Dk. Ulimboka, ambaye kwa sasa anaendelea na matibabu kwenye hospitali moja nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa habari hiyo ambayo serikali inadai kuwa ni ya uchochezi, MwanaHalisi ilianika namba ya simu ya ofisa huyo pamoja na watu wengine wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo linaloendelea kuchunguzwa na kamati maalumu iliyoundwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Vyanzo vya habari kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi waliokumbwa na sekeseke hilo, zinasema kuwa waliofukuzwa wengi ni wafanyakazi wa kitengo cha IT ambao wanadaiwa kuhusika kutoa taarifa za siri ya mawasilino kati ya Dk. Ulimboka na watu wanaoaminika kuwa ni wabaya wake.
Mmoja wa wafanyakazi kutoka Kampuni ya Tigo, aliliambia gazeti hili kuwa mbali na kutuhumiwa kutoa siri kwa Gazeti la MwanaHalisi, wafanyakazi wengine wametimuliwa kwa madai ya kufanya udanganyifu kwenye huduma za Tigo Pesa na kujipatia fedha.
“Kweli watu wengi wamefukuzwa wakituhumiwa kutoa siri kwa Gazeti la MwanaHalisi, lakini wengine walikuwa wakishirikiana na mawakala wa Tigo Pesa kuiibia kampuni.
“Kwa mfano mfanyakazi alikuwa anakubaliana na wakala kumwingizia kiasi kama cha sh milioni moja, lakini anaweza kuingiza hadi sh milioni 1.5 na kati ya hizo sh 500,000 ni mali yake,” alisema mfanyakazi huyo.
Akizungumzia na Tanzania Daima Jumatano, Mhariri Mkuu wa Gazeti la MwanaHalisi, Jabir Idrissa alishangazwa na taarifa za Tigo kuwafukuza wafanyakazi wake kwa sababu ya habari iliyochapishwa na gazeti lake.
“Chanzo chetu cha habari hakikutoka kwa wafanyakazi wa Tigo. Kama wamefukuzwa kwa sababu ya MwanaHalisi, wamewaonea bure. Kama Tigo ndio waliotupa taarifa na zile za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilitoka wapi?” alihoji Jabir na kusisitiza wafanyakazi hao wameonewa bure.
Ofisa Uhusiano wa Tigo, Edward Shila, alipohojiwa kuzungumzia tukio hilo, hakukubali wala kukataa madai hayo na kumtaka mwandishi kumtumia maswali kupitia e-mail yake ili aweze kuyatolea majibu kiofisi.
“Kama una maswali naomba uniandikie kupitia e-mail yangu ambayo nakutumia sasa hivi…maana siko tayari kutoa kauli yoyote isiyokuwa ya kiofisi,” alisema.
Naye Omary Matulla ambaye amejitambulisha kuwa ni ofisa wa kitengo cha kumbukumbu katika kampuni hiyo, alikanusha kuwapo kwa taarifa za kufukuzwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Alisema kuwa kila mfanyakazi ana mipaka ya kufanya kazi katika kampuni hiyo, na pia ni wajibu wa kila mtumishi kutunza siri kubwa.
“MwanaHalisi ana mbinu zake za kupata habari wala haiwezekani kupata habari kupitia kampuni yetu na hata hivyo jambo hilo si rahisi hata kidogo kutokea,” alikanusha Omary.
Dk. Ulimboka alitekwa usiku wa Juni 26, kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Tangu kutokea kwa tukio la kutekwa kwa Dk. Ulimboka, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wamekuwa wakiinyoshea kidole serikali kwamba ndiyo iliyohusika.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi mkoani Dar es Salaam, Suleiman Kova, hivi karibuni alitangaza kumfikisha mahakamani mtu mmoja aliyedai kukiri kuhusika na utekaji wa Dk. Ulimboka.
Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa, polisi wamekamata mtu aitwaye Joshua Malundi kutoka Kenya ambaye amekiri kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka.
Alidai kuwa mtuhumiwa alikwenda kutubu katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Kawe, Dar es Salaam.
Lakini hata hivyo, mchungaji wa kanisa hilo, Josephat Gwajima alikana kauli ya Kova juu ya mtuhumiwa huyo, akisema hajakwenda kutubu kwao.
 
