Wednesday, August 10, 2011

Wauza mafuta wabanwa, watakiwa kujieleza


MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetoa amri kwa kampuni nne kubwa zinazosambaza mafuta kurejesha huduma hiyo mara moja huku ikizitaka kujieleza, kwa nini zisichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa leseni zao za biashara.

Kampuni hizo ni pamoja na BP ambayo Serikali inamiliki nusu ya hisa pamoja na Engen, Oil Com na Camel. Mbali ya maagizo hayo mawili, Ewura pia imezitaka kampuni hizo kuhakikisha kwamba zinaendelea kutoa huduma hiyo bila kubughudhi mfumo wa usambazaji mafuta nchini.

Aidha, Ewura pia imetoa leseni kwa Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kuingiza mafuta kuanzia jana ikisema ombi lake la kupatiwa leseni ya kuuza ndani ya nchi litashughulikiwa baada ya kubainisha miundombinu yake.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu alisema kisheria, amri hiyo (Compliance Order) ni sawa na agizo la Mahakama Kuu na kwamba wahusika hawana budi kutii. Mbali na kampuni hizo, Masebu alisema pia kwamba kampuni nyingine ndogo za mafuta zinachunguzwa na zitakazothibitika kuhusika katika mgomo wa kutoa huduma hiyo muhimu ya nishati, zitachukuliwa hatua.

Agizo la Ewura limekuja sambamba na hatua ya Bunge kusitisha shughuli yake kawaida jana ambayo ilikuwa ni mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara na kujadili mgomo wa wafanyabiashara ya mafuta ambao mpaka jana, walikuwa wamesitisha uuzaji wa bidhaa hiyo katika vituo mbalimbali nchini na kusababisha kusimama kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Ombi la kujadili suala hilo liliwasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya Nishati na Madini, January Makamba.

Baada ya mjadala uliochukua sehemu kubwa ya shughuli zake za jana, Bunge liliazimia kwa kauli moja kwamba Serikali ihakikishe amri hiyo ya Ewura kama ilivyowasilishwa kwake na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja inatekelezwa.

Akihitimisha hoja yake, Makamba alitoa hoja kwamba sheria ifuate mkondo wake na kuitaka Serikali kuchukua hatua kwa kampuni zitakayokaidi agizo hilo mara baada ya muda uliotolewa kumalizika. Pia alisema: “Kwa sababu tatizo hili ni la nchi nzima na watakaoanza kunufaika ni wakazi wa Dar es Salaam, Serikali ihakikishe kuwa na mikoani mafuta yanapatikana kama kawaida.”
Wananchi wakiwa katika foleni wakisubiri kununua mafuta katika moja ya vituo vinavyouza nishati hiyo jijini Dar es Salaam.(Picha na Evance Ng'ingo).

source--habarileo & mwananchi 

RAISI KIKWETE AKABIDHIWA JUKUMU LA KULINDA MAISHA YA DK SLAA!


KWA kawaida kwenye maisha hata uendeshaji wa nchi kuna siri kubwa lakini kwa hili la sasa hakuna tena usiri bali ni ukweli kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi,CCM amejiapiza kuongeza ulinzi kwa kiongozi mkuu wa upinzani nchini na katibu mkuu wa CHADEMA, Dr Wilbroad Slaa.

Ingawaje taarifa ambayo kwa mara ya kwanza inachapwa kwenye tovuti hii lakini ukweli utabaki hivyo kuwa kutokana na umaarufu unaozidi kukua wa Dr Slaa, huku pia idadi yake ya maadui ikikua kwa kasi pia wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wamemtaka rais Kikwete kuhakikisha kuwa mwanasiasa huyo hadhuriwi na mtu kwa madai kuwa jambo lolote baya dhidi yake linaweza kuleta hali ya vurugu nchini au taharuki kutoka kwa maelfu ya wafuasi wake.

Hali hii imemshawishi rais Kikwete na serikali yake kuongeza ulinzi kwa kiongozi huyo huku taarifa zaidi zikibainisha kuwa licha ya kuwa mwanasiasa lakini pia Dr Slaa ni raia kama watanzania wengine na anahitaji ulinzi wa maisha yake pia.

