Sunday, July 24, 2011

Tanzania yanyong'onyea

'

Hali ya umeme nchini Tanzania kwa sasa inazidi kuwa si nzuri baada ya maeneo yanayotoa umeme wa maji kukaukiwa na maji kabisa hasa bwawa kubwa la Mtera. Wakati huu baadhi ya maeneo yanapata umeme kwa mgao kwa saa zisizozidi sita kwa siku. Hali hiyo imeathiri maisha ya kila siku ya watu na pia uchumi. Charles Hilary alizungumza na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ambaye ni mbunge wa Ubungo kupitia chama cha CHADEMA Mheshimiwa John Mnyika, mwanzo akitaka kujua kama kweli nchi hiyo inatarajiwa kuingia katika kipindi kigumu zaidi cha kukosekana umeme na nchi kuwa giza?
Kufahamu hali halisi ilivyo baada ya kutangazwa kuongezeka kwa mgao wa umeme nchini humo, Charles Hilary pia alizungumza na Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania Badra Masoud.

Mwandishi wa bbc John Solombi kutoka Dar es Salaam naye alituma taarifa kuhusu athari ya mgao huo uliosababisha viwanda sita kufungwa na takriban wafanyakazi 7000 kutolewa katika ajira zao. Utafiti umefanywa na shirikisho la viwanda nchini Tanzania.

2 comments:

Anonymous said...

Ni aibu kubwa sana hasa kwa nchi ambayo iko huru tangia miaka 50 iliyopita

rajabu said...

na ni aibu zaidi kutegemea chanzo cha aina moja cha umeme,mabwawa ya maji ya mtera,maporomoko ya mto pangani,bwawa la kidatu,wangewekeza pia maporomoko ya mto rusumo huko ngara na waharakishe huo mchakato wa umeme wa gesi huko songas na bila kusahau uzalishaji wa umeme kwa kutumia makaa ya mawe iwe kiwira au chanzo kingine cha aina hiyo, na c kukaa tu maofisini na fikra za mtera, umizeni vichwa viongozi na vitengo vyenu.

Post a Comment

CHANGIA MAWAZO YAKO HAPA

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...