Wednesday, August 29, 2012

Mwanamke Apigwa Na Mumewe Hadi Kuzirai Kwa Kushiriki Sensa 2012

Habari Leo, SHINYANGA
Mkazi wa Ndembezi mjini Shinyanga amepigwa na mumewe hadi kuzirai na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu baada ya kutoa ushirikiano kwa karani wa Sensa ya Watu na Makazi.



Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Evarist Mangala, alisema jana kuwa mwanamke huyo, Esther Zablon (40) alipigwa juzi saa mbili asubuhi baada ya mumewe, Ismail Yahya kupata taarifa kuwa karani wa sensa alifika nyumbani kwao na mkewe kukubali kuhesabiwa na kutoa takwimu za familia yao.



Akisimulia, Kamanda Mangala alisema karani huyo alipokwenda nyumbani hapo, mume hakuwapo na kama mkuu wa kaya, Esther akazungumza na kutoa taarifa.



Alisema baada ya mume kurudi nyumbani na kugundua kuwa mkewe alikubali kuhesabiwa, alimshambulia kwa ngumi na mateke na kusababisha mke huyo kupoteza fahamu.



Kutokana na kipigo hicho, kwa mujibu wa Kamanda Mangala, Esther alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa kwa uchunguzi na matibabu.



"Wakati mwanamke huyo akichukua fomu namba tatu ya Polisi (PF3) kituoni kabla ya kufikishwa hospitalini, huku akilia kuwa sababu ya kipigo ni yeye kukubali kuhesabiwa, jambo ambalo ni kinyume na msimamo wa dini ya mumewe (Uislamu)," alisema Kamanda Mangala.



Hata hivyo, Kamanda alisema Esther alitoroka wodini kwa kuhofia mumewe kukamatwa na hatimaye kufungwa.

Kamanda Mangala alisema Polisi wanaendelea kumtafuta Yahya na akipatikana atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili.

TID AZUNGUMZA KUHUSU TUHUMA ZA YEYE KUTAKA KUMUUA ALI KIBA...!!!

Kwenye U heard ya XXL Clouds Fm August 28 2012 Gossip Cop Soudy Brown aliripoti kwamba kuna mwanamke aliekamatwa na Polisi na kuhojiwa kwa masaa nane wakati akiwa kwenye mipango ya kumuua msanii wa bongo fleva Ally kiba.

Baada ya kuhojiwa na polisi kwa masaa nane, mwanamke huyo alikiri kwamba alitumwa na T.I.D kwenda kumuua Ally Kiba.

Alipohojiwa na Soudy Brown, T.I.D alifunguka na kusema “kwa nini nimuue Ally Kiba bwana, si mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli sasa hivi niko polisi kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi sasa sijui mwanamke gani anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo, kwa sababu gani? 

Toka nimezaliwa sijawahi kugombana na Ally Kiba, ukibisha muulize mwenyewe kama ameshawahi kukorofishana na mimi, nia ya hao watu ni kuniangusha mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe.”

Soudy alipomtafuta meneja wa Ally Kiba alijibiwa “hakuna taarifa zozote ambazo ziko tayari kutolewa kwenye vyombo vya habari sasa hivi  lakini ikiwa tayari utakua wa kwanza kujua”
 
Source:This Day Magazine

Monday, August 27, 2012

SHARO MILIONEA AVUTA MKOKO WA MILIONI 15


Katika kuthibitisha kua fani ya maigizi kibongo bongo inalipa,mkali kutoka 'bongo movie' ambae ameng'arisha nyota yake kupitia uchekeshaji Hassan Mkiety "Sharo Milionea" amevunja kibubu na kuvuta ndinga yenye thamni ya ngawira za kibongo milioni 15.

Katika mazungumzo mafupi aliyofanya na teentz.com via 4n sharo amesema makusnyo kutoka muvi alizocheza,shoo za muziki na mambo mengine kibao anayofanya ndivyo vimemuwezesha kuvuta mkoko huo na hajapata msaada kutoka kwa mapedeshee kama wasanii wengine wanavyofanya.

"Ni makusanyo tu kutoka ktk michongo yangu kama muvi,shoo za mziki wangu,ndivyo vimenipa hii ndinga.Sijaomba kwa pedeshee mim imtoto wa kiume bwana najituma.Alisema Sharo Milionea



www.teentz.com
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...