Source: Tanzania Daima

WEMA: MIMI NA DIAMOND NI KAMA RIHANNA NA CHRIS BROWN

                                                               Wema Sepetu.
                                                          Nasibu ‘Diamond’ Abdul.
 BAADA ya kubainika kuwa mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na Nasibu ‘Diamond’ Abdul wamerudisha uhusiano wao, Wema ameibuka na kuufananisha uhusiano huo na mastaa wa majuu, Chris Brown na Rihanna.
Wema alisema hayo hivi karibuni katika mahojiano yake na Mtandao wa Dar Talk ambapo aliunadi uhusiano wao na kueleza namna unavyofanana na mastaa hao wa mtoni.
“...yaani utadhani Rihanna na Chris Brown vile haya matukio maana juzi nilikuwa Kigoma, nikasikia Rihanna naye ameonekana sehemu na Chris,” alisomeka Wema.


Source: GlobalPublisher

BABA: DIAMOND ASITUMIE JINA LANGU

                                                       Nasibu ‘Diamond’ Abdu.
                                 Baba yake Diamond, Abdu Juma.

 Gladness Mallya na Hamida Hassan
SOO juu ya soo! Baada ya mkali wa Bongo Fleva,  Nasibu ‘Diamond’ Abdu kumchana baba yake, Abdu Juma katika gazeti dada na la Ijumaa, mzazi huyo ameibuka na kumtaka mwanaye asitumie jina lake tena, Risasi Mchanganyiko linashuka kwa kujiamini.
Akizungumza kwa uchungu hivi karibuni, nyumbani kwake Magomeni, Dar, mzee Abdu alisema kitendo cha Diamond kumkana kwenye vyombo vya habari  na kusema kuwa yeye siyo baba yake kilimuudhi sana na haoni sababu ya kuendelea kutumia jina lake.

 
SAUTI YA MZEE ABDU KUTOKA MAGOMENI
“Nasibu (Diamond) ni mwanangu na hilo jina nimempa mimi, nimemlea mwenyewe na kumpeleka shule, lakini leo ananikana. Kama ndivyo, aache kutumia jina langu.
“Nilimtumia meseji baada ya kuona gazeti hilo mtaani nikamwambia atafute jina lingine maana ameshasema hanitambui kama baba yake. Namshangaa sana huyu mtoto, hata sitaki kumsikia lakini ipo siku nitamtafuta nimweleze kwa mdomo.
“Sina shida na umaarufu wake kama anavyodhani, yeye aendelee na mambo yake, kwanza hana faida na mimi, si amedai aliyemlea ni mama yake? Basi aendelee naye sitaki kupigizana naye kelele,” alisema mzee Abdu.

KUMBE DIAMOND ALIWAHI KUMPELEKA WEMA KWA MZEE ABDU!
Katika kuthibitisha kwamba, Diamond anatambua yeye ni baba yake, mzee Abdu alisema, alipomvalisha Wema Sepetu pete ya uchumba alimpeleka nyumbani kwake kumtambulisha.
“Diamond alikuja kunitambulisha Wema kuwa ndiye mchumba wake ikiwa ni baada ya kumvisha pete na tulipiga naye picha,” alisema.
Hata hivyo, alikataa kutoa picha hizo kwa waandishi wetu ili zitumike gazetini.
Aliongeza: “Mama yake huwa tunaongea vizuri tu, hata siku hiyo (aliyomwandikia meseji Diamond) nilimpigia mzazi mwenzangu na kumweleza, akaniambia niachane na mambo ya magazeti na redio, mimi nitabaki kuwa baba yake.
“Jambo hilo sikubaliani nalo hata kidogo, kwa sababu tayari amenidhalilisha, hata mtaani kwangu watu wanajua kuwa mimi ni baba yake na bado wanaendelea kuniita Baba Diamond... naitika kwa shingo upande tu,” alisema Abdu.
 
AMWACHIA MUNGU
“Diamond amefanya kitu kibaya na anatakiwa kujua kuwa nimeumizwa sana na kitendo chake, lakini sina namna. Mimi namwachia Mungu, yeye ndiye anayejua kuwa ni mwanangu au lah.
“Mzazi yeyote lazima ataumizwa na maneno mabaya ya mwanaye kama alivyofanya yeye. Si maungwana watu wengine kuiga tabia ya namna hii. Diamond amenidhalilisha,” alisema.


