Dar es Salaam. Ulinzi katika ziara ya Obama ni wa hali ya juu 
kuliko ulinzi wa aliyewahi kupewa Rais yeyote wa Marekani kwa safari 
yake ya Afrika mwaka huu.
Tayari jeshi la nchi hiyo limewasili nchini, 
kuweka mambo sawa na kukagua maeneo yote ya karibu na sehemu 
atakazotembelea na kupita wakati wa ziara hiyo. Maaskari na majasusi 
zaidi ya 500 wapo Dar es Salaam kuhakikisha usalama huo na kuweka vifaa 
mbalimbali vya mawasiliano Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.
Licha ya hilo, ziara yake kutakuwa na askari 1,687
 wakataokuja kwa meli maalumu kubwa ya kivita iliyosheheni silaha 
mbalimbali, ikiwamo ndege sita za kivita aina ya AV-8B Harrier na 
helikopta za kivita 23, ambazo zinatarajiwa kupasua anga la Tanzania 
kuimarisha ulinzi.
Meli hiyo ya kisasa aina ya Wasp Class (Uk 1), pia
 itakuwa imebeba meli nyingine zaidi ya tano maalumu kwa kubeba vifaru, 
magari ya deraya, askari na vifaa vingine itatia nanga Bahari ya Hindi 
kuongeza nguvu iwapo lolote litatokea.
Taarifa inaonyesha italazimika kuwapo kwa meli 
tatu za aina hiyo wakati wa ziara yake nchini Senegal, Tanzania na 
Afrika Kusini kwani mwendo wake siyo kasi hivyo kulazimika kutumia zote 
hizo kwa ajili hiyo.
Meli hiyo kubwa imeundwa kuwezesha askari wa 
Marekani kuingia kwa urahisi eneo la vita kwa brigedi nzima, kwani 
wanaweza kutumia aina zote za vita majini, angani na ardhini. Ni meli 
aina hiyo zilizotumika vita vya Marekani na Iraq. Licha ya mitambo ya 
kivita, ina hospitali kubwa yenye uwezo wa kulaza zaidi ya wagonjwa ya 
600.
Habari kutoka gazeti la mwananchi
Habari kutoka gazeti la mwananchi


 
 









 
 
 
 
