Saturday, August 4, 2012

KILICHOMUONDOA 'ASHA NGEDELE' ORIJINO KOMEDI HIKI HAPA


UKISTAAJABU ya Mussa Hutayaona ya firauni,msemo huo umetimia hivi karibuni mkoani hapa baada ya mawaziri,wakuu wa mikoa na familiya ya Mzee Ngedele,kumpiga marufuku Mpoki kumzal ilisha dada yake wa damu Asha Ngedele kwenye vipindi vya kundi la vichekesho la Orijino Komedi.
Hali hiyo imebainika hivi karibuni baada ya familia ya Ukoo wa Ngedele kuwapiga marufuku kundi la Orijino komedy kulitaja jina la ukoo huo wa marehemu Ramadhani Ngedele wenye maskani yake maeneo ya Mji Mpya mkoani hapa. Kwa kipindi kirefu sasa baada ya kupigwa mkwala huo kundi hilo la Orijino komedy linalorusha michezo yake kila siki za alhamis kwenye luninga ya taifa ya TBC I baada ya kupigwa mkwara huo wamenywea na kukitoa kipengele hicho walichokuwa wamekipa jina la timbwili la Asha Ngedele.

Chanzo chetu cha habari cha kuamini kilidai kwamba takribani wiki mbili zilizopita familia hiyo ya Ngedele alimuita Asha Ngedele anayeishi jijini Dar es salaam kuja kwenye kikao cha familia kilichofanyika nyumbani kwao maaneo ya Mji Mpya,inadaiwa kwamba angendakuku ya kikao hicho ni kuhusina na Asha Ngedele kukubali kaka yake Mpoki kulizalilisha jina la ukoo huo wa Ngedele Mpoki na Asha Ngedele ni mtu na kaka yake wa damu ambapo Mpoki mama yake ni mdogo na Asha mama yake ni mkubwa, wazazi wao hao ni mtu na dada yake wa baba mmoja mama mmoja ambao kabila lao ni wapogolo wa lfakara wakitokea kwenye ukoo wa Kiwanga. Baada ya kupokea habari hizo mwandishi wetu aliingia kazini na kuwasaka wahusika wote ambapo wakwanza kupatikana alikuwani Mzee Msafiri Ramadhan Ngedele ambaye ni baba mdogo wa Asha alipohojiwa alisema,
“Nikweli sisi familia ya Ngedele tumezuia jina la ukoo wetu tuchafuliwa na kundi lile la Orijino Komedy mbaya zaidi na kinacho washangaza watu wengi ni kwamba Asha na Mpoki ni mtu na dada yake wa damu,hivyo ukoo tuliamua kuwapiga marufuku kulitaja jina la ukoo wetu pia jambo hilo lilikuwalikiwachukiza wajomba wa Asha na Mpoki ambao ni Waziri mstaafu Juma Ngasongwa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu hawa wanazaliwa na mama zao mama yake Asha ni mkubwa na mama yake mpoki ni mdogo"alisema mzee Msafiri Ngedele.
Alipotakiwa kuzungumzia jambo hilo mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu alisema kwamb ni kweli Asha Ngedele na Mpoki ni watoto wa dada zake na kwamba jambo hilo binafis lilikuwa likimchefua. "Mimi binafsi sijapata muda wa kukutana na hao wajomba zangu wakuzungumzana nao juu ya jambo hilo,lakini kabla ya kwenda kwa dada zangui ifakara nitakwedan kwa ukoo wa Ngedele kuzungumza nao tuangalie namna ya kuliweka sawa jambo hilo'"alisema Mwambunga ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa,alikuwa ni mkuu wa Wilaya ya Morogoro.
Mtandao huu alipofika nyumbani kwa Waziri mstaafu DktJuma Ngasongwa maene ya Riti jirani na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro kwa lengo la kusikia kauli yake juu ya jambo hilo alielezwa kwamba waziri huyo wa awamu ya tatu amesafiri. Kwa upende wake Asha Ngedele alipohojiwa kuhusiana na sakata hilo alidai kwamba kwake hakuna tataizo lolote na kwamba alilidhia jina lake kuchafuliwa'
"Kwa mtu mwenyeakili awezi kuchukua mambo ya kichezo ya kuingia na kaumjaji mtu kwamba ndio alivyo,ni kweli mimi mwenyewe nimelidhia kaka yangu kulitumia jina langu kwenye kundi lao"alisema Asha ambaye makazi yake yako jijini Dar es salaam
Mpoki alipohojiwa na mwandishi wetu kwa kupia simu yake ya kiganyani namba 0713 44 12## ambapo baada ya kusomewa tuhuma hizo alijibu kwa mkato akisema" Siko tayari kuhojiwa kwa sasa na " na kukata simu Ikumbukwe kwamba Asha Ngedele upande wa mama ni mpogolo na upande wa baba ni mrugulu,ambapo Mpoki pia upande wa mama ni Mpogolo na upande wa baba ni Mhaya Kwenye baadhi ya michezo ya kundi hilo la Orijino komedi Mpoki alisikika akimnanda dada yake huyo kwa kusema
'' We humjuia Asha Ngedele kabla ya kuja huku Dar alikuwa akijiuza pale Kahumba na kwamba alikuwa hana ukimnunulia supu ya mguu wa ng'ombe'Kongoro' unaondoka naye"
Athumani Ngedele ambye ni mdogo wake Asha alipohojiwa jana alisema kwamba kama familia walikuwa wakipata shida sana wanapojitambulsikwa jina la Ngedele" kwa mfano nikienda hospital nikitaja jina langu la Athumani Mohamed Ramadhan Ngedele watu wote waliokuwa eneo hilo wageuza shingo na kunitazama huku wengine wakiniuliza yule mwanamke kati Asha Ngedele ni ngugu yako,sio sili kunawaktia mwingine naladhimika kumkana dada yangu wa damu ambaye tumechangia baba"alisema Athuman
Mzee Msafiri Ramandhan Ngedele ambaye ndiye mkuu wa familia ya ukoo wa Ngedele baada ya ndugu zake kutangulia mbele za haki akiwemo baba mzazi wa Asha mzee Mohamed Ramadhni Ngedele.
Mzee Msafiri ambaye ni baba mdogo wa Asha ndiye aliyesima
ma kidete kulipiga marufuku kundi la Orijino komedi kulitumia jina la Ngedele kwa madai kwamba kundi hilo lilitumia jina hilo vibaya na kuzalilisha ukoo huo wa Ngedele wenye maskani yake maeneo ya Mji Mpya mkoani Morogoro.

