Thursday, June 27, 2013

The Illuminati Public Service Annoucement **Must Watch This Video**

Jambo Squad - Mamon'goo.{Official Video}


Ulinzi wa Obama haujawahi kutokea Afrika


Dar es Salaam. Ulinzi katika ziara ya Obama ni wa hali ya juu kuliko ulinzi wa aliyewahi kupewa Rais yeyote wa Marekani kwa safari yake ya Afrika mwaka huu.
Tayari jeshi la nchi hiyo limewasili nchini, kuweka mambo sawa na kukagua maeneo yote ya karibu na sehemu atakazotembelea na kupita wakati wa ziara hiyo. Maaskari na majasusi zaidi ya 500 wapo Dar es Salaam kuhakikisha usalama huo na kuweka vifaa mbalimbali vya mawasiliano Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.
Licha ya hilo, ziara yake kutakuwa na askari 1,687 wakataokuja kwa meli maalumu kubwa ya kivita iliyosheheni silaha mbalimbali, ikiwamo ndege sita za kivita aina ya AV-8B Harrier na helikopta za kivita 23, ambazo zinatarajiwa kupasua anga la Tanzania kuimarisha ulinzi.
Meli hiyo ya kisasa aina ya Wasp Class (Uk 1), pia itakuwa imebeba meli nyingine zaidi ya tano maalumu kwa kubeba vifaru, magari ya deraya, askari na vifaa vingine itatia nanga Bahari ya Hindi kuongeza nguvu iwapo lolote litatokea.
Taarifa inaonyesha italazimika kuwapo kwa meli tatu za aina hiyo wakati wa ziara yake nchini Senegal, Tanzania na Afrika Kusini kwani mwendo wake siyo kasi hivyo kulazimika kutumia zote hizo kwa ajili hiyo.
Meli hiyo kubwa imeundwa kuwezesha askari wa Marekani kuingia kwa urahisi eneo la vita kwa brigedi nzima, kwani wanaweza kutumia aina zote za vita majini, angani na ardhini. Ni meli aina hiyo zilizotumika vita vya Marekani na Iraq. Licha ya mitambo ya kivita, ina hospitali kubwa yenye uwezo wa kulaza zaidi ya wagonjwa ya 600.

Habari kutoka gazeti la mwananchi

Membe: Msije Dar wakati wa ziara ya Obama


Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.
Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.
Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa wingi wa wageni.
“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.
Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo.
“Jiji la Dar es Salaam litakuwa na mambo mengi kwa hiyo wale wenye kuja kutaka kustarehe wafute safari zao,” alisema na kuongeza: “Kama kuna watu ambao hawapo Dar es Salaam na hawana sababu za kuja mjini waache tu mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu jiji la litakuwa limejaa na baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni hao.”
Alisema katika kipindi cha siku tano zijazo, baadhi ya barabara za Jiji la Dar es Salaam zitakuwa na shughuli nyingi na nyingine zitalazimika kufungwa. Barabara itakayofungwa ni pamoja na ile ya Mwai Kibaki na ile ya Bagamoyo itakuwa na shughuli nyingi pia wakati Michelle atakapokwenda Jumba la Makumbusho, Jumanne ijayo.
Wasafiri wa mikoani
Wasafiri wa mikoani wataathirika zaidi Jumanne ijayo wakati Rais Obama atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion Ubungo.
Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.
Rais Obama atakwenda katika kituo hicho yapata saa 4.00 asubuhi na kwa kiasi kikubwa itaathiri magari ya usafirishaji wa mizigo na abiria yatakayokuwa yanatoka na kuingia Dar es Salaam kabla na wakati huo.


