Wednesday, June 6, 2012

WEMA AZUA TIMBWILI SEGEREA

                                   Wema Isaac Sepetu ‘Pedeshee’.
                                 Elizabeth Michael ‘Lulu’.

                               Kajala Masanja.

WEMA Isaac Sepetu ‘Pedeshee’, amezua timbwili lenye ujazo ndani ya Gereza la Segerea, Dar es Salaam alipokwenda kuwatembelea mastaa wenzake walio nyuma ya nondo kwa misala tofauti, Kajala Masanja na Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita Juni 2, mwaka huu ambapo Wema alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutifuana na maafande wa magereza hadi akapigwa marufuku kukanyaga tena eneo hilo.
Chanzo hicho kilidai kuwa Wema alifika gerezani hapo akiwa amesheheni mazagazaga kibao ya ‘mazawadi’ ya mashosti zake hao, jambo lililowashtua maafande wa magereza na baadhi ya ndugu na jamaa wa mahabusu wengine waliokuwa wamekwenda kuwatembelea ndugu zao.

UKAGUZI
Ilidaiwa kuwa baada ya kuwafikia maafande hao walimuomba Wema kabla hajakabidhi zawadi hizo kwa Kajala na Lulu wazikague.
Iliendelea kusemekana kwamba, wakati zoezi hilo linafanyika, ndipo mwigizaji huyo alipoanza kulalamika kucheleweshwa huku askari nao wakihoji kwa nini alinunua vitu vyote hivyo mbali badala ya kununua mahali hapo.
Chanzo hicho kilisema kuwa katika kurushiana maneno huku bangi ikitajwa ndipo kukatokea kufokeana, Wema akisisitiza kuwa wampishe akawaone rafiki zake.
Ilielezwa kuwa mzozo huo ulichukua dakika kadhaa ambapo Wema alichimba mkwara ndipo akapigwa marufuku kukanyaga gerezani hapo na kushindwa kuwaona Lulu na Kajala.

Risasi Mchanganyiko lilizungumza na Wema ili kupata ukweli wa ishu hiyo ambapo mbali na kukiri, alikuwa na haya ya kusema:
“Walisema eti kisa nilienda na vitu ambavyo sikununua pale. Ukweli ni kwamba vile vitu nilinunua pale Namanga (Dar). Hata nashindwa kuelewa kama kweli hilo ni kosa linaloweza kuwafanya kunizuia kwenda kuwatembelea rafiki zangu tena.”

source;globalpublisher

EURO 2012 HATUA YA MAKUNDI

Hatua ya makundi 2012 - kundi A
Jun 8
- Poland vs Greece
- Russia vs C. Republic
Jun 12
- Greece vs C. Republic
- Poland vs Russia
Jun 16
- Greece vs Russia
- C. Republic vs Poland

Hatua ya makundi 2012 - kundi B
Jun 9
- Netherlands vs Denmark
- Germany vs Portugal
Jun 13
- Denmark vs Portugal
- Netherlands vs Germany
Jun 17
- Portugal vs Netherlands
- Denmark vs Germany

Hatua ya makundi 2012 - kundi C
Jun 10
- Spain vs Italy
- Ireland vs Croatia
Jun 14
- Italy vs Croatia
- Spain vs Ireland
Jun 18
- Croatia vs Spain
- Italy vs Ireland

Hatua ya makundi 2012 - kundi D
Jun 11
- France vs England
- Ukraine vs Sweden
Jun 15
- Sweden vs England
- Ukraine vs France
Jun 19
- Sweden vs France
- England vs Ukraine

TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA


                        TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                        Juni 6, 2012

Tanzania imepanda kwa nafasi sita kwenye orodha ya viwango ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) iliyotolewa leo (Juni 6 mwaka huu) na shirikisho hilo.
Kwa viwango vya Mei mwaka huu, Tanzania ambayo timu yake ya Taifa (Taifa Stars) inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa namba 145 hivi sasa imefika nafasi ya 139 ikiwa na pointi 214.
Mei 26 mwaka huu Taifa Stars ilicheza mechi ya kirafiki na Malawi na kutoka suluhu. Malawi yenye pointi 324 imeporomoka kwa nafasi tano kutoka ya 102 hadi 107.
Ivory Coast ambayo katika mechi yake ya mwisho Juni 2 mwaka huu iliifunga Taifa Stars mabao 2-0 imeporomoka kwa nafasi moja kutoka ya 15 hadi 16 ikiwa na pointi 943. Hata hivyo ndiyo inayoongoza kwa upande wan chi za Afrika katika viwango hivyo.

