Habari kutoka Vatican leo hii zimethibitisha kuwa Papa Benedict XVI atajiuzulu kutoka katika nafasi yake hiyo Februari 28 mwaka huu kutokana na Umri wake kuwa mkubwa mno na kupelekea kupungua uwezo wa utendaji wa kazi zake.
Father Federico Lombardi ambaye ndiye msemaji wa Papa ametoa taarifa hizi rasmi leo kwa vyombo vya habari, ikiwa ni ujumbe wa moja kwa moja kutoka kwa Papa kwa makadinali wa kanisa hilo duniani.
Papa huyu atatimiza umri wa miaka 86 tarehe 16 mwezi April na alichaguliwa kushika nafasi hii mwaka 2005 akiwa mjerumani wa 6 kushika nafasi hiyo ya juu katika kanisa Katoliki na wa kwanza kabisa kuhudumia kanisa kama papa kutokea karne ya 21
Habari kutoka sammisago.com