Thursday, January 31, 2013

Listen & download Linez-Mahakama Ya Penzi


Listen & download Shaa-Promise


Listen & Download Hussein Machozi ft C pwaa-Ready to go


Sunday, January 27, 2013

Listen & Download Kimbunga-Mtoto Yatima



Listen & Download Ney Wa Mitego-Ndolela



Listen & Download Gelly Wa Rymes-Pull Up



BARUA YA MDAU WA AMANI KWA MH.BABA RIDHWANI KUHUSIANA NA SAKATA LA MTWARA

Katika pita pita yangu kwenye mtandao wa kijamii wa JAMII FORUM nimekutana na barua hii ya mdau mmoja kwa mh raisi nikaamua nishee na ninyi ndugu zangu kutokana na maneno mazito na ya busara aliyoyaongea mdau huyo,hii hapa isomeni;

Mheshimiwa Rais,

Najua uko bize ofisini kwako ukiendelea kutekeleza majukumu uliyopewa na Watanzania tangu 2010. Au pengine uko nchi fulani ukitembea huku na kule kuaangalia hili na lile ambalo wenzetu hao wameweza kulijenga. Au labda, kwa sababu leo ni wikiendi, uko katika ukumbi mmojawapo wa starehe hapo Magogoni ukipata kinywaji pamoja na wasaidizi wako.

Mheshimiwa Rais, najua unafika Jamii Forums mara kadhaa. Ama, kama wewe binafsi hufiki humu, wasaidizi wako wataisoma barua hii na kukufikishia ujumbe wangu. Ujumbe wangu waweza usitofautiane sana na jumbe nyingi zilizojaa vilio na machozi, ambavyo hata hivyo hukuvijali sana. Hata hivyo ujumbe huu ni wa muhimu kwako hasa kwa sababu unahusu wewe, pamoja na serikali yako kwa ujumla. Waweza kuupuuza kama ulivyozoea, ila tambua kuwa utakapoupuuza ujumbe huu, kuna siku utaukumbuka maana kwa hakika hali ya nchi si shwari.

Mheshimiwa Rais, matatizo yanapozidi, mioyo ya watu huota sugu. Kuna matukio kadhaa ambayo yameshatokea katika nchi yetu. Sitaki kuzungumzia ya nyuma ila nakukumbusha tu kuwa kuna mauaji ya watu watatu kule Arusha, mtu mmoja kule Morogoro, mwandishi wa habari kule Iringa, mtu mwingine kule Arumeru Mashariki, mtu mwingine kule Singida, na maeneo mengine mengi. Nikukumbushe pia mabomu ya Mbagala na Gongolamboto mwaka 2009 na 2011 ambayo yaligharimu maisha ya Watanzania wengi, na wengi kuachwa vilema. Nikukumbushe pia habari za machafuko ya Zanzibar na kuchomwa kwa makanisa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Rais, hayo yote ni tisa; kumi ni suala la gesi ambalo hadi sasa tumejulishwa kuwa wamefariki watu saba na wengine kujeruhiwa. Vilevile huko Morogoro na kuna mapigano ya wakulima na wafugaji, na huko Kariakoo kuna machafuko ya Machinga na Migambo.

Yote haya yanatokea na wewe uko kimya, sijui kwa nini. Umeshakuwa utamaduni wako kukaa kimya pale mambo yaanzapo na hatimaye kuibuka mwishoni mambo yakiwa yameshaharibika. Sijajua vizuri ni nani wanakushauri kufanya hivyo, kukaa kimya, ila nikujulishe tu kuwa wakushaurio wanakushauri vibaya.

Mheshimiwa, hali ya nchi iko tete sana hadi sasa. Hili swala linahitaji hatua madhubuti, si za wasaidizi wako tena, si za Mawaziri wako tena, bali wewe mwenyewe. Kutokuridhishwa na utendaji wako kumeenea kila mahali. Watoto kwa wakubwa, wanawake kwa wanaume, wanalalamika; watu wameshindwa kujua nchi unaipeleka wapi. Kumekuwa na matumizi ya silaha kwa kiasi kikubwa sana. Hali inatisha.