Maneno Mohamed Ramadhan Ngedele ambaye ni bingwa wa kusakata disko Afirika mashariki na kati aliyetapa kwenye fani hiyo miaka ya 90 akionyesha umahiri wakwe hivi karibuni ndani ya ukumbi wa DDC mkoani Morogororo.
 
 STORI NA  DISMAS TEN KWA MSAADA WA  BONGO DAWN TOWN

LOWASSA ATOA TENDE NA KANZU KWA WAISLAMU MONDULI

Mh Lowassa akimkabidhi sheikh Simba sehemu ya tende hizo.Wengine pichani kushoto ni Sheikh wa Mto wa Mbu Sheikh Nasib Idd Nasib Mnyema Kkatibu wa Bakwata wilaya ya Monduli Idd Idoya na Ustadh Swalehe Ramadhan .
Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa, ametoa katoni kadhaa za tende pamoja na jozi 100 za kanzu kwa ajili ya Waislam wa Monduli.Akipokea msaada huo, sheikh wa wilaya ya Monduli Sheikh  Mwinshehe Mwinyimgeni Salum Simba, alimshukuru mh Lowassa kwa utaratibu wake huo ambao amekuwa akiufanya kila mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa Waislam wa Monduli.

STRANGE!!!!!! MDOGO WAKE MARK ZUCKERBEG (MMILIKI WA FACEBOOK) ANAFANYA KAZI KATIKA KAMPUNI YA GOOGLE KWA SASA


Habari za kuaminika na kwamba mdogo wake mmiliki wa facebook "Mark zuckerbeg" anaeitwa  Arielle Zuckerberg ameajiliwa na kampuni ya google rasmi.Mdogo wake huyo atafanya kazi kama junior product manager for the social media marketing firm Wildfire, kitengo ambacho google wamekianzisha hivi karibuni.


