Tuesday, June 21, 2011

NGWEA, STEVE, SQUEEZER BASI ZIZZOU ENTERTAINMENT

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo waliokuwa chini ya Lebo ya Zizzou Entertainment, Albert Mangwea ‘Ngwair’, Steve RnB, Edson William ‘Baby Boy’, Squeezer na Mzee Zahir Zorro wamemaliza mkataba wao wa awali na kampuni hiyo na sasa wako huru kwenda lebo nyingine.

Akipiga stori na Showbiz, Mkurugenzi wa kampuni hiyo inayoibua na kuendeleza vipaji vya wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Tippo Athuman, aliweka plain kuwa mkataba na wasanii hao umeisha tangu Machi mwaka huu na kwamba hana mpango wa kuingia nao mkataba mwingine.

ZAHIR ZORRO

“Mkataba wao uliisha tangu Machi mwaka huu na hakuna mpango wa kuingia nao mkataba mpya, naangalia uwezekano wa kuibua vipaji vingine, kwa sasa wanaruhusiwa kuwa chini ya mtu au kampuni nyingine,” alisema Tippo.


 Tippo Athumani

Kampuni hiyo ilikuwa ikisimamia kazi za wasanii hao kama kurekodi nyimbo, kutengeneza albamu, kusimamia mauzo, utengenezaji wa video na mavazi. Wakati wasanii hao wanamaliza mkataba na Zizzou Entertainment, wimbo wa Don’t Give UP waliorekodi kwa pamoja, unabamba ile mbaya katika vituo mbalimbali vya televiseni na radio nchini. Pia Ngwea, Blu na Diamond wanatarajiwa kuonekana runingani na kusikika redioni soon kwenye kazi yao ya mwisho waliyoifanya ya kampuni hiyo

Mbunge wa Mbeya Mjini - Joseph Mbilinyi apinga ufanyikaji wa Tamasha La Fiesta 2011

Mbunge wa Mbeya Mjini Kupitia Chama cha Chadema Leo kupitia Page yake ya Facebook Ameandika ujumbe ambayo unapinga ufanyikaji wa Tamasha kubwa la Fiesta. Joseph Mbilinyi ambaye pia ni mwasisi wa mziki wa Bongo Flava aliandika Ujumbe Unaosomeka Hivi "
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...