Mheshimiwa Rais, cheche ndogo yaweza kuutafuna msitu mkubwa, hasa msitu wenye nyasi kavu. Tanzania imekabiliwa na matatizo mengi ya huduma za afya, elimu, umeme, barabara, kupanda kwa bei za vyakula, n.k. Kwa ujumla, haya yote yanaifanya Tanzania iwe kama msitu wenye nyasi kavu. Zinapotokea cheche za moto kila upande wa msitu huu, kwa hakika msitu huu utateketea. Msitu huu utakapoteketea, wewe ndiwe utakayeingia matatani zaidi. Kwa hakika, kilichowakuta wakina Ben Ali, Hussein Mubarak na wengine wengi, kinainyemelea nyumba yako.

Mheshimiwa Rais, najua walishakutahadharisha wengi, ila nami niongezee. Suala la Mtwara si la kunyamaziwa hivyo. Nakuhakikishia, badala ya kuvuna gesi Mtwara, utavuna damu, ikiwa hutachukua hatua za haraka. Watu wamechoshwa na unyonyaji wanaofanyiwa. Watu wameota sugu mioyoni mwao. Watu wameshindwa kusubiri, watu wanataka mabadiliko. Watu wanataka wasikilizwe, watu wanataka watambuliwe, watu wanataka waheshimiwe.

Mheshimiwa, ni kweli wewe una majeshi, una askari, una silaha. Lakini wananchi wana mioyo ya ujasiri, wana umoja, wana ndoto, wana hoja; hizo ndizo silaha zao ambazo kamwe majeshi na silaha haviwezi kuzishinda. Ndio maana hadi sasa watu wamekufa huko Mtwara. Watanzania wameshafikia hatua hiyo, wako tayari kufa kwa ajili ya haki. Na kama huchukui hatua za haraka za kutekeleza maoni ya Wananchi wa Mtwara, tegemea vifo vingi zaidi.

Waswahili walisema, mzarau mwiba mguuni huota tende. Naona unapuuzia huu mwiba. Tambua kuwa, mwiba unatakiwa uutoe mapema. Usipoutoa mapema, hakika, utaota tende, hakika utaozesha mguu mzima, na mwisho wake, utaupoteza mguu wako au hata mwili mzima. Kamwe, huwezi kukabiliana na madai ya wananchi kwa kuwaonyesha una majeshi makubwa kiasi gani; wala si kwa kuwaonyesha una silaha kiasi gani; wala si kwa kuwaonyesha wewe ni mwamba kiasi gani. Madai ya wananchi yanatakiwa yafafanuliwe kwa hoja na si vioja, kwa uongofu na si hofu, kwa utashi na si matusi. Watu wanapolia hadi machozi yanapowakauka, na bado wasione kusikika kwa vilio vyao, mwisho wanaamua kuzitoa damu zao, na hizo zitokapo hata wewe hutakuwa salama.

Mheshimiwa, migomo na maandamano vinapokuwa sehemu ya maisha ya wananchi, matatizo yao yasipotatuliwa hadi wagome na kuandamana, tunazalisha kizazi kikaidi, kisichoogopa silaha, kisichoogopa majeshi, kizazi kisichouogopa uongozi. Hya yakishatokea (na yameanza kutokea) nchi itaingia vitani, nchi itakuwa machafukoni, nchi haitatawalika. Tatua matatizo ya wananchi yangali machanga; udongo uwahi ungali maji. Juzi ilikuwa Arusha, leo ni Mtwara, kesho itakuwa Mwanza na Kigoma, keshokutwa Tanga na Pwani; mwisho itakuwa nchi nzima. Matokeo yake utatafuta pa kukimbilia wala hutapaona kamwe.

Tafadhali ipokee barua yangu.

Filamu ya ray iitwayo"sister marry" yapigwa marufuku na maaskofu

 
 
STAA wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ yamemkuta baada ya ile ishu yake ya kutengeneza filamu inayoitwa Sister Marry ambapo mapadri wamemtaka asiipeleke sokoni milele.

Ishu hiyo ilitokea kwenye kikao kizito cha saa 5 kilichofanyika Jumanne iliyopita katika Ofisi za Utamaduni jijini Dar es Salaam.

Washiriki wa kikao hicho walikuwa Ray, Mkurugenzi Mtendaji wa Utamaduni aliyetajwa kwa jina moja la Mwansoke, mapadri wanne na mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni wa kutoka Ofisi za Usalama wa Taifa. Kikao hicho kilikuja baada ya hivi karibuni viongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam kumtaka msanii huyo ajieleze kimaandishi ni kwa nini mtawa Sister Marry (Irene Uwoya pichani) alikuwa akifanya matendo ambayo kiuhalisia, Wakatoliki wenyewe huwa hawayafanyi.