Pia dada ake Mmiliki huyo wa facebook aitwae Randi kwa sasa ni mtayarishaji (Producer) wa Reality tv show inayokwenda kwa jina la Silicon Valley ambacho kitarushwa na Bravo.Alifanya kazi katika kampuni ya kaka yake (facebook) kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2011.


Randi alitweet kuhusiana na ajira mpya ya mdogo wake na kumtania kidogo


"Congrats Wildfire! There are officially now more Zuckerberg family members working for Google than Facebook! #awkward ;)," Alisema Randi

EMINEM THE MOST LIKED FACEBOOK USER: 60 MILLION LIKES [EMINEM NDIE MTUMIAJI WA FACEBOOK MWENYE LIKES NYINGI KULIKO WOTE.ANA LIKES MILION 6O MPAKA SASA HIVI]


Mpaka sasa eminem ndie mtumiaji wa facebook mwenye likes nyngi kuliko watumiaji wengine wote,eminem amevunja rekodi hiyo baada ya kuwaacha nyuma rihanna na lady gaga ambao ndio walikua wanaongoza kwa kuwa na likes nyingi kwenye page zao.
Page yake imekua ikiwekwa vitu vipya mara kwa mara video kutoka youtube na picha,takwimu zinaonyesha kua page ya eminem imekua ikiongeza likes mpya takribani 26000 kila siku akifuatiwa na rihanna ambae page yake huongeza likes mpya 22000 kila siku.

Thursday, August 2, 2012

Rais wa Zanzibar Dk Ali Shein Atua Kusini Pemba na Kufuturisha

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ahaj Dk.Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakiagana na Viongozi wa Mikoa ya Pemba katika Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba,baada ya kumaliza Ziara ya kisiwani humo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akisalimiana na Viongozi na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni Pemba katika chakula cha Futari aliyowaandalia wananchi na waumini Kijiji cha Mkanyageni katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan jana. 
 Sheikh Yussuf Abdalla,wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba akitoa shukurani kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Moahmed Shein,kwa kuwaandalia Chakula cha Futari,iliyofanyika jana katika Viwanja vya Skuli ya Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akijumuika na wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani,Mkoa wa Kusini Pemba,katika chakula cha Futari,aliyowaandalia Wananchi hao katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni
 Baadhi ya akina mama wa Kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika chakula cha Futari katika Mwezi mtukufu wa Ramadhan,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni Pemba   
 Baadhi ya Wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika chakula cha Futari katika Mwezi mtukufu wa Ramadhan,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) akiagana na Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba jana baada ya Chakula cha Futari aliyowaandalia katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar
 
habari kwa hisani ya hakingowi.com

Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA):Tunaunga Mkono Maandamano ya Amani Yaliyoitishwa Kupinga Hatua ya Serikali Kulifungia Gazeti la MwanaHALISI.

 Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)na Mkurugenzi wa Vijana Taifa Mh,John Mnyika

Kwa niaba ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) tukiwa ni sehemu ya wadau wa sekta ya habari nchini, tunaunga mkono maandamano ya amani mliyoitisha ya kupinga hatua ya serikali kulifungia gazeti la MwahaHALISI.

Tunawapongeza wahariri kwa mshikamano wenu katika kipindi hiki cha majaribu; endeleeni kusimama pamoja, ni umoja wenu ndio utakaokuwa kinga ya pamoja dhidi mtu au chombo chombo chochote kinachoingilia uhuru wenu. Mshikamano wenu ni ishara ya kushindwa kwa mkakati wa ‘wagawe uwatawale’ na imani kwamba umoja ni nguvu. Wahariri wote hawapaswi kukaa kimya kuhusu kufungiwa kwa MwanaHALISI kwa kuwa leo ni kwa gazeti hilo, kesho itakuwa kwa gazeti lingine; hivyo ni vyema

kuungana pamoja kulinda uhuru, taaluma na sekta ya habari nchini.

