Huyu ni Nizar Khalifan kijana ambaye amzaliwa Juni 21, 1988 katika mkoa wa Mtwara,Tanzania. Ana urefu wa futi 5 na inchi 8 pia ancheza nafasi ya kiungo katika timu yake ya Vancouver Whitecaps FC na jezi namba 16.
Alikotokea;
Nizar alianzana timu yake ya mtaani ambayo ilikuwa ikiitwa West Ham kama ile ya England ambapo kiponeekana kipaji chake. Mwaka 2005-2007 alijiunga na Mtibwa Sugar ya Morogoro na hapo alicheza mechi 57 na kushinda magoli 16. Safari haikuishia hapo ndipo alipo amua kwenda kutafuta timu nje ya akajiunga na Al Tadamon mwaka 2007 na huko nako aliweza kuifungia timu yake hiyio goli 1 kati ya mechi 18 alizocheza. M waka 2008 Nizar alijiunga na Tadamon Sour alipoichezea mechi 25 na kushinda magoli 2. Ndipo alipoamua kurudi nyumbani na kujiunga na Moro Unuite ya mkoani Morogoro hapo napo aliichezea Moro mechi 31 na kupachika goli 7. Huyo ndiye Nizar Khalfan aliyedumu katika timu ya taifa ya Tanzania(Taifa Stars) chini ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Marcio Maximo. Hakuna atakaye sahau shuti alilopiga kwa umbali takribani mita 36 ambopo Tanzania ilipocheza na Senegali katika uwanja wa CCM Kirumba Jiji Mwanza pia alipomduaza kipa wa timu hiyo Tony Silva, mpaka mpira unaisha Tanzania 1-1 Senegali.
Henry Joseph Shindika ndio jina lake kamili ambaya alizaliwa Jiji ni Mwanza 3 novemba, 1985. hivi sasa anakipiga huko Norway kwenye klabu ya Kongsvinger. Anacheza nafasi ya kiungo na anavaa jezi namba 2.
Alikotokea;
Henry Joseph alianza kucheza Simba SC ambayo maskani yake yapo mjini katika mtaa wa Msimbazi mnamo mwaka 2006-2008, kwa muda mrefu alikuwa kapteni wa timu hiyo ya Simba. Pia ameichezea timu ya Tiafa mechi zaidi ya 25.
Danny Mrwanda kijana wa kitanzania ambaye alizaliwa Jijini Arusha, mwaka 1983 April 6 ambaye ana urefu wa futi 6 na inchi 1, anacheza nafasi ya mshambiliaji katika timu yake ya Dong Tam Long An ya Veitnam.
Alikotokea;
Mwaka 2006-2008 Danny alichezea Simba SC baada ya kutokea Arusha. ndipo 2008-2009 alipo jiunga na timu ya Al Tadamon. Danny Mrwanda alirudi Simba msimu wa mwaka 2009-2010. Baada ya hapo alijiunga na klabu yake ya sasa ya huko Veitnam. Pia amechezea timu ya Taifa zaidi ya mechi 24 na kufanikiwa kufunga magoli 9.
Abdi Kassim Babi au ukipenda unaweza muita Ballack wa Unguja kama Wanzanzibar wanavyopenda kumuita. Alizaliwa 19 Octoba 1984 huko visiwa vya karafuu , Zanzibar. Sasa ni mchezaji wa timu ya Dong Tam long An ya Veitnam.
Alikotokea;
Babi ametoke visiwani Zanzibar akajiunga na Yanga ya Dar es Salaam ambayo ina maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani, alisaini kujiunga na timu yake sasa mwaka 2011 kwa mkataba wa miaka miwili. Hakuna atakae bisha Babi ni mmoja kati ya wachezaji wenye mashuti katika kikosi cha timu ya Taifa y Tanzania, hasa alipo piga shuti kali la umbali takribani mita 35 kuelekea langoni mwa kipa wa Uganda na kujaa wavuni kwenye mechi ya kirafiki katika ufunguzi wa uwanja mpya wa Taifa wa Dar es Salaam. Mechi iliyoisha kwa Tanzania kutoka kifua mbele kwa goli moja kwa bila , ama kwa hakika usiku ule tulienda kuangalia shuti la Abdi Kassim Babi kijana kutokaka visiwa vya karafuu, Zanzibar.
