Saturday, March 2, 2013

TAMBUA MABINGWA WALIOPITA, MPIRA NA JEZI ZA NIKE ZITAKAZO TUMIKA BRAZIL 2014


Hawa ndio mabingwa wa dunia wa mwaka 98,kama utakua na macho makali jamaa aliyebeba kombe ni Zinadine Zidane.Pembeni upande wa kushoto mwa zidane ni Desaily na huyu wa upande wa kulia mwa zidane Rizarazu

  Hii ni jezi itakayotumiwa na Uholanzi au Dutch Men "The Orange"

 Hii ni jezi itakayotumiwa na URENO

Hawa ndio mabingwa wa mwaka 2002,walioshika kombe kushoto Rivaldo,katikati Ronaldo,Kulia ni Gilberto
 Huu ndio mpira wa brazzuga utakaotumiwa kwenye kombe la dunia 2014
 Hii ndio jezi itakayotumiwa na Marekani
Hii ndio jezi atakayotumiwa na Brazil

Friday, March 1, 2013

Cheki hapa "TRACK LIST" ya MIXTAPE Mpya ya Meek Mill "Dreamchaser 3"


Hii ni mixape ya 3 katika mfulilizo wa mixtape za Dremchaserseries kutoka kwa meek mill

MSEMO WA ‘KUFELI MTIHANI SIYO KUFELI MAISHA’ UNAVYOWAHARIBU VIJANA!-2


NINA kila sababu ya kumshukuru Mungu ambaye amenibariki kuwa mmoja kati ya wale waliobahatika kuiona siku ya leo wakiwa bukheri wa afya.
Ni matumaini yangu kuwa, nawe umzima na uko tayari kusoma sehemu ya pili ya makala haya ambayo niliianza wiki iliyopita.
Lengo hasa la makala haya ni kuonyesha umuhimu wa elimu katika maisha ya leo. Usipokuwa umeelimika maisha yako hayawezi kwenda sawa, utakwenda lakini utafika mahali utakwama.
Ndiyo maana nikaona niwakumbushe wale wanaoona kuwa elimu haina faida wasijidanganye na nisisitize tu kwamba, msemo wa kufeli mtihani siyo kufeli maisha hauna mantiki yoyote.
Tusijipe matumaini kwa njia hiyo kwani ni ukweli usiyofichika kwamba, elimu ni kitu muhimu sana katika ulimwengu wa sasa na waliyoikosa tunashuhudia wanavyohangaika.
Juzijuzi hapa yalitangazwa matokeo ya kidato cha nne. Tumeona wengi walivyofeli. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa. Cha ajabu sasa wakati watu makini wakijadili chanzo cha kufeli huko, wapo ambao wala hawajali, wanaamini kufeli kwao hakuna madhara yoyote.
Ndiyo maana wakati mwingine unaweza kukuta mwanafunzi ana uwezo mzuri wa kufaulu kama atasoma kwa bidii na kujiwekea malengo lakini kinyume chake anachukulia kusoma kama fasheni na wala hajali pale anapopata alama mbaya.
Hajali kwa kuwa ameshajiwekea akilini mwake kwamba, hata asipofaulu maisha yake yanaweza kuwa poa tu huku akitolea mfano wale ambao hawakusoma lakini leo wana maisha mazuri.
Wengine utawasikia wakisema: Aah! Mbona fulani alipata ziro lakini mambo yake ni safi? Mbona fulani aliishia darasa la saba lakini sasa ni tajiri?” Jamani hiyo ni bahati ya mtu. Usitarajie kwa sababu mwenzako mambo yake yamemnyookea bila ya ya kwenda shule basi na wewe unaweza kuwa hivyo.
Huko ni kujidanganya. Wengi ambao hawakusoma au walikwenda shule lakini wakazembea na hatimaye kufeli hawana maisha mazuri. Hao ndiyo wamekuwa na maisha ya kushinda vijiweni huku wakipiga mizinga kwa kila mtu anayekatiza mbele yao.
Ni wasomi wachache sana ambao hawana maisha mazuri na ukifuatilia utabaini kuwa, walizembea na kushindwa kutumia elimu zao katika kuyaboresha maisha yao.
Nimalizie kwa kushauri tu kwamba, elimu ina umuhimu mkubwa sana katika maisha hivyo unapopata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii na hakikisha unafanya vizuri.
Pia itumie elimu yako vilivyo kuhakikisha unakuwa na maisha mazuri ili kujitofautisha na waliokimbia umande.

DEMU WA MBUNGE AIBU TUPU

Na Shakoor Jongo
SIKU chache baada ya gazeti damu moja na hili, Risasi Jumamosi kutoka na habari iliyoambana na picha zilizopigwa katika chumba cha hoteli zikimwonesha mbunge wa jimbo moja nchini  akijivinjari na dada mmoja wa mjini, aibu zaidi imemwangukia binti huyo baada ya picha zake za utupu kuvuja.

