Wednesday, June 6, 2012

WEMA AZUA TIMBWILI SEGEREA

                                   Wema Isaac Sepetu ‘Pedeshee’.
                                 Elizabeth Michael ‘Lulu’.

                               Kajala Masanja.

WEMA Isaac Sepetu ‘Pedeshee’, amezua timbwili lenye ujazo ndani ya Gereza la Segerea, Dar es Salaam alipokwenda kuwatembelea mastaa wenzake walio nyuma ya nondo kwa misala tofauti, Kajala Masanja na Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita Juni 2, mwaka huu ambapo Wema alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutifuana na maafande wa magereza hadi akapigwa marufuku kukanyaga tena eneo hilo.
Chanzo hicho kilidai kuwa Wema alifika gerezani hapo akiwa amesheheni mazagazaga kibao ya ‘mazawadi’ ya mashosti zake hao, jambo lililowashtua maafande wa magereza na baadhi ya ndugu na jamaa wa mahabusu wengine waliokuwa wamekwenda kuwatembelea ndugu zao.

UKAGUZI
Ilidaiwa kuwa baada ya kuwafikia maafande hao walimuomba Wema kabla hajakabidhi zawadi hizo kwa Kajala na Lulu wazikague.
Iliendelea kusemekana kwamba, wakati zoezi hilo linafanyika, ndipo mwigizaji huyo alipoanza kulalamika kucheleweshwa huku askari nao wakihoji kwa nini alinunua vitu vyote hivyo mbali badala ya kununua mahali hapo.
Chanzo hicho kilisema kuwa katika kurushiana maneno huku bangi ikitajwa ndipo kukatokea kufokeana, Wema akisisitiza kuwa wampishe akawaone rafiki zake.
Ilielezwa kuwa mzozo huo ulichukua dakika kadhaa ambapo Wema alichimba mkwara ndipo akapigwa marufuku kukanyaga gerezani hapo na kushindwa kuwaona Lulu na Kajala.

Risasi Mchanganyiko lilizungumza na Wema ili kupata ukweli wa ishu hiyo ambapo mbali na kukiri, alikuwa na haya ya kusema:
“Walisema eti kisa nilienda na vitu ambavyo sikununua pale. Ukweli ni kwamba vile vitu nilinunua pale Namanga (Dar). Hata nashindwa kuelewa kama kweli hilo ni kosa linaloweza kuwafanya kunizuia kwenda kuwatembelea rafiki zangu tena.”

source;globalpublisher

EURO 2012 HATUA YA MAKUNDI

Hatua ya makundi 2012 - kundi A
Jun 8
- Poland vs Greece
- Russia vs C. Republic
Jun 12
- Greece vs C. Republic
- Poland vs Russia
Jun 16
- Greece vs Russia
- C. Republic vs Poland

Hatua ya makundi 2012 - kundi B
Jun 9
- Netherlands vs Denmark
- Germany vs Portugal
Jun 13
- Denmark vs Portugal
- Netherlands vs Germany
Jun 17
- Portugal vs Netherlands
- Denmark vs Germany

Hatua ya makundi 2012 - kundi C
Jun 10
- Spain vs Italy
- Ireland vs Croatia
Jun 14
- Italy vs Croatia
- Spain vs Ireland
Jun 18
- Croatia vs Spain
- Italy vs Ireland

Hatua ya makundi 2012 - kundi D
Jun 11
- France vs England
- Ukraine vs Sweden
Jun 15
- Sweden vs England
- Ukraine vs France
Jun 19
- Sweden vs France
- England vs Ukraine

TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA


                        TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                        Juni 6, 2012

Tanzania imepanda kwa nafasi sita kwenye orodha ya viwango ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) iliyotolewa leo (Juni 6 mwaka huu) na shirikisho hilo.
Kwa viwango vya Mei mwaka huu, Tanzania ambayo timu yake ya Taifa (Taifa Stars) inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa namba 145 hivi sasa imefika nafasi ya 139 ikiwa na pointi 214.
Mei 26 mwaka huu Taifa Stars ilicheza mechi ya kirafiki na Malawi na kutoka suluhu. Malawi yenye pointi 324 imeporomoka kwa nafasi tano kutoka ya 102 hadi 107.
Ivory Coast ambayo katika mechi yake ya mwisho Juni 2 mwaka huu iliifunga Taifa Stars mabao 2-0 imeporomoka kwa nafasi moja kutoka ya 15 hadi 16 ikiwa na pointi 943. Hata hivyo ndiyo inayoongoza kwa upande wan chi za Afrika katika viwango hivyo.

             Boniface Wambura
            Ofisa Habari
            Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI WALA KIAPO

                               Mh. Samuel Sitta ambayeni mwakilishi wa Tanzania.
                                 Mh.Abdullah Alli Hassan Mwinyi.
                                  Mbunge Shy-Rose Banji akila kiapo chake.
                                 Shy Rose-Banji akitia saini nyaraka za kiapo.
                                 Mh.Charles Makongoro Nyerere.
                                   Mh. Alhaji. Adam Kimbisa.
                                    Dkt Twaha Issa Taslima.
                                       Mh.Nderkindo Perpetua Kessy.
                                        Mhe Bernard Musomi Murunyana.
                                      Mhe. Anjela Charless Kizigha.

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wameapishwa rasmi kushika madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hilo.

Wabunge hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana Uchumi, Margareth Zziwa kuchukua nafasi hiyo.

Wabunge wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose Saddrudin Bhanji.

