Na Gladness Mallya
KUFUATIA uvumi uliozagaa katika Jiji la Dar ukidai kwamba, msanii anayefanya vizuri kwenye gemu la sinema Bongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia, mkewe Wastara Juma ameibuka akiwataka wazushi hao kuacha mara moja tabia hiyo.
Uvumi huo ulizagaa kuanzia Jumamosi iliyopita huku watu kadhaa wakiandika kwenye kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa, staa huyo ameaga dunia.
Wastara mwenyewe alikiri kupokea simu nyingi kutoka ndani na nje ya nchi zikimpa pole kufuatia ‘kifo’ cha mumewe jambo ambalo alisema linamuumiza sana.
Aidha, Wastara alisema: “Sijui ni binadamu gani aliyeanza kusambaza uzushi huo, lakini nawaomba watu wanaotumia mitandao ya kijamii au kutumia ujumbe mfupi wa maneno kwa simu (sms) kuwa wastaarabu na wasichezee uhai wa mtu kwani mwenye uwezo huo ni Mungu pekee.”
chanzo-Global publisher