Aliyekuwa rais wa shirikisho la mchezo wa soka barani Asia, Mohamed Bin Hammam, anatarajiwa kukata rufaa dhidi ya marufuku ya maisha ya kutoshiriki katika shughuli zozote za mchezo huo, aliyopewa na shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA.
Aliyekuwa rais wa shirikisho la mchezo wa soka barani Asia, Mohammed Bin Hammam
Katika mtandao wake, Bin Hammam, ametaja matukio ya hivi karibuni kama mapambano katika vita vinavyoendelea.
Vile vile amechapisha barua inayopongeza juhudi zake, katika shirikisho hilo iliyoandikwa mwaka wa 2008 na rais wa FIFA, Sepp Blatter.
Chini ya barua hiyo kuna mstari unaosema "Hii ni mapambano na sio vita vyenyewe".
0 comments:
Post a Comment
CHANGIA MAWAZO YAKO HAPA