Wengine ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi Yahya, Mh.Nderkindo Perpetua Kessy, Dkt Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Mhe Bernard Musomi Murunyana, Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta anaeingia kwa wadhifa wake wa Uwaziri.

Wabunge hao wameapishwa pamoja jana na wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

CHANZO: FATHER KIDEVU BLOG

VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
06.06.2012
YAH: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013


Ndg. Waandishi wa Habari
Mwaka 2011/2012 Kambi ya Upinzani Bungeni ilitangaza Vipaumbele vyake katika Bajeti Mbadala ambavyo vilikuwa:
1. Kupunguza misamaha ya kodi mpaka 1% ya pato la Taifa kutoka 3%
2. Kupunguza kodi kwenye bidhaa za mafuta ya petrol na dizeli ili kupunguza mfumuko wa bei
3. Kufuta mfumo wa posho za vikao (Sitting allowances).
4. Kupeleka sehemu ya tozo ya ujuzi (Skills Development levy-SDL) kwenye bodi ya mikopo ya elimu ya juu.

Masuala haya pamoja na mengine yalikuwa sehemu ya Bajeti kivuli iliyowasilishwa Bungeni na Kambi ya Upinzani.

Mapendekezo mawili,
(1) Kodi za mafuta ya Petrol na Diseli na
(2) Tozo ya SDL yalikubaliwa na kutekelezwa. Pendekezo la misamaha ya kodi lilikubaliwa lakini Serikali imeshindwa kulitekeleza na pendekezo la kufutilia mbali posho za vikao halikukubaliwa.

Kambi Rasmi ya Upinzani inataka maelezo ya kina ya kwa nini Serikali imeshindwa kutekeleza ahadi yake iliyoitoa Bungeni kwamba misamaha ya kodi itapungizwa mpaka kufikia 1% ya pato la Taifa. Halikadhalika Kambi ya Upinzani inarejea wito wake wa kufutwa kwa Mfumo wa posho za vikao (sitting allowances).
Serikali imependekeza Bajeti ya Tshs. 15trillioni kutoka Tshs. 13 trillion. Hata hivyo ni dhahiri kwamba Bajeti ya 2011/12 ilikuwa ina changamoto kubwa za utekelezaji. Serikali ieleze itawezaje kutekeleza Bajeti ya 15trillioni?
Katika Bajeti Mbadala ya 2012/2013 Kambi ya Upinzani itajikita katika maeneo yafuatayo na kuishinikiza Serikali kuyatekeleza.

1. Kuendelea kushinikiza kupunguzwa kwa misamaha ya kodi mpaka 1% ya Pato la Taifa. Hivi sasa misamaha ya kodi ni sawa na misaada yote kutoka nchi wahisani, Tshs 1.03 trillioni ni sawa na 3% ya Pato la Taifa.
2. Kuelekeza raslimali fedha kwenye maendeleo vijijini hasa kujenga miundombinu kama barabara za vijijini na umeme vijijini.
3. Kuelekeza fedha za kutosha kukarabati Reli ya Kati na kufufua njia za Reli za Tanga, Moshi na Arusha.
4. Kuongeza wigo wa kutoza tozo la ujuzi (Skills Development Levy) ambapo sasa waajiri wote walipe ikiwemo Serikali na mashirika ya umma. Pia kupunguza tozo hili mpaka 4% ambapo 1/3 itaenda VETA na vyuo vya Ufundi na 2/3 itaenda Bodi ya Mikopo ili kukabili changamoto ya mikopo kwa wanafunzi.
5. Kushusha kima cha chini cha kodi ya mapato (PAYE) mpaka 9% ili kuwezesha wananchi wa hali ya chini kubaki na fedha za kutumia na kukuza uchumi.
6. Kuongeza mapato ya ndani na kupunguza mikopo ya kibiashara kwa kuhakikisha mapato ya ndani yanafikia 20% ya pato la taifa, kuongeza nguvu za kisheria na udhibiti ili TRA ikusanye mapato zaidi kwenye kampuni za simu na kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, mafuta na gesi.
7. Kutayarisha Taifa kuwa na uchumi wa Gesi.
8. Kupunguza /kufuta kodi kwenye bidhaaa za vyakula kwa muda maalum ili kushusha mfumuko wa bei.
9. Kuweka mfumo mpya wa elimu kwa kushirikisha sekta binafsi katika kutoa elimu kwa ubora zaidi, ikiwemo kuundwa kwa chombo cha Udhibiti wa Elimu(Regulatory authority)
10. Kutoa vipaumbele na unafuu vya kikodi kwa viwanda vya ndani vinavyotumia malighafi za nchni hasa za kilimo na zenye kuongeza ajira kama Korosho,Pamba na Mkonge.

Kambi ya Upinzani itaendelea kufuatilia kwa karibu sana suala la kukua kwa deni la Taifa amabalo limefikia hadi Tshs 22 trillioni na kutaka ukaguzi maalum kuhusu akaunti ya Deni la Taifa.

Kambi ya Upinzani itawekeza kusimamia kwa karibu suala la matumizi yasiyo na tija ya Serikali hasa kwenye magari na posho mbalimbali na Kwamba fedha nyingi zitumike kwa miradi mikubwa ya maendeleo ili kukuza ajira. Halikadhalika namna ya kupta fedha za kutekeleza mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano

Asanteni sana!
…………………………….
Zuberi Kabwe Zitto (Mb)
Waziri Kivuli-Fedha na Uchumi.

source www.globalpublisher.com
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...