Kabla Ray hajajieleza kwa maandishi ndipo alipoitwa huko na kukubaliana ana kwa ana na jopo hilo huku mashinikizo kadhaa yakielekezwa kwake.

Awali, wajumbe wote wakiwa wamekaa kwenye viti, filamu hiyo yenye saa 3 iliwekwa mwanzo mwisho huku mapadri hao wakiguna kila wakati, hasa wakati Sister Marry akiwa anafanya mambo yake mabaya

Baada ya kumalizika kwa filamu hiyo, hoja zikaanza. Mwansoke akasema vipande vyote vichafu vinyofolewe na kubaki vile ambavyo wajumbe hawakuvigunia.


Baada ya bosi huyo kusema hayo, mapadri wakasema ‘noooo’. Filamu hiyo isiende mitaani hata kidogo kwani imejaa udhalilishaji wa Wakatoliki.

Inasemekana Paroko wa Kanisa
la Mtakatifu Maximilian Kolbe lililopo Mwenge Kijijini (jina halikupatikana mara moja) yeye alipigilia msumari wa mwisho kwa maneno aliyoyatoa.

Alisema kwa kuwa filamu hiyo ilirekodiwa kwenye kanisa lake hilo, anataka vipande vyote vya kanisa hilo vitolewe ndipo iingie mtaani, jambo ambalo lilimtoa machozi Ray.

Ray sasa! Siku ya Alhamisi iliyopita, Ray alizungumza na Amani na kukiri kuwepo kwa kikao hicho. Akasema itakuwa vigumu kuviondoa vipande vya kanisa hilo kwa sababu asilimia 85 ya filamu nzima imerekodiwa Maximilian Kolbe

“Asilimia 85 ya filamu imerekodiwa Maximilian Kolbe, sasa wanaposema niviondoe ni kuimaliza filamu yote. Filamu ni ya saa 3, ukivitoa vipande vya kanisa si itabaki dakika 5 tu,” alisema Ray.

Alisema kikao kiliisha kwa maamuzi hayo, kwamba mtu wa utamaduni alisema vipande vichafu vinyofolewe huku mapadri wakitaka muvi nzima isiende sokoni na paroko wa Maximilian Kolbe akitaka kanisa lake lisionekane kwenye filamu hiyo.

Mwandishi: “Je, wewe Ray umeamuaje?”

Ray: “Sijaamua chochote kwa kweli. Niponipo tu, nimetumia fedha nyingi sana.”

Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP watua Mtwara kusaka suluhu!

Mda si mrefu uliopita Waziri mkuu Mheshimiwa Mizengo PK Pinda, Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi na IGP Saidi Mwema Wamewasili Mtwara na Sasa wapo Ikulu ndogo wakiendelea na Mazungumzo na wenyeji wao.

Wakati huohuo ndege mbili za Jeshi zimepeleka Askali Polisi na Jeshi huko Mtwara ili kuongeza nguvu ya ulinzi.

Tutaendelea kutoa updates zaidi juu ya hili

Listen and Download Izzo b ft Ngwair & Quick Rocka-Ballplayer



TAARIFA YA NDUGU ZITTO KABWE (MB) KUHUSU YANAYOENDELEA MTWARA NA MRADI WA BOMBA LA GESI ASILIA

Mbunge, Kigoma Kaskazini (Chadema) Waziri Kivuli wa Fedha Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni,  Zitto Kabwe
 

TAARIFA YA NDUGU ZITTO KABWE (MB) KUHUSU YANAYOENDELEA
MTWARA NA MRADI WA BOMBA LA GESI ASILIA
 
Serikali iache kutafuta mchawi, iende Mtwara

Katika kipindi cha wiki nne sasa kumekuwa na maandamamo, malumbano na vurugu kuhusu mradi wa kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Mradi huu wa kutandaza bomba la urefu wa kilometa 542 ni mkubwa sana hapa nchini, na una thamani kubwa zaidi kuliko miradi mingine yote  ya miundombinu iliyopata kutokea hapa nchini. Mradi huu utajengwa kwa mkopo wa dola za Kimarekani 1.2 bilioni kutoka Benki ya Exim ya China.

 

Wananchi wa Mtwara kupitia maandamano ya tarehe 27 Desemba 2012 wametaka kujua hatma ya maendeleo ya mikoa wa kusini kutokana na mradi huu wa bomba la gesi. Serikali imewajibu wananchi hawa kwa kuwaita wahaini, watu hatari na wasio elewa. Imefika mahali inapotosha madai yao kwamba hawataki gesi itoke Mtwara.