Hashim Thabit Manka ni mcheza kikapu katika ligi ya Marekani maarufu kama NBA alizaliwa mwaka 1987 februari 16 Jiji Dar es Salaam maeneo ya sinza, ni mceza kikapu kwenye timu ya Houston Rockets ya NBA. Ana urefu wa futi 7 na inch 3 na uzito wa kilo 119
Alikotokea;
Alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Makongo kabla ya kwenda kusoma Marekani na kuanza kucheza na mchezo huo wa kikapu ambao alikuwa akicheza tangu alipokuwa huku katika timu yake ya mtaani. Huko ndipo alipopata nafasi katika timu ya chuo na timu za NBA kummezea mate. Huyo ndio Hasheem Thabeet Manka mtoto wa Sinza kwa wajanja.
Tuesday, August 2, 2011
WANAMICHEZO WA TANZANIA WANAOTESA NJE YA ARDHI YAO.
Posted by
Feel At Home
at
Tuesday, August 02, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Wednesday, July 27, 2011
Batista aondolewa ukocha wa Argentina
Sergio Batista amekubali kuacha ukocha wa timu ya taifa ya Argentina baada ya nchi hiyo kutolewa hatua ya robo fainali ya kuwania kombe la Copa America.
Sergio Batista
Wenyeji Argentina walitolewa na mabingwa Uruguay kwa mikwaju ya penalti.
Batista, mwenye umri wa miaka 48, amekuwa akiifundisha Argentina kwa mwaka mmoja sasa, awali akiwa kocha wa muda, baada ya Diego Maradona kutimuliwa kufuatia kutolewa katika Kombe la Dunia mwaka 2010.
Msemaji wa Chama cha Soka cha Argentina (AFA) amesema Batista hajatimuliwa, lakini imeamuliwa "kutengua" mkataba wake.
Argentina, ambayo mara ya mwisho kunyakua kombe muhimu ilikuwa mwaka 1993 waliposhinda mashindano ya Copa America, wamefuta mechi ya kirafiki dhidhi ya Romania mjini Bucharest iliyopangwa kuchezwa tarehe 10 mwezi wa Agosti.
"Makocha wa Argentina kwa viwango vyote wanafanyiwa tathmini na tume ta makocha wa taifa," aliongeza Bialo.
"Hakuna muda maalum uliowekwa, hakuna sababu ya kuharakisha kumchagua kocha mpya, kwa hiyo kuna mchakato wa kuwasoma na kuwafikiria makocha."
Source--bbcswahili.com
Sergio Batista
Wenyeji Argentina walitolewa na mabingwa Uruguay kwa mikwaju ya penalti.
Batista, mwenye umri wa miaka 48, amekuwa akiifundisha Argentina kwa mwaka mmoja sasa, awali akiwa kocha wa muda, baada ya Diego Maradona kutimuliwa kufuatia kutolewa katika Kombe la Dunia mwaka 2010.
Msemaji wa Chama cha Soka cha Argentina (AFA) amesema Batista hajatimuliwa, lakini imeamuliwa "kutengua" mkataba wake.
Argentina, ambayo mara ya mwisho kunyakua kombe muhimu ilikuwa mwaka 1993 waliposhinda mashindano ya Copa America, wamefuta mechi ya kirafiki dhidhi ya Romania mjini Bucharest iliyopangwa kuchezwa tarehe 10 mwezi wa Agosti.
"Makocha wa Argentina kwa viwango vyote wanafanyiwa tathmini na tume ta makocha wa taifa," aliongeza Bialo.
"Hakuna muda maalum uliowekwa, hakuna sababu ya kuharakisha kumchagua kocha mpya, kwa hiyo kuna mchakato wa kuwasoma na kuwafikiria makocha."