Kwetu sisi hatua hiyo ya serikali tunaitafsiri zaidi ya kufungia gazeti la MwanaHALISI; ni hatua ya kufungia uhuru wa kusambaza habari na uhuru wa kupokea habari. Hivyo hatua hiyo ni kinyume cha haki za

binadamu, kinyume cha utawala bora na ni kikwazo kwa demokrasia na maendeleo. Hakika serikali na viongozi wake wamevuka mstari wa kukubali kukosolewa na sasa wameamua kuanza kufungia uhuru wa fikra mbadala.

Hatua ya Waziri mwenye dhamana na sekta ya habari kugeuka mlalamikaji, mwendesha mashtaka na mfungaji ni mwelekeo mbovu wa kupuuza taasisi za kusimamia uwajibikaji na haki. Uamuzi uliofanywa na serikali hauna tofauti na unaofanywa na raia wanaojichukulia sheria mikononi(mob justice). Kwa serikali inayoheshimu misingi ya asili ya haki, tulitarajia chombo chochote cha habari, kikivunja sheria ama kukiuka

maadili dhidi ya serikali, viongozi wake ama watu binafsi mashtaka ama malalamiko yangepelekwa kwa taasisi zinazohusika mathalani Baraza la Habari(MCT) ama Mahakama.

Hatua ya serikali kufungia gazeti la MwanaHALISI pamoja na kuwa imechukuliwa kwa mujibu wa sheria iliyopo, imekiuka misingi ya asili ya utawala wa sheria. Kwani kulikuwa na sheria nyingine nzuri ambazo

serikali ingeweza kutumia kupitia mahakama lakini ikaamua kuchagua kutumia sheria mbaya kwa kutumia mamlaka ya Waziri. Itakumbukwa kwamba wadau wa sekta ya habari na hata serikali yenyewe imekuwa ikikiri kwamba Sheria hiyo iliyotumiwa ni sheria mbovu inayohitaji kufutwa ama kufanyiwa marekebisho makubwa ikiwemo kupunguza mamlaka makubwa ya viongozi wa serikali dhidi ya vyombo vya habari.

Sheria yoyote inayotambulika kuwa mbovu katika jamii yoyote, inapoteza uhalali wa kihaki(legitimacy) miongoni mwa umma na hivyo kuendelea kuitumia ni kuteteresha misingi ya utawala wa sheria na kutoa mfano mbaya kwa vijana nchini na wananchi kwa ujumla. Hivyo, tunachukua fursa hii kuitaka serikali kuharakisha mchakato wa kupitisha sheria ya vyombo habari na sheria ya uhuru wa taarifa.


Aidha tumeshangazwa na uamuzi wa serikali kufanya maamuzi yake kwa ubaguzi kwa kulichukulia hatua gazeti la MwanaHALISI na kukwepa kuyachukulia hatua magazeti mengine ambayo yameandika habari

inayoshabihiana na maudhui ya habari iliyoandikwa na gazeti hilo. Kwa muda mrefu sasa, habari za uwepo wa viongozi ama makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) yenye kupanga ‘kumng’oa’ Rais Jakaya Kikwete miongoni mwa wanaotarajiwa kugombea urais kupitia chama hicho mwaka 2010 zimeandikwa na magazeti mbalimbali.

Hatua hii ya kibaguzi inaibua maswali kuhusu dhamira ya serikali kulifungia gazeti hilo wakati huu ambapo mchango wa gazeti hilo na mengine yaliyo mstari wa mbele kupinga ufisadi na kutetea rasilimali

za taifa unahitajika kwa kiasi kikubwa. Hata baada ya kulifungia gazeti la MwanaHALISI, habari za aina hiyo zimeendelea kuandikwa ikiwemo na vyombo vya habari vya nje; mathalani tarehe 24 Oktoba, 2008
kutoka Ufaransa gazeti la Africa Intelligence inayomtaja Rostam Aziz kukusanya fedha kwa ajili ya kufadhili kundi lake katika uchaguzi huo. Katika muktadha huo, serikali inapaswa kulifungia gazeti la MwanaHALISI mara moja, kama imeonyesha wazi kushindwa kuyachukulia hatua magazeti mengine.

