Tuesday, August 2, 2011

WANAMICHEZO WA TANZANIA WANAOTESA NJE YA ARDHI YAO.

Huyu ni Nizar Khalifan kijana ambaye amzaliwa Juni 21, 1988  katika mkoa wa Mtwara,Tanzania. Ana urefu wa futi 5 na inchi 8 pia ancheza nafasi ya kiungo katika timu yake ya Vancouver Whitecaps FC na jezi namba 16.

Alikotokea;
Nizar alianzana timu yake ya mtaani ambayo ilikuwa ikiitwa West Ham kama ile ya England  ambapo kiponeekana kipaji chake. Mwaka 2005-2007 alijiunga na Mtibwa Sugar ya Morogoro na hapo alicheza mechi 57 na kushinda magoli 16. Safari haikuishia hapo ndipo alipo amua kwenda kutafuta timu nje ya akajiunga na Al Tadamon mwaka 2007 na huko nako aliweza kuifungia timu yake hiyio goli 1 kati ya mechi 18 alizocheza. M waka 2008 Nizar alijiunga na  Tadamon Sour alipoichezea mechi 25 na kushinda magoli 2. Ndipo alipoamua kurudi nyumbani na kujiunga na Moro Unuite ya mkoani Morogoro hapo napo aliichezea Moro  mechi 31 na kupachika goli 7. Huyo ndiye Nizar Khalfan aliyedumu katika timu ya taifa ya Tanzania(Taifa Stars) chini ya aliyekuwa  kocha wa timu hiyo Marcio Maximo. Hakuna atakaye sahau shuti alilopiga kwa umbali takribani mita 36 ambopo Tanzania ilipocheza  na Senegali katika uwanja wa CCM Kirumba Jiji Mwanza pia alipomduaza kipa wa timu hiyo Tony Silva, mpaka mpira unaisha Tanzania 1-1 Senegali. 


Henry Joseph Shindika ndio jina lake kamili ambaya alizaliwa Jiji ni Mwanza 3 novemba, 1985. hivi sasa anakipiga huko Norway kwenye klabu ya Kongsvinger. Anacheza nafasi ya kiungo na anavaa jezi namba 2.

Alikotokea; 
Henry Joseph alianza kucheza Simba SC ambayo maskani yake yapo mjini katika mtaa wa Msimbazi mnamo mwaka 2006-2008, kwa muda mrefu alikuwa kapteni wa timu hiyo  ya Simba. Pia ameichezea timu ya Tiafa mechi zaidi ya 25. 


Danny Mrwanda kijana wa kitanzania ambaye alizaliwa Jijini Arusha, mwaka 1983 April 6 ambaye ana urefu wa futi 6 na inchi 1, anacheza nafasi ya mshambiliaji katika timu yake ya Dong Tam Long An ya Veitnam.

Alikotokea;
Mwaka 2006-2008 Danny alichezea Simba SC baada ya kutokea Arusha. ndipo 2008-2009 alipo jiunga na timu ya Al Tadamon. Danny Mrwanda alirudi Simba msimu wa mwaka 2009-2010. Baada ya hapo alijiunga na klabu yake ya sasa ya huko Veitnam. Pia amechezea timu ya Taifa zaidi ya mechi 24 na kufanikiwa kufunga magoli 9.


Abdi Kassim Babi au ukipenda unaweza muita  Ballack wa Unguja kama Wanzanzibar wanavyopenda kumuita. Alizaliwa 19 Octoba 1984 huko visiwa vya karafuu , Zanzibar. Sasa ni mchezaji wa timu ya Dong Tam long An ya Veitnam.

Alikotokea;
 Babi ametoke visiwani Zanzibar  akajiunga na Yanga ya Dar es Salaam ambayo ina maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani, alisaini kujiunga na timu yake sasa mwaka 2011 kwa mkataba wa miaka miwili. Hakuna atakae bisha Babi ni mmoja kati ya wachezaji wenye mashuti katika kikosi cha timu ya Taifa y Tanzania, hasa alipo piga shuti kali la umbali takribani mita 35 kuelekea langoni mwa kipa wa  Uganda na kujaa wavuni kwenye mechi ya kirafiki katika ufunguzi wa uwanja mpya wa Taifa wa  Dar es Salaam. Mechi iliyoisha kwa  Tanzania kutoka kifua mbele kwa goli moja kwa bila , ama kwa hakika usiku ule tulienda kuangalia shuti la Abdi Kassim Babi kijana kutokaka visiwa vya karafuu, Zanzibar. 



Hashim Thabit Manka ni mcheza kikapu katika ligi ya Marekani maarufu kama NBA alizaliwa mwaka 1987 februari 16 Jiji Dar es Salaam maeneo ya sinza, ni mceza kikapu kwenye timu ya Houston Rockets ya NBA. Ana urefu wa futi 7 na inch 3 na uzito wa kilo 119

Alikotokea;
Alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Makongo kabla ya kwenda kusoma Marekani na kuanza kucheza na mchezo huo wa kikapu ambao alikuwa akicheza tangu alipokuwa huku katika timu yake ya mtaani. Huko ndipo alipopata nafasi katika timu ya chuo na timu za NBA kummezea mate. Huyo ndio Hasheem Thabeet Manka mtoto wa Sinza kwa wajanja.

0 comments:

Post a Comment

CHANGIA MAWAZO YAKO HAPA

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...