 

Kimsingi Serikali haijajibu hoja yeyote ya msingi ya wananchi wa Mtwara kuhusu mradi wa kusafirisha gesi. Badala yake imekuwa ikijaribu kupotosha madai ya watu wa Mtwara kupitia mikutano na vyombo vya habari.

 

Tangu maandamano haya yatokee, na baadaye mikutano ya hadhara na
hatimaye matukio ya kusikitisha ya kuharibu mali za watu, mauaji ya
watu na majeruhi mbalimbli, Serikali na hasa Wizara yenye dhamana ya
mradi huu, imekuwa ikitoa matamko kwenye vyombo vya habari badala ya
kwenda Mtwara kuzungumza na wananchi, kusikiliza madai yao na kuona
namna ya kutekeleza madai hayo. Kutokana na Serikali kutofanya hivyo,
kusikiliza na kuzungumza na wananchi wa Mtwara, vurugu mbaya sana zimeendelea mkoani humo.


Mwezi uliopita, Desemba 2012, tatizo lilionekana kuwa ndogo na lenye kuhusiana zaidi na ukosefu wa kushirikishwa kwa wananchi. Badala ya kushughulikia
tatizo likiwa bado ndogo, Serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisemakuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogoro

huu.

 

Leo hali iliyopo mkoani Mtwara inasikitisha sana, maana mali za wananchi zinaharibiwa, nyumba zinachomwa moto na watu wanapoteza maisha. Tunalaani matukio haya kwa nguvu zetu zote, maana kinachotokea Mtwara si Utanzania. Tusipowasikiliza wananchi na kutatua mgogoro huu kwa kuwashirikisha, hali itazidi kuzorota wakati tukitupiana lawama.

 

Hivi sasa serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisema kuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogoro huu.

 

Kwanza, Serikali imekuwa ikiaminisha umma kwanza suala hili limechukuliwa kisiasa. Pili, Serikali imekuwa ikirudia kusema kuwa baadhi ya makampuni ya uwekezaji nchini na mataifa ya Magharibi yamekuwa yakichochea wananchi wa Mtwara.

 

Katika mwendelezo wa mtindo wa Serikali wa ‘management by press conferences’ jana Jumamosi Naibu Waziri wa Nishati na Madini ndugu George Simbachawene aliwaambia wahariri kwamba mimi Zitto Kabwe ninachochea wananchi wa Mtwara, ninatumiwa, na si mzalendo. Vile vile alitoa vielelezo kadhaa kuonyesha kuwa mradi wa kujenga bomba la gesi ni gharama sawasawa. Akasisitiza kwamba mimi ni mwongo.

 

Katika kipindi chote cha mgogoro wa Gesi Mtwara, sijafika Mtwara. Sijafanya mkutano wowote na waandishi zaidi ya kuandika mawazo yangu, kama Mtanzania kuhusu suala hili.

 

Nimeandika makala nne na zimechapishwa katika magazeti kadhaa hapa nchini na kwenye blogu yangu (www.zittokabwe.com).

 


 

Sitaki kubishana na Naibu Waziri ama Kiongozi yeyote ya Serikali kwa sasa. Hatuwezi kuendelea kulumbana, kuzozana, kuzodoana na kurushiana maneno wakati nchi yetu inaungua. Huu sio wakati wa kutafuta mchawi bali kutafuta majawabu ya changamoto zilizopo mbele yetu.

 

Yanayotokea Mtwara ni fundisho kwetu kwa Taifa namna ya kukabili changamoto za utajiri wa rasilimali, ili kuweka mkakati, mambo haya yanayotokea Mtwara yasitokee tena Tanzania. Tutaweza kuzuia maafa haya iwapo tutaweka uwazi katika mikataba, tutashirikisha wananchi kwenye unyonyaji wa maliasili za nchi, na iwapo tutaweka uwajibikaji.

