Monday, June 24, 2013

Kitenge Maulid Kitenge atangaza kugombea ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CCM!


Mtangazaji maarufu wa kipindi cha michezo na taarifa ya habari ITV na Radio One, Kitenge Maulid Kitenge kwa kupitia mtandao wa Instagram na Twitter ametangaza kugombea ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CCM.
Kitenge anakuwa miongoni mwa watu maarufu na wasanii waliotangaza nia hiyo kama Soggy Dogg Hunter (CHADEMA, Segerea) na Afande Sele (CHADEMA, Morogoro).
Aidha, kuna tetesi kuwa huenda wasanii MwanaFA (CCM) na Prof Jay (CHADEMA) wakatangaza nia bila kumsahau msanii wa Bongo movie Ray Kigosi.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...