Kwenye
U heard ya XXL Clouds Fm August 28 2012 Gossip Cop Soudy Brown
aliripoti kwamba kuna mwanamke aliekamatwa na Polisi na kuhojiwa kwa
masaa nane wakati akiwa kwenye mipango ya kumuua msanii wa bongo fleva
Ally kiba.
Baada ya kuhojiwa na polisi kwa masaa nane, mwanamke huyo alikiri kwamba alitumwa na T.I.D kwenda kumuua Ally Kiba.
Alipohojiwa
na Soudy Brown, T.I.D alifunguka na kusema “kwa nini nimuue Ally Kiba
bwana, si mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli sasa hivi niko polisi
kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi sasa sijui mwanamke gani
anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo, kwa sababu gani?
Toka
nimezaliwa sijawahi kugombana na Ally Kiba, ukibisha muulize mwenyewe
kama ameshawahi kukorofishana na mimi, nia ya hao watu ni kuniangusha
mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe.”
Soudy
alipomtafuta meneja wa Ally Kiba alijibiwa “hakuna taarifa zozote
ambazo ziko tayari kutolewa kwenye vyombo vya habari sasa hivi lakini
ikiwa tayari utakua wa kwanza kujua”
Source:This Day Magazine