Mkuu wa soka barani Asia, Mohamed Bin Hammam, leo amepigwa marufuku asishiriki katika shughuli za soka katika maisha yake yote.
Hii ni baada ya shirikisho la soka duniani, FIFA, kumpata na hatia ya kosa la kutoa hongo, kabla ya uchaguzi wa rais wa shirikisho hilo mwezi uliopita.
Uamuzi uliotolewa Jumamosi ni kufuatia kikao cha maadili cha FIFA nchini Uswisi, mkutano ambao ulifanyika katika kipindi cha siku mbili.Bin Hammam, raia wa Qatar, tarehe 29 Mei alijiondoa katika kuwania urais wa FIFA, na siku tatu baadaye, Sepp Blatter, mwananchi wa Uswisi, alichaguliwa tena pasipo kupingwa, kuliongoza shirikisho hilo kwa awamu nyingine ya nne.
0 comments:
Post a Comment
CHANGIA MAWAZO YAKO HAPA