             Boniface Wambura
            Ofisa Habari
            Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI WALA KIAPO

                               Mh. Samuel Sitta ambayeni mwakilishi wa Tanzania.
                                 Mh.Abdullah Alli Hassan Mwinyi.
                                  Mbunge Shy-Rose Banji akila kiapo chake.
                                 Shy Rose-Banji akitia saini nyaraka za kiapo.
                                 Mh.Charles Makongoro Nyerere.
                                   Mh. Alhaji. Adam Kimbisa.
                                    Dkt Twaha Issa Taslima.
                                       Mh.Nderkindo Perpetua Kessy.
                                        Mhe Bernard Musomi Murunyana.
                                      Mhe. Anjela Charless Kizigha.

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wameapishwa rasmi kushika madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hilo.

Wabunge hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana Uchumi, Margareth Zziwa kuchukua nafasi hiyo.

Wabunge wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose Saddrudin Bhanji.

Wengine ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi Yahya, Mh.Nderkindo Perpetua Kessy, Dkt Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Mhe Bernard Musomi Murunyana, Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta anaeingia kwa wadhifa wake wa Uwaziri.

Wabunge hao wameapishwa pamoja jana na wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

CHANZO: FATHER KIDEVU BLOG

VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
06.06.2012
YAH: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013


Ndg. Waandishi wa Habari
Mwaka 2011/2012 Kambi ya Upinzani Bungeni ilitangaza Vipaumbele vyake katika Bajeti Mbadala ambavyo vilikuwa:
1. Kupunguza misamaha ya kodi mpaka 1% ya pato la Taifa kutoka 3%
2. Kupunguza kodi kwenye bidhaa za mafuta ya petrol na dizeli ili kupunguza mfumuko wa bei
3. Kufuta mfumo wa posho za vikao (Sitting allowances).
4. Kupeleka sehemu ya tozo ya ujuzi (Skills Development levy-SDL) kwenye bodi ya mikopo ya elimu ya juu.

Masuala haya pamoja na mengine yalikuwa sehemu ya Bajeti kivuli iliyowasilishwa Bungeni na Kambi ya Upinzani.

Mapendekezo mawili,
(1) Kodi za mafuta ya Petrol na Diseli na
(2) Tozo ya SDL yalikubaliwa na kutekelezwa. Pendekezo la misamaha ya kodi lilikubaliwa lakini Serikali imeshindwa kulitekeleza na pendekezo la kufutilia mbali posho za vikao halikukubaliwa.

Kambi Rasmi ya Upinzani inataka maelezo ya kina ya kwa nini Serikali imeshindwa kutekeleza ahadi yake iliyoitoa Bungeni kwamba misamaha ya kodi itapungizwa mpaka kufikia 1% ya pato la Taifa. Halikadhalika Kambi ya Upinzani inarejea wito wake wa kufutwa kwa Mfumo wa posho za vikao (sitting allowances).
Serikali imependekeza Bajeti ya Tshs. 15trillioni kutoka Tshs. 13 trillion. Hata hivyo ni dhahiri kwamba Bajeti ya 2011/12 ilikuwa ina changamoto kubwa za utekelezaji. Serikali ieleze itawezaje kutekeleza Bajeti ya 15trillioni?
Katika Bajeti Mbadala ya 2012/2013 Kambi ya Upinzani itajikita katika maeneo yafuatayo na kuishinikiza Serikali kuyatekeleza.