Kadhalika kwa mtiririko wa matukio katika taifa letu, kuna mwelekeo wa Serikali na CCM kuminya maoni yenye kumkosoa au kumgusa Rais Kikwete. Mjadala wa Rais Kikwete ‘kung’olewa’ katika uchaguzi mwaka 2010 unaelekea kuichukiza kwa kiasi kikubwa Serikali na CCM. Gazeti la MwanaHALISI liliandika habari ya namna hiyo, likafungiwa na Serikali. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiwa katika ‘Operesheni Sangara’, alitoa hoja hiyo na matokeo yake CCM ikaibuka na kujibu kwa

vitisho na vioja.

Vijana wa Tanzania wangependa kupata mfano uongozi bora wenye kukubali kukosolewa na kukubali mabadiliko badala ya uongozi legelege wenye kuendeleza udikitekta wa kimawazo na hivyo kuminya fikra huru. Si dhambi kwa CHADEMA ama mtu yoyote kutaka kuiondoa CCM ama kiongozi
wake yoyote madarakani mwaka 2010 kupitia njia za kidemokrasia.

Mwisho, tunatoa mwito kwa watanzania wote kusoma alama za nyakati na kuunga mkono harakati hizi za wahariri na wadau wa sekta ya habari kutetea uhuru wa kweli katika taifa letu. 

Jamii itambue kwamba kitisho cha uhuru na haki kwa mtu Fulani au mahali Fulani ni tishio kwa watu wote na mahali pote.

 Yanayofanywa kwa vyombo vya habari, yanaweza pia kufanywa kwa watetezi wengine kwani hivi karibuni taifa limeshuhudia Asasi ya HAKIELIMU ikitishiwa kutokana na jitihada zake za kuhamasishamabadiliko ya fikra katika sekta ya elimu na kupiga vita ufisadi unaoathiri sekta hiyo.

 Tuko katika kipindi cha majaribu; kuibuka kwa mijadala yenye kuchochea mgawanyiko/ubaguzi, kuongezeka kwa matabaka na malalamiko juu ya hali za maisha. Katika wakati huu ambapo misingi ya nchi yetu iliyopo katika Ngao ya Taifa ya Uhuru na Umoja inapotikiswa ni wakati wa kuunganisha “Nguvu ya Umma” kupinga ainazote za ufisadi na kutetea rasilimali za taifa kwa kuhamasisha maadili, fikra mbadala na mabadiliko ya kweli. Kuunga mkono maandamano ya wadau wa sekta ya habari ni sehemu ya azma hiyo. Mshikamano, daima; 

pamoja, tutashinda!

Wasalaam,

John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana Taifa.
 
habari kwa hisani ya hakingowi.com

MAKAMU WA RAIS DKT GHARIB BILAL AFUTURISHA MIGOMBANI UNGUJA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa dini ya Kiislam, katika swala ya Magharibi wakati alipojumuika na waumini hao katika Futari ya pamoja aliyowaandalia na kufuturu nao Migombani Unguja mjini Zanzibar jana Agosti 01, 2012.










Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Waumini wA dini ya Kiislam, baada ya kufuturu nao futari ya pamoja aliyowaandalia Migombani Unguja mjini Zanzibar jana, Agosti 01, 2012. 
 Wake wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal (wa pili kulia) na Mama Asha Bilal (katikati) wakijumuika na waumini wa dini ya Kiislam, wakati wa futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kwa waumini hao iliyofanyika Migombani Unguja, mjini Zanzibar jana Agosti 01, 2012. 
  Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akipiga picha ya pamoja na baadhi ya kinamama, baada ya kushiriki nao katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, iliyofanyika jana Migombani Unguja mjini Zanzibar
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, akipiga picha ya pamoja na baadhi ya kinamama, baada ya kushiriki nao katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, iliyofanyika jana Migombani Unguja mjini Zanzibar. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais
 
 Habari kwa hisani ya www.hakingowi.com
 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...