Source--bbcswahili.com
Posted by
Feel At Home
at
Wednesday, July 27, 2011
1 comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Barclays Msimamo wa Ligi Kuu ya England
Jumatano, 27 Julai 2011 00:00 UK
| Position | Timu | M | TG | PNT |
|---|---|---|---|---|
| Full Barclays Msimamo wa Ligi Kuu ya England | ||||
| 1 | Arsenal | 0 | 0 | 0 |
| 2 | Aston Villa | 0 | 0 | 0 |
| 3 | Blackburn | 0 | 0 | 0 |
| 4 | Bolton | 0 | 0 | 0 |
| 5 | Chelsea | 0 | 0 | 0 |
| 6 | Everton | 0 | 0 | 0 |
| 7 | Fulham | 0 | 0 | 0 |
| 8 | Liverpool | 0 | 0 | 0 |
| 9 | Man City | 0 | 0 | 0 |
| 10 | Man Utd | 0 | 0 | 0 |
| 11 | Newcastle | 0 | 0 | 0 |
| 12 | Norwich | 0 | 0 | 0 |
| 13 | QPR | 0 | 0 | 0 |
| 14 | Stoke | 0 | 0 | 0 |
| 15 | Sunderland | 0 | 0 | 0 |
| 16 | Swansea | 0 | 0 | 0 |
| 17 | Tottenham | 0 | 0 | 0 |
| 18 | West Brom | 0 | 0 | 0 |
| 19 | Wigan | 0 | 0 | 0 |
| 20 | Wolves | 0 | 0 | 0 |
Posted by
Feel At Home
at
Wednesday, July 27, 2011
1 comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Mubarak wa Misri 'agoma kula'
Aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak ni dhaifu na amegoma kula, kulingana na shirika rasmi la habari nchini humo.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo, akituhumiwa na makosa ya rushwa na kuamuru kufanyika kwa mauaji ya waandamanaji.Mkuu wa hospitali ambapo Bw Mubarak ameshikiliwa huko Sahrm al-Sheikh amesema alikuwa mnyonge, amepungua uzito, na hakuwa akila vya kutosha kumweka hai, shirika la MENA limeripoti.
Lakini wakosoaji wamesema ugonjwa wa Bw Mubarak ni kama njama ya kuepuka kufikishwa mahakamani.
Wafuasi wa upinzani wanatia shaka ripoti hiyo. Wanaamini mamlaka husika zinajaribu tu kuzuia kuanza kwa kesi ya Bw Mubarak, inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Miongoni mwa ripoti nyingi zilizotolewa kuhusu afya ya Bw Mubarak ya hivi karibuni imesema madaktari wake wataamua katika saa za hivi karibuni, iwapo ulaji wake wa hivi sasa hautoshi kumweka hai.
Mwandishi wa BBC Cairo, Jon Leyne, alisema, sasa hivi kuna ushahidi unaozidi kuibuka kwamba ni mtu anayedhoofika kadri siku zinavyoendelea.
Bw Mubarak alipinduliwa mwezi Februari katika ghasia maarufu zilizosababisha vifo vya zaidi ya watu 840.
Source--bbcswhili.com
Posted by
Feel At Home
at
Wednesday, July 27, 2011
1 comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Pembe za ndovu zachomwa Kenya
Tani tano za pembe za ndovu zilizopatikana kwa njia haramu zimechomwa moto Kenya. Wazir Khamsin wa BBC alishuhudia shughuli hiyo.
Source--bbcswhili.com
Posted by
Feel At Home
at
Wednesday, July 27, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Sunday, July 24, 2011
Tanzania yanyong'onyea
Hali ya umeme nchini Tanzania kwa sasa inazidi kuwa si nzuri baada ya maeneo yanayotoa umeme wa maji kukaukiwa na maji kabisa hasa bwawa kubwa la Mtera. Wakati huu baadhi ya maeneo yanapata umeme kwa mgao kwa saa zisizozidi sita kwa siku. Hali hiyo imeathiri maisha ya kila siku ya watu na pia uchumi. Charles Hilary alizungumza na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ambaye ni mbunge wa Ubungo kupitia chama cha CHADEMA Mheshimiwa John Mnyika, mwanzo akitaka kujua kama kweli nchi hiyo inatarajiwa kuingia katika kipindi kigumu zaidi cha kukosekana umeme na nchi kuwa giza?
Kufahamu hali halisi ilivyo baada ya kutangazwa kuongezeka kwa mgao wa umeme nchini humo, Charles Hilary pia alizungumza na Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania Badra Masoud.Mwandishi wa bbc John Solombi kutoka Dar es Salaam naye alituma taarifa kuhusu athari ya mgao huo uliosababisha viwanda sita kufungwa na takriban wafanyakazi 7000 kutolewa katika ajira zao. Utafiti umefanywa na shirikisho la viwanda nchini Tanzania.