1. Kuendelea kushinikiza kupunguzwa kwa misamaha ya kodi mpaka 1% ya Pato la Taifa. Hivi sasa misamaha ya kodi ni sawa na misaada yote kutoka nchi wahisani, Tshs 1.03 trillioni ni sawa na 3% ya Pato la Taifa.
2. Kuelekeza raslimali fedha kwenye maendeleo vijijini hasa kujenga miundombinu kama barabara za vijijini na umeme vijijini.
3. Kuelekeza fedha za kutosha kukarabati Reli ya Kati na kufufua njia za Reli za Tanga, Moshi na Arusha.
4. Kuongeza wigo wa kutoza tozo la ujuzi (Skills Development Levy) ambapo sasa waajiri wote walipe ikiwemo Serikali na mashirika ya umma. Pia kupunguza tozo hili mpaka 4% ambapo 1/3 itaenda VETA na vyuo vya Ufundi na 2/3 itaenda Bodi ya Mikopo ili kukabili changamoto ya mikopo kwa wanafunzi.
5. Kushusha kima cha chini cha kodi ya mapato (PAYE) mpaka 9% ili kuwezesha wananchi wa hali ya chini kubaki na fedha za kutumia na kukuza uchumi.
6. Kuongeza mapato ya ndani na kupunguza mikopo ya kibiashara kwa kuhakikisha mapato ya ndani yanafikia 20% ya pato la taifa, kuongeza nguvu za kisheria na udhibiti ili TRA ikusanye mapato zaidi kwenye kampuni za simu na kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, mafuta na gesi.
7. Kutayarisha Taifa kuwa na uchumi wa Gesi.
8. Kupunguza /kufuta kodi kwenye bidhaaa za vyakula kwa muda maalum ili kushusha mfumuko wa bei.
9. Kuweka mfumo mpya wa elimu kwa kushirikisha sekta binafsi katika kutoa elimu kwa ubora zaidi, ikiwemo kuundwa kwa chombo cha Udhibiti wa Elimu(Regulatory authority)
10. Kutoa vipaumbele na unafuu vya kikodi kwa viwanda vya ndani vinavyotumia malighafi za nchni hasa za kilimo na zenye kuongeza ajira kama Korosho,Pamba na Mkonge.

Kambi ya Upinzani itaendelea kufuatilia kwa karibu sana suala la kukua kwa deni la Taifa amabalo limefikia hadi Tshs 22 trillioni na kutaka ukaguzi maalum kuhusu akaunti ya Deni la Taifa.

Kambi ya Upinzani itawekeza kusimamia kwa karibu suala la matumizi yasiyo na tija ya Serikali hasa kwenye magari na posho mbalimbali na Kwamba fedha nyingi zitumike kwa miradi mikubwa ya maendeleo ili kukuza ajira. Halikadhalika namna ya kupta fedha za kutekeleza mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano

Asanteni sana!
…………………………….
Zuberi Kabwe Zitto (Mb)
Waziri Kivuli-Fedha na Uchumi.

source www.globalpublisher.com

Thursday, May 31, 2012

MASTAA WASHINDANA KUANIKA MAPAJA YAO

                                                             Aunt Ezekiel.
                                                    Mayasa Mrisho ‘Maya’.
                                                     Jennifer Kyaka ‘Odama’.

Na Imelda Mtema

SURA za mauzo kwenye anga la Bongo Movies, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Aunt Ezekiel na Mayasa Mrisho ‘Maya’ walifunikana kwa kuvaa nguo zenye kuacha mapaja yao nje hali iliyozua ‘muwashawasha’ kwa wanaume wenye tamaa za mahaba.
Ishu hiyo ilichukua nafasi juzikati kwenye Ukumbi wa Nyumbani Lounge, jijini Dar ambapo mastaa hao walialikwa kusherehekea uzinduzi wa bidhaa mpya ya kinywaji.
“Mh! Jamani hawa wametufanyia makusudi kushindana kuvaa viguo vifupi, hawajui kuwa wanatupa wakati mgumu?” alisikika akihoji mdau mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Dick.
Habari na www.globalpublisher.com

DUDE: ALIYEIROGA BONGO MOVIES AMEKUFA

                                                           Kulwa Kikumba ‘Dude’

Na Erick Evarist

MSANII Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameweka ‘plain’ kuwa kitendo cha wasanii wenzake (Bongo Movies Club) kumtenga amekifananisha na tasnia hiyo ya filamu kurogwa na mtu ambaye ameshafariki.
Akifafanua kauli yake hiyo, Dude alisema wasanii wameshindwa kuelewa kuwa wanapaswa kukanyana wenyewe kwa wenyewe lakini anapofanya hivyo wanafikia hatua ya kumtenga.
“Tunashindwa kuitumia fursa ya rais wetu anayependa sanaa kwa sasa, badala yake tunafanya mambo ya ajabu ambayo kimsingi yanatudhalilisha kwa jamii.
“Hatujui rais ajaye atapenda nini, kama akipenda uvuvi si itakuwa imekula kwetu...sasa wasanii ukiwakumbusha wabadilike, wao wanakuona adui,” alisema Dude.
Hivi karibuni ilidaiwa kuwa Dude ametengwa na Club ya Bongo Movies baada ya staa huyo kufanya mahojiano na Kituo cha Runinga cha Clouds na kuwaonya wenzake juu ya mwenendo wa kitabia.