Wengine watakaoathirika ni wakazi wa Kimara, Mbezi, Kibamba hadi Kiluvya. Athari nyingine ya usafiri itakuwa katikati ya jiji ambako Obama na msafara watakuwa na shughuli nyingi na hasa ile ya ufunguzi wa barabara karibu na Ikulu na kukutana na wafanyabiashara kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Jumatatu ijayo.
Watumiaji wengine wa barabara watakaopata shida ni wale wa Barabara ya Bagamoyo hasa pale Rais Obama na mkewe watakapokwenda kuweka mashada ya maua kwenye ubalozi wa zamani wa Marekani uliopuliwa na mabomu mwaka 1998.
Ulinzi hoteli za kitalii
Mashushushu wa ndani na nje ya nchi wamezingira kwenye hoteli kubwa za Dar es Salaam na walionekana katika baadhi ya hoteli hizo, wakiwatumia mbwa maalumu kufanya ukaguzi wa chumba hadi chumba.
Tofauti na utaratibu uliozoeleka, baadhi ya hoteli zenye hadhi ya nyota tano zimeanza kutumia mitambo maalumu ya kompyuta kuwafanyia ukaguzi wageni wote wanaoingia.
Wamchongea JK
Mtandao wa Kutetea Waandishi wa Habari Duniani (CPJ), umemwandikia barua Rais Obama ukimtaka kujadiliana kwa kina na mwenyeji wake Rais Kikwete wakati wa ziara yake nchini kuhusiana na vitendo vya kuuawa na kuteswa kwa waandishi wa habari wa Tanzania.
Katika barua hiyo iliyosainiwa na Mtendaji Mkuu wa CPJ, Joel Simon na nakala yake kusambazwa kwa viongozi mbalimbali akiwemo Rais Kikwete mwenyewe, mtandao huo ulitolea mfano wa kuuawa kwa Mwandishi wa Channel 10, Daudi Mwangozi na Issa Ngumba wa Redio Kwizera. Pia kupigwa na kuteswa kwa Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation, Absalom Kibanda.


Akizungumzia mkutano wa Smart Partnership utakaoanza kesho, Membe alisema utajadili jinsi ya kutumia sayansi na teknolojia kukuza uchumi.
Viongozi watakaohudhuria mkutano huo ni Waziri Mkuu wa Malayasia, Najib Razak, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Uhuru Kenyetta (Kenya), Boni Yayi (Benin), Ali Omar Bongo (Gabon), Ikililou Dhoinine (Comoro), Faure Gnassingbe (Togo), Ernest Koroma (Sierra Leone), Blaise Compaore (Burkina Fasso), Mahinda Rajapaska (Sri Lanka) na Mfalme wa Swaziland, Mswati II, ambaye aliwasili jana.

Habari kutoka gazeti la Mananchi

Wednesday, June 26, 2013

Listen & Download New Song-Solo Thang-Kalata 3


Nash_MC_akiwaponda_mashabiki_wa_hip_hop_Tanzania


Lady_Jaydee_#39;s_Nothing_But_The_Truth_Review


Listen & Download New Music-Stopa Rymes ft Joh Makini-Nimesha Vurugwa


Listen & Download New Music | AT-Kitumbua


New Music | Mwana Fa_AY ft J Martin-Bila Kukunja Goti


Tuesday, June 25, 2013

Elinika na Katuni Za Kipanya : Kipanya Leo


‘Ambulance’ iliyombeba Mzee Madiba iliharibika

Gari hilo la kubebea wagonjwa liliharibika mitambo yake likiwa njiani ambapo lilikaa dakika 40

Afrika Kusini. Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela maarufu kama Madiba imedaiwa alipata wakati mgumu wakati akielekea hospitalini baada ya gari la wagonjwa lililokuwa likimsafirisha wiki mbili zilizopita, kuharibika mitambo likiwa njiani kwenda hospitalini.
Taarifa za kuharibika kwa gari hilo zilitolewa juzi na msemaji wa rais wa Afrika Kusini Mac Maharaj, ambaye alidhibitisha kuwa gari hilo lilipata  matatizo na ililazimika  Rais huyo wa zamani kuhamishiwa katika gari nyingine.
Hata hivyo Maharaj, alisema tukio hilo halikuwa na tishio lolote kwa afya ya mzee  Mandela, kwa sababu aliongozana  na madaktari wa kutosha.
Dakika 40
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Marekani CBS  lilisema kuwa vyanzo kadhaa vilidai kuwa Mandela alilazimika kukaa eneo hilo ambapo gari  hilo la wagonjwa liliharibika kwa muda wa dakika 40.