Source:GlobalPublishaer

KANISA KONGO LAMFUNGISHA NDOA MUME NA WAKEZE WATATU, MKANGANYIKO WAIBUKA

                                Anikulapo Kuti akiwa na wake zake watatu wakati wa ndoa yao.
 FELA Anikulapo Kuti, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ametoa mpya kwa walimwengu kwa kufunga ndoa na wanawake watatu.
Mtu huyo ambaye anatumia jina la mwanamuziki  aliyevuma zamani wa Nigeria, hayati Fela Anikulapo Kuti,  amefunga ndoa hiyo kufuatia mchungaji wa kanisa lake nchini humo kuwaambia waumini wake kwamba wanaweza kuoa wanawake wengi, jambo ambalo limeleta mkanganyiko mkubwa kwa waumini wa madhehebu ya Kikristo barani Afrika.
Ndoa hiyo ilifungwa kama kawaida, ambapo watu hao wanne waliapa kuwa mume na wake zake, wakishuhudiwa na watu kibao huku kiongozi aliyeifungisha ndoa hiyo akinukuu vifungu vya Biblia ambavyo hutumiwa na Wakristo wote.
Tukio hili limeleta mkanganyiko mkubwa na kuwaacha watu wengi wakijiuliza mengi kuhusu madhehebu ya Kikristo yanavyojiingiza katika matendo yasiyoendana na imani yao, ambayo inasisitiza mke au mume kuwa na mwenza mmoja tu.


Suorce; www.informationnigeria.org

Tuesday, August 7, 2012

SOMA ALICHOKIANDIKA POLISI ALIYEJINYONGA MORO, ALIMWANDIKIA BARUA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KUMLIPUA IGP,

Nakala ya barua ya askari Dunga kwa Waziri wa Mambo ya Ndani

 Nakala ya barua inaendelea hapa
Baadhi ya wananchi na maaskari wakijadiliana jambo kwenye mwili huo wa Afande Dunga
Danstan Shekidele
Siku chache kabla ya kifo chake askari polisi mwenye namba F 3276, Donald Mathew (33), aliyejinyonga juu ya mti katika daraja la Shani, mkoani Morogoro alimwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani kueleza kinachodaiwa kuwa ni ufisadi unaofanywa na vigogo wa polisi nchini, imebainika.

Polisi huyo aliyefahamika sana kwa jina la Dunga aliwahi kutoa tuhuma nzito dhidi ya maofisa, wakaguzi na polisi wa kawaida, mkoani Morogoro mwaka jana lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya maofisa hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fustine Shilogile, jana alisema jeshi hilo, lilipokea taarifa za kujinyonga Mathew jana asubuhi.

Alisema askari huyo, aijinyonga kwa kutumia vipande vya kamba ya kanga ambavyo viliunganishwa na hakuacha ujumbe wowote unaoeleza sababu ya kuchukua uwamuzi huo.

Alisema askari huyo kabla ya kufanya tukio hilo, alionekana mitaani akinywa pombe katika Baa ya Shani.

Alisema baada ya kuonekana amelewa, Mathew aliamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu, kitendo kilichofanya baadhi ya askari polisi waliokuwa eneo hilo, kumfuata na kumsihi avae nguo.

Alisema marehemu, alihamishiwa mkoani Singida kikazi, lakini Novemba, mwaka jana aliamua kuacha jeshi.

“Pamoja na kwamba marehemu aliacha kazi mwaka jana, sisi kama jeshi bado tunamtambua kama askari mwenzetu… kwa msingi huo tutasafirisha mwili wake Agosti 8, mwaka huu kwenda nyumbani kwake mkoani Kilimanjaro,” alisema Kamanda Shilogile.

Alipoulizwa kama kifo cha Mathew kimesababishwa na baadhi ya askari waliohusishwa kwenye tuhuma za kuhusika na biashara za dawa za kulevya, Kamanda Shilogile alisema uchunguzi unaendelea, na kwamba ikibainika kama kuna askari aliyehusika atachukuliwa hatua kali.

Hata hivyo, askari huyo mwishoni mwa mwaka jana, alitoa tuhuma mbalimbali ambazo zilichapishwa katika moja ya magazeti linalotoka mara mbili kwa wiki, zikiwatuhumu askari 9 wa kikosi cha kupambana na majambazi wa kutumia silaha kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

Tuhuma nyingine alizotoa ni polisi kukamata majambazi wenye silaha, lakini huachiwa baada ya kupewa fedha na mali mbalimbali, hivyo kushindwa kuwafikisha kituoni.

Alisema tuhuma nyingine ni polisi kuwakamata wafanyabiashara wa pombe haramu aina ya gongo na bangi bila kuwachukulia hatua zozote baada ya kuhongwa.