 www.globalpublisher.com

Tuesday, May 29, 2012

AJINYONGA KWA MADAI YA UGUMU WA MAISHA

Jamaa akiwa ananing’inia muda mchache baada ya kujinyonga.
Marehemu akionekana kwa nyuma.
Baada ya kuteremshwa chini na Wasamaria wema.
Mke wa marehemu akilia kwa uchungu.
Majirani waliokusanyika eneo la tukio.

MWANAMME mmoja ambaye hakutambulika jina lake, aliyekuwa mkazi wa Kigogo-Mbuyuni jijini Dar es Salaam asubuhi ya kuamkia leo (Mei 29), amejinyonga kwa madai ya ugumu wa maisha uliosababishwa na kukosa ajira.
Wakizungumza na mtandao wa huu, baadhi ya majirani ambao walihojiwa walisema kuwa jamaa huyo kwa muda mrefu alikuwa hana kazi hivyo kumsababishia ugumu wa maisha ambao ulikuja kumfanya ajinyonge.
“Siku zote mwanaume ameumbwa kutafuta riziki na si kukaa kusubiri kuletewa riziki. Jamaa huyu alikuwa akikaa tu nyumbani akimuachia mkewe aende akatafute riziki, matokeo yake ndio haya,” alisema jirani mmoja aliyekuwepo eneo la tukio.

Habari na www.globalpublisher.com

Tuesday, May 15, 2012

ORODHA YA WAJANE WA KANUMBA

HABARI hii haina lengo la kumhukumu mtu, mwenye uwezo huo ni Mwenyezi Mungu pekee, lakini Ijumaa Wikienda lina orodha ndefu ya warembo waliowahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ ambapo uchunguzi umethibitisha kuwa, kifo cha staa huyo kimewaacha ‘wajane’ hao katika vilio vya kila kukicha.
Uchunguzi makini uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa nyota huyo alikuwa na uhusiano na wasichana mbalimbali wakiwemo ma-miss, wanamuziki, wasanii wa sinema na wasio na fani yoyote ile.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, kifo cha Kanumba bado kinawachuruzisha machozi wasichana hao kama inavyokuwa kwa wanawake walioolewa halafu wakaondokewa na waume zao (wajane).
‘Wajane’ hao waliotajwa kuendelea kumwaga machozi ni kama ifuatavyo;
WEMA SEPETU
Ni Mrembo wa Tanzania mwaka 2006/07 ambaye kwa sasa ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo. Awali yeye na marehemu Kanumba walijaribu kuficha penzi lao lakini kadiri siku zilivyosonga, hakukuwa na kificho tena.
Kifo cha Kanumba ni pigo kwake, bado anamlilia hadi sasa. Wakati wa msiba alikiri kuwa hakuwahi kutengana moja kwa moja na marehemu.
SYLVIA SHALLY
Ni mrembo wa Miss Dar City Centre 2009, alikuwa na uhusiano na Kanumba, walianza walipokutana katika shindano la kumtafuta Unique Model kwenye Hoteli ya Giraffe, Dar.
Yeye bado hajaamini kama staa huyo aliaga dunia ghafla.
QUEEN SUZY
Ni Mnenguaji wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, aliwahi kudaiwa kuwa na uhusiano na marehemu Kanumba wakati fulani akipiga mzigo kwenye Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’ ambapo mara nyingi Kanumba alikuwa akienda nyumbani kwake.
Anasema kifo cha Kanumba mpaka sasa bado ni ndoto kwake na hakuamini.
SHAMSA FORD
Orodha inamtaja mcheza filamu huyu ambaye aliwahi kuwa na uhusiano na marehemu wakati wakiigiza sinema ya Saturday Morning.
Kifo cha Kanumba kwake ni pengo kwa sababu ndiye aliyemwingiza kwenye ‘gemu’ la sanaa ya maigizo na atamlilia marehemu kila atakapokuwa akimkumbuka.
AGNESS GERALD ‘MASOGANGE’
Orodha hiyo inamjumuisha muuza nyago huyu kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva na filamu ambaye anadaiwa aliwahi kuwa na uhusiano na Kanumba wakiwa kwenye Kundi la Sanaa la Kaole la jijini Dar.
Kifo cha Kanumba anasema bado kinamchuruzisha machozi kila anapokumbuka, hasa mara ya kwanza alipopokea taarifa za kufariki kwake.
SHARZ
Huyu ni mrembo aliyecheza filamu ya marehemu iitwayo The Shock. Ndiye mpenzi wa Kanumba aliyetangaziwa kuolewa, lakini ghafla waliachana na Sharz hajaonekana tena kwenye muvi.
Kifo cha marehemu kilimkuta akiwa masomoni, Kenya. Kilio chake anasema kitadumu na kudumu na kudumu.

