Friday, April 27, 2012

WARAKA WA VICENT KIGOSI (RAY) KWA WATANZANIA JUU YA MSIBA WA KANUMBA

Waraka huo ulinaswa hivi karibuni kupitia blogu yake ambapo baada ya kuupitia tukaona ni vyema ukasomwa na Watanzania wote ili kuweza kupata jibu la kwa nini yeye hahusiki? Waraka huo ni huu hapa chini…

Yapata wiki tatu sasa tangu msanii mwenzangu Steven Kanumba aage dunia na kama ilivyo kwa kila kitu kinapotokea huandamana na kila aina ya maneno na hisia mbalimbali kutokana na mitazamo yawatu kupishana kuhusiana na jambo husika.
Kulingana na muktadha huo, msiba wa Steven Kanumba umekumbwa na maneno na hisia kama hizo, hususan mazingira ya kifo chake. Kinachosikitisha zaidi watu wengi (ambao wanajitambulisha kama wapenzi wa Kanumba) na baadhi ya vyombo binafsi vya habari vimekuwa vikinihusisha na kifo hicho kwa kusema kwamba kwa njia moja au nyingine nahusika na mauaji ya Steven Kanumba.


Kwa muda wote huo tangu msiba ulipotokea mpaka leo hii nashika kalamu kujaribu kuyaweka sawa na kuondosha hisia chafu katika fikra za watu. Nimekuwanikipitia katika wakati mgumu sana kwa jinsi ambavyo nimekuwa nikinyooshewa vidole kila upande nikihusishwa na kifo hicho.
Kiujumla nimezingatia maoni ya wapenzi na mashabiki wangu wakinitaka kuwa na subira ila kuna usemi usemao, uongo ukirudiwa sana jamii huusadiki na kuuona ukweli, nimeona nisikae kimya ila niweke sawa hili kwamba sihusiki na kifo cha Steven Kanumba.
Nasema wazi kwanza sihusiki kabisa na kifo cha Kanumba kwa kuzingatia mazingira yenyewe ya kifo kilivyotokea. Wakati kifo hicho kinatokea, nilikuwa sehemu nyingine kabisa na mimi nilikuwa mtu wa tatu kutaarifiwa kwamba Kanumba amepatwa na mkasa ambao baadaye ulisababisha kifo chake.


Hata nilipofika katika Hospitali ya Muhimbili (tofauti na watu wanavyodhani kuwa nilifika nyumbani kwake, ukweli mimi nilimkuta tayari amepelekwa Muhimbili), nilikuta tayari alikuwa ameshafariki ndiyo maana hata polisi wanaohusika na usalama wa raia, si tu kwamba hawakuniweka chini ya ulinzi, sikuitwa hata kuhojiwa kwa sababu hakunamazingira yoyote yanayonihusisha mimi nakifo hicho.


Kitu kikubwa kilichokuwa kinaendelea baina yetu ni kwamba tulijenga ushindani wa kuendeleza kazi mbele kwa kila mmoja akitoa kazi, mwingine anamjibu.


Watu wanaojaribu kuonesha kuwa tofauti zetu ilikuwa ni uadui, huwa hawajui wapi tulikotoka ndiyo maana wanasema wasemavyo na katika kuthibitisha kuwa tofauti hizo hazikufikia katika uadui

Kumtuhumu mtu kwa namna yoyote ile bila ya uthibitisho wa tuhuma hizo, ni kosa kwa sheria za nchi na pia kama ni mfuasi wa dini yoyote ni dhambi, kwani wakati ukisema hayo huku hujui uhalisia bali unasukumwa na nguvu za hisia tu ni sawa na kumchafua mtu huyo katika jamii bila ya kujua jamii inamchukuliaje.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...