Tovuti hii inatoa wito kwa watanzania wenye tabia ya kubisha pasipo hoja au utafiti kufanya upelelezi kwenye mikutano ya Dr Slaa na misafara yake ndipo watabaini ni jinsi gani uongozi wa rais Kikwete unafanya kazi ya kumlinda kikamilifu Dr Slaa ili asidhuriwe na wabaya wake.

source-- www.novakambota.com

Haya ndio Maisha ya Shule za Serikali za Bweni

Hii ni picha ya Ndani ya bweni katika shule ya Sekondari ya Mwaru iliyopo Singida vijijini kweli mwanafunzi kwa hali hii anaweza kuwa Msomi wa kutegemewa na taifa letu na kuwa mwanasayansi tegemeo la nchi yetu tunaomba serikali iwasaidie wanafunzi hawa kwakweli wanaweza kufauli kati ya hawa wa shule za serikali na wale wanaosoma shule St au Private. Mungu ibariki Tanzania.

source--global publisher

POLISI UINGEREZA WALAUMIWA KUTOZIMA GHASIA

Polisi wakiwadhibiti vijana wakati wa ghasia mjini Manchester nchini Uingereza jana.

MACHAFUKO zaidi yameendelea maeneo kadhaa nchini Uingereza baada ya kushuhudia ghasia na uporaji usiku kucha kuamkia Jumatatu.

Mkuu wa polisi katika mji wa Manchester amesema maafisa wake wamekuwa na wakati mgumu kukabiliana na magenge ya vijana aliowataja kufanya vitendo vya jinai.

Katika mji wa pili mkubwa Birmingham, vijana waliwalenga polisi kwa mawe pamoja na kupora maduka. Zaidi ya washukiwa mia moja wamekamatwa katika maeneo ya Manchester na Midlands. Matukio haya yameacha idara ya Polisi kulaumiwa na raia kwamba haijawajibika ipasavyo katika kuthibiti hali.

Idara ya ujasusi imejipata tena matatani, hata kabla ya kuuguza sakata ya udukuzi wa simu, idara hii imeanza kutiliwa shaka utendakazi wake na umma.Ni wakati mgumu sana kwa idara ya polisi katika miaka mingi.

Mwezi jana polisi walijipata matatani kufuatia sakata iliyokumba gazeti ya News Of the world.Mkuu wa polisi Paul Stephenson aliye na ujuzi wa miaka mingi alilazimika kujiulu pamoja na afisa wake wa juu Jon Yates.

Kuondoka kwa wawili hao kulipelekea kuwepo na mageuzi katika idara ya polisi hali ambayo imepelekea kulegea katika kufanya maamuzi ya haraka kufuatia ghasia zilizozuka wikendi iliyopia katika eneo la Totten ham..Machafuko yalichacha kiasi cha polisi kushindwa kuthibiti hali.

Waliachwa kuwalinda wazima moto badala ya kuwakamata waporaji.Hata hivyo mkuu wa polisi Simon Foy amewatetea maafisa wake akisema walifanya kila wawezalo kuthibiti hali japo wamekabiliwa na wakati mgumu.

Aidha suala lingine limeathiri idara ya polisi ni mpango wa serikali kupunguza matumizi yake ambapo bajeti ya polisi imepunguzwa, hivyo kupunguza maafisa wa usalama. Inakadiriwa kwamba ifikapo mwaka 2015 takriban polisi 34,000 watakuwa wameachishwa kazi Uingereza na Wales.

Hakuna ishara ya wizara ya ndani kubatilisha mpango wa kupunguza makadirio ya polisi, lakini ikiwa ghasia hizi zitaendelea huenda mawaziri wakashurutishwa kuachana na mpango huo unaotaka kupunguza marupurupu ya polisi wakati wa masaa ya ziada na malipo mengine.

Huku haya yakiarifiwa Marekani nayo imetoa onyo kwa raia wake dhidi ya kuzuru Uingereza. Aidha raia wake wanaoishi Uingereza wameonywa dhidi ya kushiriki kwenye ghasia hizo au kuwa karibu na matukio ya ghasia. Hatua kama hii imekuwa ikilenga maeneo ya vita duniani. Lakini matukio yanayoendelea Uingereza bila shaka imewaacha wengi vinnywa wazi kote duniani.

source--bbc

Maaskofu 10 jela maisha

  

Maaskofu 10 kati ya 12 Bongo wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya hawana namna ya kuchomoka, serikali imewalenga na shabaha zimekubali, hivyo wanachongoja ni adhabu kali inayoweza kufikia kifungo cha maisha jela.