Posted by
Feel At Home
at
Sunday, July 24, 2011
2
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
KIM NA KRIS KUFUNGA NDOA
Kim Kardashian and Kris humphrier
Mwanamitndo kim kardashia anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake kris humphrier ambaye ni mchezaji wa kikapu nchini marekani. Kim na kris wanatarajia kufunga ndoa ya agost 20, mwaka huu. Kardashian ametua jijin los angeles ili kuendelea na shughuli za maandalizi ya harusi yao na humphries. Hata hivyo kardashia alifanya mahojiano mengi na waandishi wa habair jijini new york kabla ya kwenda los angeles. Kardashian alisema ''kwa kweil nimekuwa na ndoto ya kuolewa tangu nikiwa mdogo.
Posted by
Feel At Home
at
Sunday, July 24, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Hammam kukata rufaa
Aliyekuwa rais wa shirikisho la mchezo wa soka barani Asia, Mohamed Bin Hammam, anatarajiwa kukata rufaa dhidi ya marufuku ya maisha ya kutoshiriki katika shughuli zozote za mchezo huo, aliyopewa na shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA.
Aliyekuwa rais wa shirikisho la mchezo wa soka barani Asia, Mohammed Bin Hammam
Katika mtandao wake, Bin Hammam, ametaja matukio ya hivi karibuni kama mapambano katika vita vinavyoendelea.
Vile vile amechapisha barua inayopongeza juhudi zake, katika shirikisho hilo iliyoandikwa mwaka wa 2008 na rais wa FIFA, Sepp Blatter.
Chini ya barua hiyo kuna mstari unaosema "Hii ni mapambano na sio vita vyenyewe".
Posted by
Feel At Home
at
Sunday, July 24, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Hammam apigwa marufuku maisha
Mkuu wa soka barani Asia, Mohamed Bin Hammam, leo amepigwa marufuku asishiriki katika shughuli za soka katika maisha yake yote.
Hii ni baada ya shirikisho la soka duniani, FIFA, kumpata na hatia ya kosa la kutoa hongo, kabla ya uchaguzi wa rais wa shirikisho hilo mwezi uliopita.
Uamuzi uliotolewa Jumamosi ni kufuatia kikao cha maadili cha FIFA nchini Uswisi, mkutano ambao ulifanyika katika kipindi cha siku mbili.Bin Hammam, raia wa Qatar, tarehe 29 Mei alijiondoa katika kuwania urais wa FIFA, na siku tatu baadaye, Sepp Blatter, mwananchi wa Uswisi, alichaguliwa tena pasipo kupingwa, kuliongoza shirikisho hilo kwa awamu nyingine ya nne.
Posted by
Feel At Home
at
Sunday, July 24, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Friday, July 22, 2011
Hatimae Langa kuachana kabisa na matumizi ya madawa yakulevya
Msanii mwenye heshima kubwa kwenye muziki wa Hip Hop Tanzania mtu mzima Langa ambae kwa muda mrefu alikua amejikita kwenye matumizi ya madawa ya kulevya (Unga) Leo hii ametimba ndani ya the people's station Clouds FM kwenye kipindi cha XXL akiwa ameweza kutambulisha ujio wake mpya kwenye game na pia kutoa tamko rasmi kua kwasasa amefanikiwa kujitoa kwenye matumizi ya madawa ambayo yalimtesa kwa muda wa miaka zaidi ya mitano na kueleza mipango yake ya kuanzisha rehab yake mwenyewe ambayo itaweza kusaidia vijana ambao wanapitia matatizo ambayo yeye ameyapitia na akaweza kujitoa....................................
Posted by
Feel At Home
at
Friday, July 22, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Wednesday, July 13, 2011
ROSTAM AZIZ HAACHA UBUNGE WA IGUNGA-TABORA NA UJUMBE WA HALMASHAURI KUUYA TAIFA (CCM)
Mbunge wa Igunga mkoani Tabora kupitia ccm ameajiudhuru nafasi zote za kisiasa kubwa alizokuanazo mwazoni.Mbunge huyo wa ccm ameitisha mkutano leo jimboni kwake nakuanza kuwaelezea maamuzi mazito aliyokuwanayo,ata hivyo amesema uwamuzi wake autokani na kauli ya hivi kalibuni ya chama chake ya 'Kujivua gambamba' bali ni utashu wake binafsi na kuamua kuendelea na biashara zake.Ata hivyo amakua akiusishwa sana na ufisadi kwa kiasi kikubwa.
