Saturday, June 8, 2013

Cheki picha kadhaa zinazomwonyesha Amber Rose na muonekano wake mpya wa nywele,Hana kipala tena





Breaking News : Mbunge wa Mtwara Mjini akamata kwa uchochezi!

Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnein Murji ametiwa mbaroni na Jeshi La Polisi kwa tuhuma za uchochezi na kuhusika katika vurugu zilizotokea hivi karibuni katika viunga vya mji wa Mtwara.

Habari za kuthibitika zinaeleza kwamba mbunge huyo amekamatwa saa 2:30 jioni hii naanashikiliwa katika kituo Kikuu cha Polisi
Mjini Mtwara.

Katibu wa Mbunge huyo Meckland Millanzi amethibitisha kukamatwa kwa Murji na kwamba anahusishwa na mvurugu hizo.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Advera Senso amesema kwamba Murji amekamatwa hivi punde nyumbani kwake
katika eneo la Shangani.

Taarifa zimebainisha kwamba Murji amekamatwa na kwamba hati ya kumkamata imeeleza anatuhumiwa kuchochea vurugu za kupinga gesi ya Mtwara kwenda jijini Dar es Salaam.

Siku chache zilizopita zilizuka vurugu kubwa katika mji wa Mtwara na viunga vyake baada ya wananchi wa mji huo kuandamana baada ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kusomwa na Waziri wa wizara hiyo kueleza msimamo wa serikali kwamba mpango wa kusafirisha gesi jijini Dar es Salaam uko pale pale.

Awali kabla ya vurugu hizo kutokea shughuli mbalimbali za kijamii zilisimama huku watu wasiofahamika kusambaza vipeperushi kuhamasisha kusimama kwa shughuli hizo.

Kutokana na vurugu hizo baadhi ya watu walipoteza maisha, nyumba kuchomwa moto na madaraja kuharibiwa vibaya.

Mpaka sasa watu zaidi ya 80 wamekamatwa na jeshi la polisi na kushtakiwa mahakamani.

Chanzo : JamiiForum

Big Sean Azungumzia Collabo Yake Na Eminem

 Big Sean hivi karibuni ameongea na MTV Kuhusiana na ujio wa ngoma yake mpya ambayo amefanya na Eminem

Kama ukikumbuka vizuri kipindi cha nyuma alishawahi kuweka picha kadhaa kwenye mtandao zinazomwonyesha yeye pamoja na Eminem wakiwa studio ila hakuwahi kuzungumza chochote kuhusiana na picha hizo
Big Sean ambae pia ni msanii kutoka detroit sehem ambayo anatokea eminem pia amesema ngoma hiyo itakua "The Biggest Hit Of Detroit"

Thursday, June 6, 2013

Download Hapa mixtape mpya ya Kanye West-YEEZUS

J cole atimae aiachia rasmi ngoma iliyokua inasubiriwa kwa hamu ambayo mkali Kendricl Lamar ameshrikishwa




J.Cole ameiachia rasmi ngoma yake inayokwenda kwa jina la "Fobidden Fruit" ambayo ilikua inasubiriwa kwa hamu na mashabiki kutokana na kumshirikisha mkali Kendrick Lamar,Hii ngoma itapatikana kwenye Album Mpya ya J.Cole inayoitwa "Born Sinner" itakayoingia sokoni tar 18/5.Isikilize na idownload hapa chini

Listen and Download Exclusive Audio | Kanye West ft D Banj-Scape Goat (Remix)




Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...