HABARI hii haina lengo la kumhukumu mtu, mwenye uwezo huo ni Mwenyezi
Mungu pekee, lakini Ijumaa Wikienda lina orodha ndefu ya warembo
waliowahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Steven Kanumba ‘The
Great’ ambapo uchunguzi umethibitisha kuwa, kifo cha staa huyo
kimewaacha ‘wajane’ hao katika vilio vya kila kukicha.
Uchunguzi
makini uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa nyota huyo alikuwa na
uhusiano na wasichana mbalimbali wakiwemo ma-miss, wanamuziki, wasanii
wa sinema na wasio na fani yoyote ile.
Kwa mujibu wa chanzo chetu
cha uhakika, kifo cha Kanumba bado kinawachuruzisha machozi wasichana
hao kama inavyokuwa kwa wanawake walioolewa halafu wakaondokewa na waume
zao (wajane).
‘Wajane’ hao waliotajwa kuendelea kumwaga machozi ni kama ifuatavyo;
WEMA SEPETU
Ni Mrembo wa Tanzania mwaka 2006/07 ambaye kwa sasa
ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo. Awali yeye na marehemu Kanumba
walijaribu kuficha penzi lao lakini kadiri siku zilivyosonga, hakukuwa
na kificho tena.
Kifo cha Kanumba ni pigo kwake, bado anamlilia hadi
sasa. Wakati wa msiba alikiri kuwa hakuwahi kutengana moja kwa moja na
marehemu.
SYLVIA SHALLY
Ni mrembo wa Miss Dar City Centre 2009, alikuwa na
uhusiano na Kanumba, walianza walipokutana katika shindano la kumtafuta
Unique Model kwenye Hoteli ya Giraffe, Dar.
Yeye bado hajaamini kama staa huyo aliaga dunia ghafla.
QUEEN SUZY
Ni Mnenguaji wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa
Ngwasuma’, aliwahi kudaiwa kuwa na uhusiano na marehemu Kanumba wakati
fulani akipiga mzigo kwenye Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta
International’ ambapo mara nyingi Kanumba alikuwa akienda nyumbani
kwake.
Anasema kifo cha Kanumba mpaka sasa bado ni ndoto kwake na hakuamini.
SHAMSA FORD
Orodha inamtaja mcheza filamu huyu ambaye aliwahi kuwa na uhusiano na marehemu wakati wakiigiza sinema ya Saturday Morning.
Kifo cha Kanumba kwake ni pengo kwa sababu ndiye aliyemwingiza kwenye
‘gemu’ la sanaa ya maigizo na atamlilia marehemu kila atakapokuwa
akimkumbuka.
AGNESS GERALD ‘MASOGANGE’
Orodha hiyo inamjumuisha muuza nyago
huyu kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva na filamu ambaye anadaiwa
aliwahi kuwa na uhusiano na Kanumba wakiwa kwenye Kundi la Sanaa la
Kaole la jijini Dar.
Kifo cha Kanumba anasema bado kinamchuruzisha
machozi kila anapokumbuka, hasa mara ya kwanza alipopokea taarifa za
kufariki kwake.
SHARZ
Huyu ni mrembo aliyecheza filamu ya marehemu iitwayo The
Shock. Ndiye mpenzi wa Kanumba aliyetangaziwa kuolewa, lakini ghafla
waliachana na Sharz hajaonekana tena kwenye muvi.
Kifo cha marehemu kilimkuta akiwa masomoni, Kenya. Kilio chake anasema kitadumu na kudumu na kudumu.
AUNT EZEKIEL
Ishu ilibumburuka mwaka jana pale Klabu ya Bongo Movie (Viwanja vya
Leaders, Kinondoni, Dar) ilipotangaza kumsimamisha ndipo yakaibuka
makubwa kuwa alifanyiwa hivyo kwa sababu alimmwaga Kanumba. Baada ya
hapo uhusiano wao ukakatika.
Alikuwa mstari wa mbele kwenye kifo cha marehemu, mpaka Muhimbili kuuhifadhi mwili. Anasema hatakaa asahau kifo hicho.
ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’
Kwa sasa anashikiliwa na sheria kwenye
Gereza la Segerea, Dar akiwa mshukiwa wa kwanza katika kifo cha Kanumba
kufuatia ugomvi wa kimapenzi kati yao.
Siku ya tukio, baada ya
ugomvi huo Lulu aliondoka na huko alikokwenda alipata habari kwamba
mpenzi wake huyo amefariki dunia, akasema haitatokea akaamini.
SALMA HAMIDU
Ni mdada mkazi wa jijini Mwanza, yeye anatajwa
kwenye listi ya ‘wajane’ kufuatia hivi karibuni kuibuka akidai ana mtoto
wa kike aliyezaa na marehemu Kanumba aitwaye, Treasure.
Kwa vyovyote vile, kwa kuondokewa na mzazi mwenzake, Salma atakuwa analia kila kukicha, hasa anapomwangalia Treasure.
PASCALIA MACHA
Ni mkazi wa Sumbawanga, Rukwa. Aliibuka na kudai
akiwa anaishi Dar, aliwahi kuwa na uhusiano na marehemu na kufanikiwa
kupata naye mtoto.
ISABELLA FRANCIS
Huyu ni msanii anayekuja juu kwenye tasnia ya
uigizaji Bongo. Amewahi kukiri kuwa ‘alishatoka’ na marehemu kwa mapenzi
motomoto na wakamwagana bila bifu.
Kifo cha mpenzi wake huyo kwake
ni kitendawili ambacho anaamini siku si nyingi, Mungu atakitegua kuwa
maigizo na uhalisia wa marehemu utarudia kama zamani.
WALIOKWENDA NYUMBANI KWA MAMA KANUMBA
Wajane hao hawajaishia hapo
kwani wiki mbili baada ya kifo cha staa huyo wa filamu za Bongo wako
warembo, kwa nyakati tofauti, waliokwenda nyumbani kwa marehemu maeneo
ya Vatican City Hotel, Sinza na kumkabili mama’ke wakimwambia wao
walikuwa wachumba wa Kanumba.
Mama Kanumba aitwaye Flora Mtegoa aliwahi kukiri kwa mapaparazi kuhusu ‘wachumba’ hao ambapo alisema idadi yao ilifikia watano.
TUNAMNUKUU:
“Sishangai kusikia kuna wanawake wanaodai walizaa na
marehemu mwanangu maana hapa wameshakuja wasichana, nadhani wamefika
watano sasa, kila mmoja anadai yeye alikuwa mchumba wa marehemu (kicheko
cha uchungu).”
www.globalpublisher.com