Ayman al-Zawahiri, ambaye kwa muda mrefu mno amekuwa msaidizi wa Osama Bin Laden  katika kuiongoza Al-Qaeda, na akishikilia nafasi ya pili katika kutoa amri, sasa  ataliongoza kundi hilo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa katika wavuti ya kundi hilo. 
Bin Laden aliuawa nchini Pakistan alipopigwa risasi na kikosi maalum kutoka  nchini Marekani mwezi Mei.
Kundi la Al-Qaeda limeonya kwamba litaendelea na vita vyake dhidi ya Marekani  na Israel chini ya uongozi wa Zawahiri.
Wadadisi wa masuala ya Al-Qaeda wanaelezea kwamba Zawahiri, mwenye umri wa  miaka 59, na aliyezaliwa nchini Misri, ni mtu mwerevu sana, lakini hana uwezo wa  kuwavutia wafuasi wengi kama alivyofanya Osama.
Baadhi ya wadadisi wanasema yeye ndiye aliyepanga na kuendesha shughuli  nyingi zilizohusiana na shambulio la Marekani la 9/11.
Kwa muda wa miaka mingi, msaidizi wa Bin Laden, ambaye atakayefanikiwa  kumpata atapokea dola milioni 25 (pauni milioni 15), alitazamiwa kurithi  madaraka hayo.
Taarifa iliyotangaza madaraka hayo ilichapishwa katika wavuti ya Al-Qaeda, na  kusemekana imetolewa na uongozi wa juu unaotoa amri katika kundi hilo.
"Sheikh Dk Ayman al-Awahiri, Mungu amsaidie, katika kuendelea na uongozi wa  kundi", taarifa ilielezea.
Taarifa ilielezea kwamba chini ya Zawahiri, itaendelea na vita vitakatifu vya  Jihad dhid ya Marekani na Israel, "hadi majeshi yote ya wavamizi yanaondoka  kutoka ardhi ya Waislamu".


 
 









 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment
CHANGIA MAWAZO YAKO HAPA