Kwenye
 U heard ya XXL Clouds Fm August 28 2012 Gossip Cop Soudy Brown 
aliripoti kwamba kuna mwanamke aliekamatwa na Polisi na kuhojiwa kwa 
masaa nane wakati akiwa kwenye mipango ya kumuua msanii wa bongo fleva 
Ally kiba.
Baada ya kuhojiwa na polisi kwa masaa nane, mwanamke huyo alikiri kwamba alitumwa na T.I.D kwenda kumuua Ally Kiba.
Alipohojiwa
 na Soudy Brown, T.I.D alifunguka na kusema “kwa nini nimuue Ally Kiba 
bwana, si mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli sasa hivi niko polisi 
kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi sasa sijui mwanamke gani
 anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo, kwa sababu gani? 
Toka
 nimezaliwa sijawahi kugombana na Ally Kiba, ukibisha muulize mwenyewe 
kama ameshawahi kukorofishana na mimi, nia ya hao watu ni kuniangusha 
mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe.”
Soudy
 alipomtafuta meneja wa Ally Kiba alijibiwa “hakuna taarifa zozote 
ambazo ziko tayari kutolewa kwenye vyombo vya habari sasa hivi  lakini 
ikiwa tayari utakua wa kwanza kujua”
Source:This Day Magazine 

 
 









 
 
 
 