Habari za kiuchunguzi zinasema kuwa, maaskofu wawili wanaweza kupona kwa sababu ushahidi haujajitosheleza lakini 10 hawana ujanja, kwa hiyo wapo kwenye mkondo wa kupokea adhabu ya kifungo cha maisha jela watakapofikishwa mahakamani na kukutwa na hatia.

Katika ‘kusapoti’ uchunguzi wetu, wiki iliyopita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,( Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi aliwaahidi wabunge kwamba ushahidi utakaoambatana na mkanda wa video utapelekwa bungeni ili waheshimiwa hao wajionee jinsi baadhi ya viongozi wa dini walivyokosa maadili.

Lukuvi alikazia kuwa viongozi hao wa dini, wengi wao wapo chini ya mtandao unaoongozwa na askofu mkubwa kutoka Nigeria ambaye ameshanaswa na hivi sasa anaishi nyuma ya nondo za moja ya magereza yetu.

Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya katika Jeshi la Polisi nchini, Godfrey Nzowa aliliambia gazeti hili wikiendi iliyopita kwamba mtu anayekutwa na hatia ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha maisha jela.

Nzowa alisema: “Tumekuwa wakali sana, tunasimamia kifungo cha maisha jela ili kukomesha biashara hii haramu. Inawezekana hakimu akapima kosa la mshtakiwa na kumhukumu miaka 30 jela lakini ukweli ni kwamba sasa hivi adhabu ya juu ni kifungo cha maisha jela.”

Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa Lukuvi, Nzowa alikataa kutaja majina ya viongozi wa dini wanaotuhumiwa kuwa ‘wazungu wa unga’ lakini alisisitiza kwamba kila kitu kinakwenda kwa hatua na kwamba arobaini yao imefika bila chenga.

“Majina hatutayatoa kwa vyombo vya habari kwa sasa, tupo makini sana. Wakati ukifika mtawaona wahusika na hatutanii, tuna vielelezo vya kutosha kuwatia hatiani,” alisema Kamanda Nzowa.

source--global publisher

Monday, August 8, 2011

WAKENYA WANAOKABILIWA NA NJAA, WAHAKIKISHIWA KUPATA CHAKULA



















Katibu mkuu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya, Abbas Gullet, anawahakikishia wakenya wote wanaokabiliwa na njaa kwamba msaada wa chakula uliotolewa na mpango wa Kenyans for Kenya, utagawanywa bila mapendeleo.  Akiongea mapema leo katika afisi za shirika hilo, gullet amesema awamu ya pili ya kusambaza chakula hicho cha msaada itatekelezwa katika maeneo ambako chakula cha msaada hakijafika. Wakati huo huo, wanaharakati wa kundi la unga revolution, wanaopigania kupunguzwa kwa gharama ya maisha, wanawataka Rais Mwai Kibaki na Waziri mkuu Raila Odinga kuchukuwa hatua za kupunguza bei za vyakula nchini.

SHEREHE ZA NANE NANE TANZANIA MWAKA 2011

Sherehe hizi zanatumika kuendeleza na kukuza ujuzi wa wafugaji na wakulima nchini.Hili kukuza na kuongeza bidhaa mbalimbali zinazotokana na shughuli hizi kwani asilimia kubwa ya wananchi yanajishughulisha na ufugaji wa ng'ombe,mbuzi,kuku na ulimagi wa mazao mbalimbali kama mahindi,mpunga,alizeti.Siku kuu ya nane nane nchini imefanyika mjini Dodoma.Watu mbalimbali wamefika mji hapa.Wakulima na wafugaji,ofisi za serikali na wadau mbalimbali wamefika kuonesha bidhaa na uduma wanazotowa.Pia wananchi mbalimbali kutoka mikoa ya jirani na wenyeji wameudhuuria.Makamu wa rais wa Tanzania alikuwa mgeni rasmi wa sherehe hizi Dkt Bilal.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...