Tuhuma nyingine, zinazodaiwa kufanywa na askari hao ni kushirikiana na matapeli, kutapeli raia wa kigeni na kushirikiana na majambazi kuvunja maduka na kuiba mali za wafanyabiashara nyakati za usiku.\
 
Source:morogoroyetu blog

Kipanya


Monday, August 6, 2012

BEYONCE ACHORA SURA YA JAY Z KWENYE KUCHA ZAKE

Mwanadada superster BEYONCE amewasuprise mashabiki wake kufatilia kitendo chake cha kuchora sura ya mume wake ambae pia ni Msanii mkubwa wa hiphop duniani JIGGA MAN.Beonce aliachia picha mtandaoni ambayo inaonyesha mikono yake miwili ambayo kwenye kidole cha katikati cha mkono mmoja amechora picha ya sura ya JAY Z na mkono mwengine amechora picha yake wote wakiwa wamesmile.Kucha zingine zimezungukwa na nakshi za gold na mapambo mengine ambayo kwa pamoja yanatengeneza jina la "B n JZ"

Jay-Z Gives Approval To Chris Brown & Rihanna's Reconciliation!

Jay-Z has reportedly decided to support his close friend Rihanna by giving his seal of approval to her reconciliation with her ex-boyfriend Chris Brown.
The hip-hop mogul has a close relationship with Rihanna, who is signed to his Roc Nation management label, and was furious when Chris brutally assaulted her in 2009. Despite recent reports Jay-Z had given Rihanna a warning not to reconcile with Chris or he'd drop her from the Roc, sources say he has had a change of heart and wants to support Rihanna with whatever she chooses to do.


"Jay-Z sees Rihanna like a daughter and has sent his right-hand man Jay to Barbados to see what's going on with her and Chris," a source told The Sun.


"She admitted they're pretty much back on and Jay told her they're all behind her and want her to be happy."


Rihanna was said to have hooked up with Chris last month while both were holidaying in Cannes.

Sunday, August 5, 2012

LONDON 2012 OLYMPIC PHOTOS - DAY 9


Gold medalist Tiki Gelana of Ethiopia rests at the finish line on The Mall after the Women's Marathon on Day 9 of the London 2012 Olympic Games.


L-R) Kara Goucher and Shalane Flanagan of the USA at the finish line after competing during the Women's Marathon on Day 9 of the London 2012 Olympic Games at The Mall.

Serena Williams (L) and Venus William of the USA return a shot against Andrea Hlavackova and Lucie Hradecka of Czech Republic during the women's Doubles Tennis gold medal match on Day 9 of the London 2012 Olympic Games at Wimbledon.



Fredrik Loof (L) and Max Salminen of Sweden celebrate overall victory after competing in the men's Star Sailing Medal Race on Day 9.


China celebrates winning the match against Republic of Korea during women's Volleyball on Day 9 of the London 2012 Olympic Games at Earls Court.



Serena Williams (R) and Venus Williams (L) of the United States celebrate after defeating Andrea Hlavackova and Lucie Hradecka of Czech Republic in the Women's Doubles Tennis gold medal match on Day 9.

                                                        SOURCE www.london2012.com

PHOTOS FROM DAY 8 OF LONDON 2012 OLYMPIC GAMES

 (L-R) Tianna Madison of the United States, Allyson Felix of the United States, Shelly-Ann Fraser-Pryce of Jamaica, Blessing Okagbare of Nigeria, Carmelita Jeter of the United States, Veronica Campbell-Brown of Jamaica, Murielle Ahoure of Cote d'Ivoire and Kelly-Ann Baptiste of Trinidad and Tobago compete in the Women's 100m Final on Day 8.


 Jessica Ennis of Great Britain reacts after winning gold in the Women's Heptathlon on Day 8 of the London 2012 Olympic Games at Olympic Stadium on August 4.


 (R-L) Bronze medalist Yanfeng Li of China , gold medalist Sandra Perkovic of Croatia and silver medalist Darya Pishchalnikova of Russia pose on the podium during the medal ceremony for Women's Discus Throw on Day 8


 Sungdong Baek of the Republic of Korea scores a penalty during the Men's Football Quarter Final match between Great Britain and the Republic of Korea, on Day 8.




 Daniel Sturridge of Great Britain takes and misses a penalty in the shoot out during the Men's Football Quarter Final match between Great Britain and Republic of Korea on Day 8 of the London 2012 Olympic Games at Millennium Stadium


Shelly-Ann Fraser-Pryce of Jamaica (R) crosses the line to win the gold ahead of silver medalist Carmelita Jeter of the United States and bronze medalist Veronica Campbell-Brown of Jamaica during the Women's 100m Final on Day 8.



 Micah Richards of Great Britain jumps for the ball with Sungryong Jung and Dongwon Ji of Republic of Korea  during the men's Football quarter-final match.




Kobe Bryant #10 of United States puts up a shot against Lithuania during the men's Basketball Preliminary Round match on Day 8
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...