Saturday, July 21, 2012

Mtoto wa kambo wa msanii Usher Rymond afariki dunia


Tumepata habari ya kustusha kua mtoto wa kiume wa Tameka Raymond ambae ni mtoto wa kambo wa Msanii usher rymond amefarki dunia siku ya leo.Mtoto huyo aliekua na miaka 11 amefariki kutokan kufatia majeraha aliyokua nayo mtoto huyo yaliyotokana na ajali mbaya aliypiapata mapema mwezi huu.

Daktari aliekua anamtibia mtoto huyo aliamua kuondoa mchine maalum iliyokua inamsaidia kupumua mtoto huyo baada ya daktari kuona majeraha hayo yalikua makubwa sana kwa mtoto huyo kuweza kupona

Glover alipata ajali ya piki piki za majini siku ya tarehe 8 mwezi huu kufuatia kugongana na mwenzie ambae alipoteza muelekeo wa piki piki yake.

Jana Tameka alitweet single moja ya mtoto huyo akiwa na mdogo wake cinco ambae ni mtoto wa usher rymond.

Huyu ndie mbongo anaemiliki "Lamborghini" yenye thamani ya Bilioni moja!!!!!



Na Wilbert Molandi

“HII sasa ni kufuru!” Hivi ndivyo utakavyoweza kusema kwa Davies Mosha ambaye ni makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, ambaye nafasi yake kwa sasa klabuni hapo inashikiliwa na Clement Sanga.
Kwa tafsiri ya haraka, yawezekana Mosha anaweza kuwa ndiye kiongozi pekee wa soka nchini kumiliki gari la kifahari na lenye gharama kubwa aina ya Lamborghini kama ambalo linamilikiwa na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.


Gari analomiliki Mosha ambalo lina rangi ya njano, linaaminika kuwa miongoni mwa magari yenye thamani kubwa siyo tu Tanzania na Afrika, bali duniani kote, kwani hata siku Rooney alipolinunua wenzake wengi hawakutegemea, siyo kwa sababu hana fedha, ila kwa kuwa hakuwa mtu wa matumizi ya magari yenye thamani kubwa kama hilo.
Mosha ameliambia Championi Ijumaa kuwa anamiliki magari kadhaa ya kifahari kwa matumizi yake binafsi na familia yake.


Yafuatayo ni maelezo kuhusiana na gari hilo la kifahari kwa kuanzia kiwango cha mafuta na usumbufu anaoupata akiwa katika mizunguko yake.
Ameinunua kwa bei gani?
“Kutokana na ubora wa gari hili, nililazimika kutoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya kulinunua, kama unavyojua ni fedha nyingi, nimenunua kwa mapenzi yangu.
Alipolinunua
“Hili gari kaniuzia mtoto wa Bakhresa (Yusuph), baada ya kufikia makubaliano kati yake na mimi, aliniuzia Julai 2011.
Spidi ya gari
“Hili gari kasi yake ya mwisho ni 360, ni kasi kali na inatosha kwa matumizi yangu binafsi.
Matumizi ya mafuta



“Matumizi ni ya kawaida wala siyo ya kuogopesha sana, inategemea na umbali utakaotembea.
Usumbufu anaoupata
“Usumbufu mkubwa ninaoupata kiukweli, nikiwa naendesha barabarani, madereva wengine wanalishangaa sana, hali inayosababisha kutokea ajali au msuguano mara kadhaa.
“Hivi karibuni dereva mmoja aliigonga sehemu ya tairi la nyuma kushoto kutokana na kuishangaa, ilikuwa maeneo ya Masaki hapahapa Dar es Salaam.



“Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha,” anasema Mosha.

Habari na picha kwa hisani ya www.globalpublisher.com

HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR KWA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa misingi ya kutodhulumiana katika bei, viwango na vipimo hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati alipokuwa akisoma risala ya Ramadhani  kwa wananchi kupitia vyombo vya habari kwa mwaka huu wa 1433 Hijriya sawa na mwaka 2012 Miladia.


Katika maelezo yake Alhaj Dk. Shein alisema kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni wa neema kibiashara lakini ni vyema kufanya neema hiyo iwe kwa wauzaji na kwa wanunuzi.


Alieleza kuwa Muuzaji anauza bidhaa zake nyingi  zaidi kwa hivyo anapaswa kuhakikisha zina ubora na anachuma faida kwa kiasi ya anachouza.


Aidha, alisema kuwa mnunuzi naye anahitaji kupewa bei iliyo nafuu hasa kwa bidhaa ambayo Serikali imeipunguza kodi, kwani Serikali kama kawaida itapunguza ushuru kwa biadhaa muhimu za chakula ili

kuwawezesha wananchi kupata unafuu wa bei.

“Ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya wafanyabiashara wenye tamaa wanasafirisha bidhaa kama vile unga, sukari na mchele walizotozwa kodi ya chini na kuzisafirisha kwa njia ya magendo nje ya Zanzibar ili wapate faida kubwa’,alisema Alhaj Dk. Shein.

