Wiki
 iliyopita tuliongea katika leo tena juu ya kisa cha Marehemu Nasra 
pichani.Mama huyu alikuwa mkazi wa Bunda mkoani Mara lakini Dar es 
salaam alifika kufanya matibabu katika hospital ya Muimbili.Kwa miaka 
takribani 23 alikuwa mke wa bwana Elia Makumbati na kujaaliwa kupata 
watoto wanne mkubwa kabisa yupo chuo kikuu cha UDOM.Kwa miaka yote 
wamekuwa na misuko suko sana kwenye ndoa mama akiwa anapigwa sana hata 
kuchanwa na viwembe.
 Mwezi
 wa pili walitofautiana baada ya bwana kuoa mke mwingine.Wakiwa 
wametofautiana na Nasra kuendelea na maisha siku hiyo bwana akamfata 
akamkuta barabarani anatoka kazini.Akiwa na rafiki yake wanatembea 
akamfungia breki mguuni akamwambia anataka kuongea nae.Nasra akakataa 
akamwambia kama kuna maongezi hawezi kuongea nae kama vipi amfate 
nyumbani huku anaendelea kutembea.Bwana yule akamfata kwa nyuma 
akamgonga na gari na baada ya Nasra kuanguka akanasa chini hivyo 
kuendelea kumburuza umali wa kama mita 150 hivi.Alipofika kwenye tuta 
akanasuka bwana ndio kushuka kwenye gari kukimbia.
Kiukweli aliumia sana sana ngozi yote ya mgongoni,mbavuni,makalio,ikavuka na kubaki kwenye lami.Sikio lake la kushoto lote likaliwa na lami,mbavu 7 zilivunjika pamoja na mguu.Akapelekwa hospitali na baadae kulazwa Bugando Mwanza lakini ikawa anahitajika kuhamishiwa hospital ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.Akiwa muhimbili alikuwa na hali mbaya sana baadae ikathibitika kuwa ameumia ndani kwa ndani kwani alibadilika sana akavimba na kuwa mweusi.Kwamuda wote wa miezi takribani sita alikuwa katika maumivu makali na bahati mbaya hakuweza kupambana tena kupigania maisha yake.
Nasra pichani kulia mwenye kilemba chekundu akiwa na ndugu zake wakati akiwa mzima.
Usiku wa kuamkia jumanne ya 
tarehe 10 Nasra akaaga dunia.Ilikuwa ni huzuni sana jinsi alivyoteseka 
na namna mazingira ya kifo chake kilivyotokea.Tulikuwa na matumaini kuwa
 angeweza kupona maana dakika za mwisho alikuwa anaongea japo kwa shida.
Tunaomba mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Nasra mahala pema peponi,Amina.
                                            SOURCE    http://dinamarios.blogspot.com




 
 









 
 
 
 
