Saturday, April 28, 2012

TUNDU LISSU MACHOZI PWAA! BAADA YA KUSHINDA KESI YA KUPINGA UBUNGE WAKE

    Mbunge wa singida nashariki (tundu lissu) akilia kwa furaha huku akibembelezwa na mbunge wa viti maalum kataru mkoa wa manyara (rose kamili),Baada ya mahakama kuu kutupia mbali pingamizi la kupinga matokeo yaliyompa ubunge lissu

 Lissu akifutwa machozi na mkewe wakati wakitoka nje ya mahakama mjini singida


Friday, April 27, 2012

WARAKA WA VICENT KIGOSI (RAY) KWA WATANZANIA JUU YA MSIBA WA KANUMBA

Waraka huo ulinaswa hivi karibuni kupitia blogu yake ambapo baada ya kuupitia tukaona ni vyema ukasomwa na Watanzania wote ili kuweza kupata jibu la kwa nini yeye hahusiki? Waraka huo ni huu hapa chini…

Yapata wiki tatu sasa tangu msanii mwenzangu Steven Kanumba aage dunia na kama ilivyo kwa kila kitu kinapotokea huandamana na kila aina ya maneno na hisia mbalimbali kutokana na mitazamo yawatu kupishana kuhusiana na jambo husika.
Kulingana na muktadha huo, msiba wa Steven Kanumba umekumbwa na maneno na hisia kama hizo, hususan mazingira ya kifo chake. Kinachosikitisha zaidi watu wengi (ambao wanajitambulisha kama wapenzi wa Kanumba) na baadhi ya vyombo binafsi vya habari vimekuwa vikinihusisha na kifo hicho kwa kusema kwamba kwa njia moja au nyingine nahusika na mauaji ya Steven Kanumba.


Kwa muda wote huo tangu msiba ulipotokea mpaka leo hii nashika kalamu kujaribu kuyaweka sawa na kuondosha hisia chafu katika fikra za watu. Nimekuwanikipitia katika wakati mgumu sana kwa jinsi ambavyo nimekuwa nikinyooshewa vidole kila upande nikihusishwa na kifo hicho.
Kiujumla nimezingatia maoni ya wapenzi na mashabiki wangu wakinitaka kuwa na subira ila kuna usemi usemao, uongo ukirudiwa sana jamii huusadiki na kuuona ukweli, nimeona nisikae kimya ila niweke sawa hili kwamba sihusiki na kifo cha Steven Kanumba.
Nasema wazi kwanza sihusiki kabisa na kifo cha Kanumba kwa kuzingatia mazingira yenyewe ya kifo kilivyotokea. Wakati kifo hicho kinatokea, nilikuwa sehemu nyingine kabisa na mimi nilikuwa mtu wa tatu kutaarifiwa kwamba Kanumba amepatwa na mkasa ambao baadaye ulisababisha kifo chake.


Hata nilipofika katika Hospitali ya Muhimbili (tofauti na watu wanavyodhani kuwa nilifika nyumbani kwake, ukweli mimi nilimkuta tayari amepelekwa Muhimbili), nilikuta tayari alikuwa ameshafariki ndiyo maana hata polisi wanaohusika na usalama wa raia, si tu kwamba hawakuniweka chini ya ulinzi, sikuitwa hata kuhojiwa kwa sababu hakunamazingira yoyote yanayonihusisha mimi nakifo hicho.


Kitu kikubwa kilichokuwa kinaendelea baina yetu ni kwamba tulijenga ushindani wa kuendeleza kazi mbele kwa kila mmoja akitoa kazi, mwingine anamjibu.


Watu wanaojaribu kuonesha kuwa tofauti zetu ilikuwa ni uadui, huwa hawajui wapi tulikotoka ndiyo maana wanasema wasemavyo na katika kuthibitisha kuwa tofauti hizo hazikufikia katika uadui

Kumtuhumu mtu kwa namna yoyote ile bila ya uthibitisho wa tuhuma hizo, ni kosa kwa sheria za nchi na pia kama ni mfuasi wa dini yoyote ni dhambi, kwani wakati ukisema hayo huku hujui uhalisia bali unasukumwa na nguvu za hisia tu ni sawa na kumchafua mtu huyo katika jamii bila ya kujua jamii inamchukuliaje.

Thursday, April 26, 2012

Wastara awaonya wanaomzushia kifo Sajuki



Na Gladness Mallya
KUFUATIA uvumi uliozagaa katika Jiji la Dar ukidai kwamba, msanii anayefanya vizuri kwenye gemu la sinema Bongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia, mkewe Wastara Juma ameibuka akiwataka wazushi hao kuacha mara moja tabia hiyo.