Posted by
Feel At Home
at
Wednesday, July 13, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Tuesday, June 21, 2011
NGWEA, STEVE, SQUEEZER BASI ZIZZOU ENTERTAINMENT
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo waliokuwa chini ya Lebo ya Zizzou Entertainment, Albert Mangwea ‘Ngwair’, Steve RnB, Edson William ‘Baby Boy’, Squeezer na Mzee Zahir Zorro wamemaliza mkataba wao wa awali na kampuni hiyo na sasa wako huru kwenda lebo nyingine.
Akipiga stori na Showbiz, Mkurugenzi wa kampuni hiyo inayoibua na kuendeleza vipaji vya wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Tippo Athuman, aliweka plain kuwa mkataba na wasanii hao umeisha tangu Machi mwaka huu na kwamba hana mpango wa kuingia nao mkataba mwingine.

Tippo Athumani
Akipiga stori na Showbiz, Mkurugenzi wa kampuni hiyo inayoibua na kuendeleza vipaji vya wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Tippo Athuman, aliweka plain kuwa mkataba na wasanii hao umeisha tangu Machi mwaka huu na kwamba hana mpango wa kuingia nao mkataba mwingine.
ZAHIR ZORRO
“Mkataba wao uliisha tangu Machi mwaka huu na hakuna mpango wa kuingia nao mkataba mpya, naangalia uwezekano wa kuibua vipaji vingine, kwa sasa wanaruhusiwa kuwa chini ya mtu au kampuni nyingine,” alisema Tippo.

Tippo Athumani
Kampuni hiyo ilikuwa ikisimamia kazi za wasanii hao kama kurekodi nyimbo, kutengeneza albamu, kusimamia mauzo, utengenezaji wa video na mavazi. Wakati wasanii hao wanamaliza mkataba na Zizzou Entertainment, wimbo wa Don’t Give UP waliorekodi kwa pamoja, unabamba ile mbaya katika vituo mbalimbali vya televiseni na radio nchini. Pia Ngwea, Blu na Diamond wanatarajiwa kuonekana runingani na kusikika redioni soon kwenye kazi yao ya mwisho waliyoifanya ya kampuni hiyo
Posted by
Feel At Home
at
Tuesday, June 21, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Mbunge wa Mbeya Mjini - Joseph Mbilinyi apinga ufanyikaji wa Tamasha La Fiesta 2011
Mbunge wa Mbeya Mjini Kupitia Chama cha Chadema Leo kupitia Page yake ya Facebook Ameandika ujumbe ambayo unapinga ufanyikaji wa Tamasha kubwa la Fiesta. Joseph Mbilinyi ambaye pia ni mwasisi wa mziki wa Bongo Flava aliandika Ujumbe Unaosomeka Hivi "
Posted by
Feel At Home
at
Tuesday, June 21, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Friday, June 17, 2011
RATIBA LIGI KUU WINGEREZA
| Opening weekend - Saturday, 13 August |
| Blackburn v Wolves |
| Fulham v Aston Villa |
| Liverpool v Sunderland |
| Manchester City v Swansea |
| Newcastle v Arsenal |
| QPR v Bolton |
| Stoke v Chelsea |
| Tottenham v Everton |
| West Bromwich Albion v Manchester United |
| Wigan v Norwich |
| Saturday, 20 August |
| Arsenal v Liverpool |
| Aston Villa v Blackburn |
| Bolton v Manchester City |
| Chelsea v West Bromwich Albion |
| Everton v QPR |
| Manchester United v Tottenham |
| Norwich v Stoke |
| Sunderland v Newcastle |
| Swansea v Wigan |
| Wolves v Fulham |
| Saturday, 27 August |
| Aston Villa v Wolves |
| Blackburn v Everton |
| Chelsea v Norwich |
| Liverpool v Bolton |
| Manchester United v Arsenal |
| Newcastle v Fulham |
| Swansea v Sunderland |
| Tottenham v Manchester City |
| West Bromwich Albion v Stoke |
| Wigan v QPR |
Kwa msaada wa ;BBC Sport-Premier league fixtures
Posted by
Feel At Home
at
Friday, June 17, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
AJALI! AJALI!
Mida ya asubuhi katika barabara ya Bagamoyo kulitokae ajali iliyohusisha Gari ya abiria aina ya ISUZU na TAXI. Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa pikipiki alimaalufu kama bodaboda na dereva wa bajaji. Dereva wa TAXI aliwaishwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Posted by
Feel At Home
at
Friday, June 17, 2011
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook




