 

 

Rais Kikwete Kikwete ana majibu; ayatoe sasa kwa wana Mtwara

 

Kwa mujibu wa Mpango Kabambe wa Umeme nchini (Power System Master Plan), kulikuwa na mradi wa kufua umeme MnaziBay, ambao Rais Jakaya Kikwete aliagiza utekelezwe mara moja. Serikali ieleze umma kuhusu mradi huo wa kujenga kituo cha kufua umeme 300MW MnaziBay Mtwara na kujenga msongo wa umeme wa 300KV mpaka Singida. Umeishia wapi? Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 12 Oktoba 2012, Rais Jakaya Kikwete alipokea ripoti ya ujenzi wa mradi huu kutoka makampuni ya China National Machinery & Equipment Import & Export Corporation (CMEC) ya China na Siemens ya Ujerumani, ambayo kwa pamoja yalitarajia kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kutokana na gesi katika eneo la Mnazi Bay, mjini Mtwara na pia kujenga njia ya kusafirisha umeme ya kilomita 1,100 kutoka Mtwara hadi Singida. Mradi huu ungegarimu dola za kimarekani milioni 684 na Rais aliagiza utekelezwe haraka sana. Huu mradi uliishia wapi? Kwa nini Serikali ipo kimya kuhusu mradi huu ambao ungejibu kabisa maswali ya watu wa Mtwara? Taarifa ya Ikulu kuhusu mradi huu imeambatanishwa hapa.

 

Tufanyeje?

 

Hapa tulipofikia ni lazima kwanza kabisa kusikia kilio cha wananchi wa Mtwara ikiwemo kuelewa madai yao. Swali kubwa kubwa la watu wa Mtwara na Kusini kwa ujumla ni ‘tunanufaikaje’? Jibu la swali hili si ahadi za miradi bali ni vitendo. Hapa ndipo serikali inaposhindwa kushughulikia suala hili, kutoelewa madai ya wananchi na kuyapotosha.Viongozi wa kisiasa wenye ushawishi kutoka pande zote, chama tawala na vyama vya upinzani, waende Mtwara kuzungumza na wananchi, lakini wawasikilize kwanza.

 

  1. Lazima viongozi tujenge utamaduni wa kusikiliza wananchi na si kuwahutubia tu. Wananchi wa Mtwara wana madai ambayo lazima viongozi tukae kitako kuwasikiliza kisha kufanya nao majadiliano ambayo yatatoa mwafaka. Rais mstaafu, Ndugu Benjamin Mkapa ameshatoa kauli kuhusu suala hili. Ni wakati mwafaka sasa kwa viogozi wengine kumuunga mkono kwa kwenda Mtwara na kukaa na wananchi wa Wilaya zote za Mtwara, kusikiliza hoja zao na kuona namna ya kupata ufumbuzi wa suala hili. Wakati hatua hii inachukuliwa, wananchi waombwe kutulia na kuacha vurugu za aina yeyote ile, na Serikali isimamishe mradi mpaka hapo suluhu na wananchi itakapopatikana.

 

  1. Wakati juhudi hizo zinaendelea Serikali iweke wazi mkataba wa ujenzi wa bomba, kwani ni dhahiri gharama za mradi huu ni kubwa mno kulingana na uhalisia wa miradi ya namna hii duniani kote. Katika taarifa zote kwa umma Serikali imekuwa ikisema kwamba mradi utagharimu jumla ya dola za kimarekani 1.2 bilioni, lakini katika taarifa ambayo Wizara ya Nishati na Madini imesambaza jana kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini imesema mradi utagharimu dola za kimarekani milioni 875. Usiri katika mkataba huu unaashiria kwamba Serikali inaficha kitu. Hivyo njia pekee ni kutaka mkataba uwe wazi kwa wananchi.

 

  1. Wakati tunawataka wananchi wa Mtwara kuruhusu utulivu, ni vema Serikali ijiandae kutoa majawabu ya madai ya wananchi hao. Majawabu ya Serikali yajikite kueleza wananchi wa Mtwara wanafaidikaje na rasilimali ya gesi asilia kwa maendeleo yao. Wananchi wa Mtwara wanataka uwajibikaji wa Serikali kwenye utajiri wa nchi, na wamechoka na porojo za orodha ya miradi isiyotekelezwa.

 

Viongozi twendeni Mtwara kusikiliza wananchi wetu. Nchi inaungua na hatuwezi kuendelea kuzozana badala ya kuzima moto huu hatari kama vita vya MajiMaji. Mimi nakwenda Mtwara haraka na mara baada ya viongozi wangu wa chama kutoa ridhaa.

 

 

ZITTO KABWE

Mbunge, Kigoma Kaskazini (Chadema)

Waziri Kivuli wa Fedha

Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni



Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...