Kutokana na mambo hayo Alhaj Dk. Shein alisema kuwa husababisha upungufu wa baadhi ya vyakula na kuwasababishia shida wananchi wakati huu  wa mwezi wa Ramadhani.


Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein alitoa shukurani kwa wakulima nchini kwa kujiandaa kuwaopa huduma nzuri wananchi hasa katika upatikanaji wa chakula kwa ajili  ya futari huku akieleza kuwa serikali imeweka

mazingira mazuri ya biashara hasa katika Mwezi huo wa Ramadhani.

Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nayo itajitahidi kufanya kila linalowezekana ili kuwasaidia wananchi katika kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji katika maeneo mbali mbali nchini.


Alhaj Dk. Shein alisema kuwa Serikali imo katika juhudi za kuwaandalia wananchi wake maisha bora, kwa kupitia mageuzi ya katiba na pia kwa kuhesabiwa watu, mambo ambayo yamo katika sheria.
 Habari kwa hisani ya www.fatherkidevu.blogspot.com

Friday, July 20, 2012

Maisha PLUS hiyooo yaja!!


SHINDANO maalum lililotamba miaka nyuma la Maisha Plus, ambalo washiriki wake hukaa kwa miezi miwili kijijini, linatarajiwa kuanza hivi karibuni kwa kushirikiana na shirika la Oxfam Tanzania, kupitia program yake ya ‘Mama shujaa wa chakula’.

Akizungumza kwa jana, Kiongozi Mtendaji wa kampuni ya DMB, Masoud Ali ‘Masoud Kipanya’ alisema kuwa, shindano hilo la aina yake linakuja tena kwa msimu wa tatu, likiwa na utofauti kabisa, huku mambo mbalimbali yakiboreshwa, ikiwemo mshindi kuibuka na kitita cha sh milioni 20.

Kipanya alisema kuwa, kwa kushirikiana na wadhamini wakuu, Oxfam Tanzania, kupitia program yao ya ‘Mama shujaa wa chakula’, ambako watapata fursa ya kuwaweka wanawake kwenye shindano, kwa kukaa ndani ya jumba hilo la Maisha Plus huko kijijini kwa wiki mbili.

“Kwa kushirikiana na Oxfam, shindano hili tumeborsha na litakuwa la aina yake, ambapo washiriki watakaobahatika kushiriki, watafurahia na watajifunza mengi na safari hii Mama shujaa wa chakula nao watabahatika kukaa kwa wiki mbili, kisha watatoka na washiriki wa Maisha Plus kuendelea na kinyang’anyiro cha kuwania kitita hicho cha milioni 20,” alisema Kipanya.

Aidha, aliwataka vijana wa kitanzania, kuchangamkia fursa hiyo, ambako wanatarajia kuanza kufanya usaili mkoani Arusha, Agosti 3 na kisha kuendelea kwenye mikoa mingine 14, ikiwemo ya Bara na viswani Zanzibar.

Pia, alitoa wito kwa wadhamini wengine, kutumia nafasi hii kujitokeza ili kupata kutangaza, kwani shindano hilo licha ya kufanyika misimu miwili ya 2009 na 2010,  huku 2011 likishindwa kufanyika kutokana na kukosa udhamini, limejizolea sifa na kupendwa na watu wa rika mbalimbali.
 
 Habari kwa hisani ya www.fatherkidevu.blogspot.com

Wasio tambulika ajali ya Boti ya Skagit waanza kuzikwa na serikali





Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli iliozama na kukosa watu wake zikipelekwa kuzikwa na Serikali katika Eneo la Kama lililotayarishwa makusudi kwa ajili hio.

KAMA HUKUPATA KUZIONA PICHA ZA MWANAMKE ALIYEBULUZWA NA GARI NA MUMEWE HIZI HAPA

 Wiki iliyopita tuliongea katika leo tena juu ya kisa cha Marehemu Nasra pichani.Mama huyu alikuwa mkazi wa Bunda mkoani Mara lakini Dar es salaam alifika kufanya matibabu katika hospital ya Muimbili.Kwa miaka takribani 23 alikuwa mke wa bwana Elia Makumbati na kujaaliwa kupata watoto wanne mkubwa kabisa yupo chuo kikuu cha UDOM.Kwa miaka yote wamekuwa na misuko suko sana kwenye ndoa mama akiwa anapigwa sana hata kuchanwa na viwembe.


 Mwezi wa pili walitofautiana baada ya bwana kuoa mke mwingine.Wakiwa wametofautiana na Nasra kuendelea na maisha siku hiyo bwana akamfata akamkuta barabarani anatoka kazini.Akiwa na rafiki yake wanatembea akamfungia breki mguuni akamwambia anataka kuongea nae.Nasra akakataa akamwambia kama kuna maongezi hawezi kuongea nae kama vipi amfate nyumbani huku anaendelea kutembea.Bwana yule akamfata kwa nyuma akamgonga na gari na baada ya Nasra kuanguka akanasa chini hivyo kuendelea kumburuza umali wa kama mita 150 hivi.Alipofika kwenye tuta akanasuka bwana ndio kushuka kwenye gari kukimbia.