Uvumi huo ulizagaa kuanzia Jumamosi iliyopita huku watu kadhaa wakiandika kwenye kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa, staa huyo ameaga dunia.

Wastara mwenyewe alikiri kupokea simu nyingi kutoka ndani na nje ya nchi zikimpa pole kufuatia ‘kifo’ cha mumewe jambo ambalo alisema linamuumiza sana.

Aidha, Wastara alisema: “Sijui ni binadamu gani aliyeanza kusambaza uzushi huo, lakini nawaomba watu wanaotumia mitandao ya kijamii au kutumia ujumbe mfupi wa maneno kwa simu (sms) kuwa wastaarabu na wasichezee uhai wa mtu kwani mwenye uwezo huo ni Mungu pekee.”

chanzo-Global publisher

DIAMOND KUKAGUA HELIKOPTA ATAKAYOSHUKA NAYO DAR LIVE


 Diamond akiwa na wasanii wa kundi la Pah One wakielekea uwanjani.

 Diamond akiwa na wasanii wa kundi la Pah One juu ya helkopta.…

Kapteni wa helkopta hiyo, Nasser akisalimiana na Diamond.

Raisi wa wasafi Bongo, Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’ leo alikuwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere kukagua helkopta atakayoshuka nayo Jumapili hii ndani ya Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem.
Hbr Picha na Erick Evarist

Chanzo-Global publisher

Sunday, April 22, 2012

WABUNGE WALIVYOWEKA SAHIHI KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU (#VOTEOFNOCONFIDENCE)

 Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma juzi. Kulia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anayefanya zoezi la kukusanya sahihi za wabunge ili aweze kuwasilisha bungeni hoja kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, kesho Jumatatu.

Mbunge wa wa Kasulu Mjini, Moses Machali akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma juzi. Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Kusini, Zitto Kabwe anayetaka kuwasilisha bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma juzi.

Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma juzi.
Mbunge wa Bukombe, Prof Kulikoyela Kahigi akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Katikati ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.

Chanzo cha habari:www.globalpublisher.com

JACOB ZUMA AOA MKE WA SITA, NI BONGI NGEMA




 Hapa ni wakati wa ndoa ya kimila.

Zuma akiwa amevaa ngozi ya chui na kubeba ngao wakati wa harusi ya kimila.

RAIS wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, jana Jumamosi ameoa mke wa sita katika sherehe ya siku ya pili iliyopambwa kwa shamra za kabila la Wazulu. Rais huyo mwenye umri wa miaka 70 alimwoa Bongi Ngema siku ya Ijumaa katika mvumo wa nyimbo za Kizulu akiwa amevaa ngozi ya chui na kubeba ngao huku akiwa amezungukwa na wanaume waliokuwa wamvalia nguo za wapiganaji wa kijadi.

Msimamizi wa ndoa hiyo alikuwa ni mke wa nne wa Zuma aitwaye Nkandla katika sherehe iliyofanyika KwaZulu-Natal na kufuatiwa na sherehe za kisasa ambazo zilikuwa ni pamoja na kukata keki.

Zuma na Ngema wana mtoto wa miaka saba wa kiume. Ndoa hiyo ni ya tatu katika miaka minne iliyopita naya pili tangu ashike urais wa nchi hiyo mwaka 2009 akiwa rais mwenye wake wengi.

Kiongozi huyo ameoa mara sita na ana watoto 21 ambapo mmoja wa wake zake amekufa na mwingine ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Nkosazana Dlamini-Zuma – ametalikiana naye. Wanawake hao hufaidika kwa kusafiri na rais huyo na kufanya kazi za ukatibu mahsusi, pamoja na kufuatana naye katika ziara za kiserikali.

Pamoja na kwamba Zuma aligharimia ndoa hiyo yeye mwenyewe, serikali pia imeongeza bajeti yake maradufu kwa zaidi ya Dola milioni mbili kutokana na kumwoa mwanamke huyo akiwa mmoja wa familia yake.

Hata hivyo, ndoa ya wanawake wengi inaonekana kupoteza umaarufu nchini Afrika Kusini ambapo ustaarabu wa nchi za Magharibi unazidi kuota mizizi ambapo idadi kubwa ya watu wa nchi hiyo hawakubaliani na utamaduni huo hivi sasa.

Chanzo cha habari :www,global publisher.com
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...