Habari kwa wote ndugu wafuatiliaji wa blog hii. Nataka nizungumze japo kwa ufupi juu ya hali halisi ya binadamu kuwa na pande zake za hisia na jinsi anavyoweza kizimiliki katika wakati mwafaka.
Siku zote tumekuwa ni watu wa kupenda kufurahia mambo mazuri yanayotutokea na kusahau kwamba siku moja mambo hubadilika na kuwa kinyume na tulivyozoea, hapa ndipo ninapo kumbuka maneno ya "wahenga" yaani watu wa zamani hasa waswahili wa pwani hii na inchi hii ya Tanzania kwamba "kesho bora, inajengwa na leo" hivyo husikatike tamaa na matatizo machache yanayo kupata kwa wakati unaijenga kesho yako bora.
Bandugu, jamaa na marafiki lazima tujipe majukumu bila ya kuchoka na kuvunjika moyo na hali mbaya zozote zinazotukuta katika harakati za maisha yetu. Bora kuteseka leo ili uje kuvuna matunda mazuri uliyoyapanda kipindi upo kwenye mapigano yako ya maisha hususani mashuleni na sehemu zetu za kazi, hakuna mafanikio bila ya maumivu.
Huu ni walaka wangu kwenu wenzangu mliopo nyuma yangu na mbele yangu. Usilaumu nafsi yako eti "kila siku mimi", hapana hizo ni dalili za kushindwa kusonga mbele. Binadamu kama binadamu hashindwi kitu mpaka siku unakwenda chini ya ardhi. usijikatishe tamaa na kurudi nyuma.
Mungu yupo pamoja na sisi wenye kusubiri.