Aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak ni dhaifu na amegoma kula, kulingana na shirika rasmi la habari nchini humo.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo, akituhumiwa na makosa ya rushwa na kuamuru kufanyika kwa mauaji ya waandamanaji.Mkuu wa hospitali ambapo Bw Mubarak ameshikiliwa huko Sahrm al-Sheikh amesema alikuwa mnyonge, amepungua uzito, na hakuwa akila vya kutosha kumweka hai, shirika la MENA limeripoti.
Lakini wakosoaji wamesema ugonjwa wa Bw Mubarak ni kama njama ya kuepuka kufikishwa mahakamani.
Wafuasi wa upinzani wanatia shaka ripoti hiyo. Wanaamini mamlaka husika zinajaribu tu kuzuia kuanza kwa kesi ya Bw Mubarak, inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Miongoni mwa ripoti nyingi zilizotolewa kuhusu afya ya Bw Mubarak ya hivi karibuni imesema madaktari wake wataamua katika saa za hivi karibuni, iwapo ulaji wake wa hivi sasa hautoshi kumweka hai.
Mwandishi wa BBC Cairo, Jon Leyne, alisema, sasa hivi kuna ushahidi unaozidi kuibuka kwamba ni mtu anayedhoofika kadri siku zinavyoendelea.
Bw Mubarak alipinduliwa mwezi Februari katika ghasia maarufu zilizosababisha vifo vya zaidi ya watu 840.
Source--bbcswhili.com
1 comments:
alokuwa Rais wa MIsri Hosni Mubarak,alikuwa Rais wa 3 wa Misri baada ya Baba wa Taifa hilo Gamal Abdel Nasser na kisha kufuatiwa na Anwar Sadaat aliyeuwawa mwaka 1981, na tangia hapo nchi ya Misri ikatawaliwa na Mubarak alokuwa rubani wa ndege za kivita za Misri, alitawala kwa miongo 3 mpaka alipong'olewa madarakani na waandamanaji walikuwa wakikusanyika kila uchao katika viwanja vya Tahrir na sasa nchi hiyo iko chini ya Baraza la kijeshi linalofanya mchakato wa kuandaa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu
Post a Comment
CHANGIA MAWAZO YAKO HAPA