Wednesday, July 27, 2011

Batista aondolewa ukocha wa Argentina

Sergio Batista amekubali kuacha ukocha wa timu ya taifa ya Argentina baada ya nchi hiyo kutolewa hatua ya robo fainali ya kuwania kombe la Copa America.

 
                                                             Sergio Batista
Wenyeji Argentina walitolewa na mabingwa Uruguay kwa mikwaju ya penalti.

Batista, mwenye umri wa miaka 48, amekuwa akiifundisha Argentina kwa mwaka mmoja sasa, awali akiwa kocha wa muda, baada ya Diego Maradona kutimuliwa kufuatia kutolewa katika Kombe la Dunia mwaka 2010.

Msemaji wa Chama cha Soka cha Argentina (AFA) amesema Batista hajatimuliwa, lakini imeamuliwa "kutengua" mkataba wake.

Argentina, ambayo mara ya mwisho kunyakua kombe muhimu ilikuwa mwaka 1993 waliposhinda mashindano ya Copa America, wamefuta mechi ya kirafiki dhidhi ya Romania mjini Bucharest iliyopangwa kuchezwa tarehe 10 mwezi wa Agosti.

"Makocha wa Argentina kwa viwango vyote wanafanyiwa tathmini na tume ta makocha wa taifa," aliongeza Bialo.

"Hakuna muda maalum uliowekwa, hakuna sababu ya kuharakisha kumchagua kocha mpya, kwa hiyo kuna mchakato wa kuwasoma na kuwafikiria makocha."


Source--bbcswahili.com

Barclays Msimamo wa Ligi Kuu ya England

Jumatano, 27 Julai 2011 00:00 UK

PositionTimuMTGPNT
Full Barclays Msimamo wa Ligi Kuu ya England
1Arsenal000
2Aston Villa000
3Blackburn000
4Bolton000
5Chelsea000
6Everton000
7Fulham000
8Liverpool000
9Man City000
10Man Utd000
11Newcastle000
12Norwich000
13QPR000
14Stoke000
15Sunderland000
16Swansea000
17Tottenham000
18West Brom000
19Wigan000
20Wolves000

Mubarak wa Misri 'agoma kula'

Aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak ni dhaifu na amegoma kula, kulingana na shirika rasmi la habari nchini humo.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo, akituhumiwa na makosa ya rushwa na kuamuru kufanyika kwa mauaji ya waandamanaji.

Mkuu wa hospitali ambapo Bw Mubarak ameshikiliwa huko Sahrm al-Sheikh amesema alikuwa mnyonge, amepungua uzito, na hakuwa akila vya kutosha kumweka hai, shirika la MENA limeripoti.

Lakini wakosoaji wamesema ugonjwa wa Bw Mubarak ni kama njama ya kuepuka kufikishwa mahakamani.

Wafuasi wa upinzani wanatia shaka ripoti hiyo. Wanaamini mamlaka husika zinajaribu tu kuzuia kuanza kwa kesi ya Bw Mubarak, inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Miongoni mwa ripoti nyingi zilizotolewa kuhusu afya ya Bw Mubarak ya hivi karibuni imesema madaktari wake wataamua katika saa za hivi karibuni, iwapo ulaji wake wa hivi sasa hautoshi kumweka hai.

Mwandishi wa BBC Cairo, Jon Leyne, alisema, sasa hivi kuna ushahidi unaozidi kuibuka kwamba ni mtu anayedhoofika kadri siku zinavyoendelea.

Bw Mubarak alipinduliwa mwezi Februari katika ghasia maarufu zilizosababisha vifo vya zaidi ya watu 840.

Source--bbcswhili.com

Pembe za ndovu zachomwa Kenya

Tani tano za pembe za ndovu zilizopatikana kwa njia haramu zimechomwa moto Kenya. Wazir Khamsin wa BBC alishuhudia shughuli hiyo.