Kiukweli aliumia sana sana ngozi yote ya mgongoni,mbavuni,makalio,ikavuka na kubaki kwenye lami.Sikio lake la kushoto lote likaliwa na lami,mbavu 7 zilivunjika pamoja na mguu.Akapelekwa hospitali na baadae kulazwa Bugando Mwanza lakini ikawa anahitajika kuhamishiwa hospital ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.Akiwa muhimbili alikuwa na hali mbaya sana baadae ikathibitika kuwa ameumia ndani kwa ndani kwani alibadilika sana akavimba  na kuwa mweusi.Kwamuda wote wa miezi takribani sita alikuwa katika maumivu makali na bahati mbaya hakuweza kupambana tena kupigania maisha yake.

               Nasra pichani kulia mwenye kilemba chekundu akiwa na ndugu zake wakati akiwa mzima.


Usiku wa kuamkia jumanne ya tarehe 10 Nasra akaaga dunia.Ilikuwa ni huzuni sana jinsi alivyoteseka na namna mazingira ya kifo chake kilivyotokea.Tulikuwa na matumaini kuwa angeweza kupona maana dakika za mwisho alikuwa anaongea japo kwa shida.
Tunaomba mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Nasra mahala pema peponi,Amina.
                                            SOURCE    http://dinamarios.blogspot.com

Thursday, July 19, 2012

TUNAWATAKIA WAISLAMU WOTE DUNIA NZIMA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN!!!!

Leo ni mwanzo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan!!!Tunawatakia waislamu wote dunia nzima Ramadhan njema na mungu awajaalie wamalize salama.
Kwa wale wote wasio waislamu,kipindi hiki cha mwezi wa ramadhani ni muda mzuri wa kujifunza utamaduni wa kiislamu.Hv unajua kuwa muislam ambae amefunga haruhusiwi kula wala kunywa chochote kuanzia asubuhi mpaka litakapozama jua? Basi huo ndio mwezi mtukufu wa ramadhan ambao umeanza leo.

AJALI YA MV SKAGIT;HII NDIO IDADI YA MAITI ZILZOOKOLEWA MPAKA SASA



                                    Waokoaji wakiendelea na shughuli ya uokoaji
                                          Meli ya mv skagit ikionokeana kabla ya ajali

Zoezi la uokoaji katika tukio la kuzama kwa meli ya Mv Skagit linaendelea hadi sasa ambapo tayari maiti 31 zimepatikana,watu walionusurika na 146 na113 bado wanatafutwa.Siku 3 za maombolezo zimetangazwa na Waziri wa nchi ofisi ya waziri sera na uratibu wa bunge,Mh Lukuvi na shughuli za bunge zimehairishwa mpaka kesho kufuati tukio hili

Sunday, July 15, 2012

AJABU NA KWELI: BAHARI YA KISIWA CHA FAROE ILIPOBADILKA NA KUWA NYEKUNDU KUTOKANA NA DAMU NYINGI ZILIZOMWAGIKA KUFATIA KUUAWA KWA IDADI KUBWA YA NYANGUMI

Bahari ya kisiwa cha FAROE kila mwaka ifikapo tarehe 22 mwezi wa 11 hubadilika na kua nyekundu kutokana na utamaduni wa wakazi wa kisiwa hicho wa wa kuadhimisha siku ya kitaifa ya uwindaji wa NYANGUMI.Sikukuu hiyo ya kitamaduni imepewa jina la GRINDADRAP.Uwindaji huo wa NYANGUMI si kwa ajili ya malengo ya kibiashara kwa sababu nyama za nyangumi hao hugawiwa kwa wananchi wote wa kisiwa hicho.Wavuvi hao huwaburuza NYANGUMI hao hadi pembezoni mwa bahari na kuwakatakata mapande ya nyama na kuacha damu ikitiririka kuelekea BAHRINI na kusababisha BAHARI hiyo kuwa na rangi nyukundu.

EXCLUSIVE:JAMAA AUZA INI LAKE KWA AJILI YA KUNUNUA iPOD na iPHONE

Mwanafunzi wa kijapani auza ini lake kwa ajili ya kununua ipad na iphone.Jina lake ni Xiao Zheng na ni mwanafunzi katika chuo cha Anhui Province CHINA ameuza ini lake kwa $3400 kwa mtu asie julikana na kununua ipad na iphone.Hospitali ambayo ilihusika na operation wa jamaa huyo walidai kutofahamu chochote juu ya lengo la jamaa huyo kutoa ini lake.Kwahiyo jamaa huyo sasa hivi anamiliki iphone 4 mpya na ipad 2.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...