Shirika hilo la CBS lilisema kuwa wakati Mandela alipokuwa akihamishwa katika  gari nyingine viwango vya joto vilikuwa chini sana.
Mandela alilazwa hospitalini huku hali yake ikiwa mbaya kutokana na maambukizi ya mapafu ya mara kwa mara na tangu wakati huo alikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Hii ni mara ya tatu kwa Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.
Mandela, aliye na umri wa miaka 94, alilazwa hospitalini mnamo Juni 8, baada ya kupata matatizo ya kupumua, ugonjwa ambao umekuwa ukimsumbua mara kwa mara.
Akiongea na Shirika la Habari la Enca, Mac Maharaj alisema kuwa ‘hakuna tatizo lililotokea’ kwani walikuwa makini, wakati wa tukio hilo.
Alipotakiwa kutoa maelezo kwamba ilikuwaje gari la kubebea wagonjwa  ilitumike ikiwa  na hitilafu za kimitambo  alisema  “Hili ni tukio la kawaida. Hakuna anayeweza kutarajia kuwa gari lililokuwa likienda vizuri lingeweza kukumbwa na hitilafu za kimitambo.”

Ini na figo
Taarifa za ndani zilisema kwamba  ini na figo za rais huyo wa zamani zilikuwa zikifanya kazi kwa asilimia 50. Kiongozi huyo vile vile alitarajiwa kufanyiwa upasuaji maalumu  kuziba kidonda kilichokuwa kikivunja damu.
Kwa mujibu wa mjukuu wa  Madiba, Ndaba Mandela alisema babu yake  alikuwa akiendelea vyema na alikuwa akitarajiwa kuwa atatoka hospitalini hivi karibuni.
 “Ni Mungu pekee anayeweza kumchukua…sisi kama familia tutazidi kushukuru na kusherekea maisha yake,”alisema  Ndaba Mandela.
Wakati huohuo mmoja wa wanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Dk. Ramphele amezindua chama kipya cha kisiasa kutoa changamoto kwa chama tawala cha ANC kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo hapo mwakani.
Dk. Ramphele aliwaambia wafuasi wake waliokusanyika wakati wa uzinduzi wa chama hicho mjini Pretoria kuwa ANC haitakiwi kuaminiwa kuinua uchumi wa nchi hiyo.
Chama chake kijulikanacho kama Agang chenye maana ya kujenga kimejipanga kupigana na rushwa na kuimarisha sekta ya elimu kama malengo  yao makuu.
Dk Ramphele ni mkurugenzi wa zamani wa Benki ya Dunia na ni mke wa zamani wa mpigania uhuru wa Afrika Kusini hayati Steven Biko
 
Habari kutoka gazeti la mwananchi

Monday, June 24, 2013

Kitenge Maulid Kitenge atangaza kugombea ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CCM!


Mtangazaji maarufu wa kipindi cha michezo na taarifa ya habari ITV na Radio One, Kitenge Maulid Kitenge kwa kupitia mtandao wa Instagram na Twitter ametangaza kugombea ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CCM.
Kitenge anakuwa miongoni mwa watu maarufu na wasanii waliotangaza nia hiyo kama Soggy Dogg Hunter (CHADEMA, Segerea) na Afande Sele (CHADEMA, Morogoro).
Aidha, kuna tetesi kuwa huenda wasanii MwanaFA (CCM) na Prof Jay (CHADEMA) wakatangaza nia bila kumsahau msanii wa Bongo movie Ray Kigosi.

Abdu Kiba ft Ally Kiba - Kidela.(Official Video)

Quick Rocka ft Ngwair & Shaa - My Baby ( Official Video )

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...