Source--bbcswhili.com

Sunday, July 24, 2011

Tanzania yanyong'onyea

'

Hali ya umeme nchini Tanzania kwa sasa inazidi kuwa si nzuri baada ya maeneo yanayotoa umeme wa maji kukaukiwa na maji kabisa hasa bwawa kubwa la Mtera. Wakati huu baadhi ya maeneo yanapata umeme kwa mgao kwa saa zisizozidi sita kwa siku. Hali hiyo imeathiri maisha ya kila siku ya watu na pia uchumi. Charles Hilary alizungumza na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ambaye ni mbunge wa Ubungo kupitia chama cha CHADEMA Mheshimiwa John Mnyika, mwanzo akitaka kujua kama kweli nchi hiyo inatarajiwa kuingia katika kipindi kigumu zaidi cha kukosekana umeme na nchi kuwa giza?
Kufahamu hali halisi ilivyo baada ya kutangazwa kuongezeka kwa mgao wa umeme nchini humo, Charles Hilary pia alizungumza na Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania Badra Masoud.

Mwandishi wa bbc John Solombi kutoka Dar es Salaam naye alituma taarifa kuhusu athari ya mgao huo uliosababisha viwanda sita kufungwa na takriban wafanyakazi 7000 kutolewa katika ajira zao. Utafiti umefanywa na shirikisho la viwanda nchini Tanzania.

KIM NA KRIS KUFUNGA NDOA

                                  

Kim Kardashian and Kris humphrier
 Mwanamitndo kim kardashia anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake kris humphrier ambaye ni mchezaji wa kikapu nchini marekani. Kim na kris wanatarajia kufunga ndoa ya agost 20, mwaka huu. Kardashian ametua jijin los angeles ili kuendelea na shughuli za maandalizi ya harusi yao na humphries. Hata hivyo kardashia alifanya mahojiano mengi na waandishi wa habair jijini new york kabla ya kwenda los angeles. Kardashian alisema ''kwa kweil nimekuwa na ndoto ya kuolewa tangu nikiwa mdogo.

Hammam kukata rufaa

Aliyekuwa rais wa shirikisho la mchezo wa soka barani Asia, Mohamed Bin Hammam, anatarajiwa kukata rufaa dhidi ya marufuku ya maisha ya kutoshiriki katika shughuli zozote za mchezo huo, aliyopewa na shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA.
                     Aliyekuwa rais wa shirikisho la mchezo wa soka barani Asia, Mohammed Bin Hammam

Bin Hammam ambaye anatoka Qatar, alipewa hukumu hiyo kufuatia tuhuma za kununua kura wakati wa uchaguzi wa urais wa FIFA ambao alikuwa mmoja wa wagombea wa kiti cha urais.
Katika mtandao wake, Bin Hammam, ametaja matukio ya hivi karibuni kama mapambano katika vita vinavyoendelea.
Vile vile amechapisha barua inayopongeza juhudi zake, katika shirikisho hilo iliyoandikwa mwaka wa 2008 na rais wa FIFA, Sepp Blatter.
Chini ya barua hiyo kuna mstari unaosema "Hii ni mapambano na sio vita vyenyewe".

Hammam apigwa marufuku maisha

Mkuu wa soka barani Asia, Mohamed Bin Hammam, leo amepigwa marufuku asishiriki katika shughuli za soka katika maisha yake yote.

Hii ni baada ya shirikisho la soka duniani, FIFA, kumpata na hatia ya kosa la kutoa hongo, kabla ya uchaguzi wa rais wa shirikisho hilo mwezi uliopita.
Uamuzi uliotolewa Jumamosi ni kufuatia kikao cha maadili cha FIFA nchini Uswisi, mkutano ambao ulifanyika katika kipindi cha siku mbili.
Bin Hammam, raia wa Qatar, tarehe 29 Mei alijiondoa katika kuwania urais wa FIFA, na siku tatu baadaye, Sepp Blatter, mwananchi wa Uswisi, alichaguliwa tena pasipo kupingwa, kuliongoza shirikisho hilo kwa awamu nyingine ya nne.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...