Tuesday, September 6, 2011

Yobo afurahia kurudi klabu ya Fenarbahce

Mlinzi wa Everton Joseph Yobo amejiunga tena na klabu ya Uturuki ya Fenerbahce kwa mkopo wa muda mrefu

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Nigeria mwenye umri wa miaka 31, msimu uliopita aliichezea klabu hiyo kwa mkopo, akaisaidia kuweza kunyakua ubingwa wa ligi ya Uturuki maarufu Super Lig.

Yobo, ambaye mkataba wake na Everton unamalizika mwaka 2014, hakucheza mechi yoyote ya maandalizi ya Ligi Kuu ya England.

"Nina furaha kila kitu kimekamilika, ilikuwa miezi mitatu migumu," alisema.

Fenerbahce ilikuwa na nia ya kuendelea kumtumia mlinzi na mkataba huo mpya wa mkopo ulikamilishwa kabla ya kumalizika dirisha la usajili nchini Uturuki siku ya Jumatatu.

Yobo alionekana tayari kujiunga na klabu ya Fenerbahce mwishoni mwa msimu wa 2010-11 lakini badala yake akarejea Everton.

Tangu wakati huo klabu hiyo ya Uturuki ilikuwa katika kashfa ya kupanga matokeo ya mechi na ikapoteza ubingwa wa ligi na kufuzu kwa ubingwa wa Europe.

Lakini Yobo hayupo tayari kujumuishwa na kashfa hiyo.

Fenerbahce pia imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji kutoka Cameroon Henri Bienvenu Ntsama kutoka klabu ya BSC Young Boys ya Switzerland.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ametia saini mkataba wa miaka minne kuichezea klabu hiyo wenye thamani ya dola milioni 5.7.

1 comments:

Anonymous said...

safiii yobosafiii yobo

Post a Comment

CHANGIA MAWAZO YAKO HAPA

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...