Mjasiriamali huyo wa mjini, katika habari hiyo jina lake lilifichwa lakini sasa tunalianika kwa jina moja la Sheila ambaye makazi yake ni Kinondoni jijini Dar.
Habari za moto zilizopatikana kutoka kwa vyanzo makini vya Ijumaa, vimepenyeza maelezo ya kutosha kuhusu ‘mjasiriamali’ huyo kuwa ni moto wa kuotea mbali kwa vigogo.
“Sheila ni mjanja sana, ana mawasiliano ya vigogo wengi ndiyo maana anawapata kirahisi lakini sasa sijui hii akili ya kijinga ya kupiga picha chafu anaipata wapi. Kwa mtu anayefikiri sawasawa hawezi kufanya upuuzi kama huu,” kilieleza chanzo chetu kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini.

Folda lenye picha chafu za dada huyo zilizopigwa katika mikao ya kihasarahasara (haziwezi kuachwa wazi gazetini) zipo kwenye dawati letu kama ushahidi – anayetaka kuziona aje ofisini kwetu Global Publishers zilizopo Bamaga – Mwenge, Dar.
 “Hizi picha sasa hivi zimezagaa sana mitandaoni, yaani anajiabisha sana. Sijui kwa nini wasichana wa siku hizi wanakuwa na tabia mbaya kiasi hicho,” kieleza chanzo chetu kikisisitiza kutoandikwa jina lake gazetini.

Chanzo ;Global Publisher

Pombe Noma: Abakwa Baada ya Kuzidiwa na Pombe

Huyu ni mrembo aliyekuwa amepata mwaliko toka kwa jamaa mmoja ambaye walijuana katika birthdaya ya rafiki yake.....

Inadaiwa kuwa Binti huyu anasifika kwa kuwachuna wanaume wanaoigia katika anga zake na kuwatelekeza.Bahati mbaya msimu huu haukuwa wake baada ya kuwekea madawa ya kulevya katika kinywaji chacke......


Binti hakuweza kuusoma mchezo maana tayari pombe ilikuwa imeshaanza upanda kichwani....Baada ya muda, mrembo alikuwa hoi bin taabani na ndipo wavulana hao walipombeba na kumbaka na kisha kumwacha

Source:Mpekuzi

Wednesday, February 27, 2013

Download | ASAP Rocky ft Trey Songz - Same Bitch.mp3

Tuesday, February 26, 2013

LISOME HAPA TAMKO LA JUMUIYA ZA KIISLAMU KUHUSU MAUAJI YA VIONGOZI WA DINI NA UCHOCHEZI WA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR KULAANI MASHAMBULIZI NAMAUAJI YA VIONGOZI WA DINI PAMOJA NA KUPINGA KAULI ZA UCHOCHEZI DHIDI YAZANZIBAR


Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu Mlezi wa Viumbe. Sala na salamu zimfikie Mtume wetu Mtukufu Muhammad (S.A.W), jamaa zake, maswahaba zake waongofu na wote wanaowafuata kwa wema hadi Siku ya Malipo.

Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar lililokaa Jumapili tarehe23/2/2013 katika kikao cha kutathmini matukio ya kushambuliwa na kuuliwa viongozi wa Dini yakiwemo ya karibuni ya kupigwa risasi na kuuliwa Padri Mushi pamoja na kupigwa mapanga na kuuliwa Sheikh Ali Khamis Bin Ali Khatibu wa Mwakaje na kuendelea kutolewa kwa kauli za uchochezi dhidi ya Zanzibar linatamka ifuatavyo:

1. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linalaani vikali na kwa nguvu zote matukio ya kushambuliwa na kuuliwa viongozi wa Dini likiwemo tukio la karibuni la kupigwa risasi na kuuwawa Padri Mushi kulikofanywa na wahalifu wasioitakia mema Zanzibar.


2. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linapenda kuweka wazi kuwa uhai ni tunu kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu aliyotunukiwa binaadamu hivyo hakuna mwenye mamlaka ya kuiondoa haki hiyo isipokuwa yeye mweyewe Mwenyezi Mungu. Kutokana na ukweli huu ndio maana Sheria za Kiislamu zimeweka wazi mtu mwenye kumuuwa mwenziwe naye auliwe kama inavyoelezwa katika Kitabu kitufu cha Quran kama ifuatavyo:

“Na humo (katika Taurati) tuliwaandikia ya kwamba mtu (huuwawa kwa sababu yakuuwa mtu) kwa mtu, ……….” (5:44)

Hivyo, vitendo vya kiharamia vya kushambuliwa viongozi wa Dini kulikoanziakwa kumwagiwa tindikali Sheikh Soraga, kupigwa risasi Padri Ambrose Mkenda, kuuliwa Padri huko Musoma, kupigwa risasi na kuuwawa Padri Mushi na kushambuliwa kwa mapanga na kuuliwa Sheikh Ali Khamis Bin Ali Khatibu wa Mwakaje kwa dhulma kulikofanywa na wahalifu ni jambo lisilokubalika na Uislamu na Waislamu wenyewe. Aidha wahusika wa matendo haya wawe wafuasi wa Dini yoyoteile bado watahesabika ni wahalifu kwani vitendo vya kihalifu na kiharamia kamwehaviwezi kunasibishwa na Dini fulani.

3. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linaviomba vyombohusika kufanya upelelezi wa kina kuhusu matukio haya kwa kuzingatia uadilifu namisingi ya kazi zao ili kuwabaini wahalifu na kufikishwa katika vyombo vyakisheria. Aidha Baraza linavitahadharisha vyombo hivyo kuepuka kufanya kazi yaokwa kusukumwa na matashi binafsi, jazba, chuki, matashi ya baadhi ya wanasiasana viongozi wa Dini pamoja na shindikizo la baadhi ya vyombo vya habari.

4. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linalaani na kupinga kwa nguvu zake zote kauli aliyoitoa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania na baadhi ya vyombo vya habari kuihusisha Zanzibar na ugaidi kutokana na tukio la kuuliwa Padri Mushi. Kauli hii inaonesha kuwa Mheshimiwa Waziri anaibagua Zanzibar katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu tunavyoelewa sisi suala la usalama wa nchi ni suala la Muungano hivyo huwezi kuihusisha Zanzibar pekee na suala la ugaidi. Hivyo, Baraza linaona kuwa kauli hizi zinazotolewa ni mbinu za makusudi za kuichafua Zanzibar katika Jumuiya ya Kimataifa kutokana na chuki binafsi dhidi ya Zanzibar na watu wake.

5. Aidha Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linamtaka Mheshimiwa Waziri kwa kulinda heshima yake kuwajibika kwa Watanzania kwa kujiuzulu kutokana na kushindwa kulinda usalama wa wananchi wakiwemo viongozi wa Dini ambao ndio walezi wa jamii.

6. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linalaani kauli za uchochezi zinazoendelea kutolewa na baadhi ya vyombo vya habari zinazochochea chuki, uadui, uhasama na mtafaruku kati ya Waislamu na Wakristo na kusahau kuwa Waislamu wameishi na Wakristo kwaamani, mapenzi na mashirikiano hapa Zanzibar karne na karne. Baraza linaona kuwa vyombo hivyo vya habari vinatekeleza ajenda ya kuivuruga Zanzibar kwa kuchochea vita vya kidini ili kufikia malengo yao wanayoyajua wenyewe. Hivyo, Baraza linaiomba Serikali kuvidhibiti kwa kuvichukulia hatua vyombo vyote vinavyotumia matukio haya kuchochea uadui na chuki kati ya Waislamu na Wakristo.

7. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linaviomba vyombo vya habari vya Zanzibar kuwajibika kwa Wazanzibari wanaolipa kodi kwa kuwapasha taarifa sahihi juu ya matukio muhimu yanayotokea katika jamii yao badala ya wananchi kutegemea kupokea taarifa za upotoshaji na uchochezi kutoka katika vyombo vya habari visivyotutakia mema.

8. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linaziomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar kuwasilisha kwa Watanzania taarifa ya wazi ya matokeo ya uchunguzi wa matukio haya kwa kuanzia na lile la kumwagiwa tindi kali Sheikh Soraga, kupigwa risasi Padri Ambrose Mkenda, kuuliwa Padri huko Musoma, kupigwa risasi na kuuwawa Padri Mushi na kushambuliwa kwa mapanga na kuuliwa Sheikh Ali Khamis Bin Ali Khatibu wa Mwakaje.

9. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linawaomba Wazanzibari wote kuwa watulivu katika kipindi hichi ambapo upelelezi wa matukio haya ukiendelea. Aidha Baraza linawasihi Wazanzibari wote bila ya kujali tofauti zao za kidini kulinda umoja wao na kudumisha amani pamoja na kukataa kugawanywa ilikuwatoa katika ajenda yao ya msingi ya kudai Mamlaka Kamili ya Zanzibar katikaMuungano.

MOLA WETU MTUKUFU TUNAKUOMBA UINUSURU ZANZIBAR NA WATU WAKE DHIDI YA MAADUI WANDANI NA NJE WASIOITAKIA MEMA NCHI YETU

Imesainiwa na:

Sheikh Ali Abdalla Shamte
Amir wa Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar


Habari imetoka JamiiForum

KUA WA KWANZA KUDOWNLOAD NYIMBO MPYA YA NGWAIR AKIWA NA TID (MNYAMA) HAPA


Monday, February 25, 2013

KUTOKA SAMMISAGO.COM | PICHA 12 ZA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MAZISHI YA GOLDIE


Andrew Harvey Mume wa Goldie Akijitayarisha Kuingia Kanisani.


Andrew Harvey Mume wa Goldie Akimgusa Mkono Goldie Kabla Ya Sala.





Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...