AUNT EZEKIEL
Ishu ilibumburuka mwaka jana pale Klabu ya Bongo Movie (Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar) ilipotangaza kumsimamisha ndipo yakaibuka makubwa kuwa alifanyiwa hivyo kwa sababu alimmwaga Kanumba. Baada ya hapo uhusiano wao ukakatika.
Alikuwa mstari wa mbele kwenye kifo cha marehemu, mpaka Muhimbili kuuhifadhi mwili. Anasema hatakaa asahau kifo hicho.
ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’
Kwa sasa anashikiliwa na sheria kwenye Gereza la Segerea, Dar akiwa mshukiwa wa kwanza katika kifo cha Kanumba kufuatia ugomvi wa kimapenzi kati yao.
Siku ya tukio, baada ya ugomvi huo Lulu aliondoka na huko alikokwenda alipata habari kwamba mpenzi wake huyo amefariki dunia, akasema haitatokea akaamini.
SALMA HAMIDU
Ni mdada mkazi wa jijini Mwanza, yeye anatajwa kwenye listi ya ‘wajane’ kufuatia hivi karibuni kuibuka akidai ana mtoto wa kike aliyezaa na marehemu Kanumba aitwaye, Treasure.
Kwa vyovyote vile, kwa kuondokewa na mzazi mwenzake, Salma atakuwa analia kila kukicha, hasa anapomwangalia Treasure.
PASCALIA MACHA
Ni mkazi wa Sumbawanga, Rukwa. Aliibuka na kudai akiwa anaishi Dar, aliwahi kuwa na uhusiano na marehemu na kufanikiwa kupata naye mtoto.
ISABELLA FRANCIS
Huyu ni msanii anayekuja juu kwenye tasnia ya uigizaji Bongo. Amewahi kukiri kuwa ‘alishatoka’ na marehemu kwa mapenzi motomoto na wakamwagana bila bifu.
Kifo cha mpenzi wake huyo kwake ni kitendawili ambacho anaamini siku si nyingi, Mungu atakitegua kuwa maigizo na uhalisia wa marehemu utarudia kama zamani.
WALIOKWENDA NYUMBANI KWA MAMA KANUMBA
Wajane hao hawajaishia hapo kwani wiki mbili baada ya kifo cha staa huyo wa filamu za Bongo wako warembo, kwa nyakati tofauti, waliokwenda nyumbani kwa marehemu maeneo ya Vatican City Hotel, Sinza na kumkabili mama’ke wakimwambia wao walikuwa wachumba wa Kanumba.
Mama Kanumba aitwaye Flora Mtegoa aliwahi kukiri kwa mapaparazi kuhusu ‘wachumba’ hao ambapo alisema idadi yao ilifikia watano.
TUNAMNUKUU:
“Sishangai kusikia kuna wanawake wanaodai walizaa na marehemu mwanangu maana hapa wameshakuja wasichana, nadhani wamefika watano sasa, kila mmoja anadai yeye alikuwa mchumba wa marehemu (kicheko cha uchungu).”
www.globalpublisher.com

NJEMBA AFUMWA AKIMCHUNA MBWA!

-Ilikuwa ni kwa ajili ya mishikaki, supu ya kuuza
 UKISTAJABU ya Musa utaona ya firauni, hali hiyo iliwatokea wakazi wa Ubungo Kibangu pale mkazi mmoja aliyetajwa kwa jina la Rajabu aliponaswa na wananchi akimchuna mbwa.
Baada ya Rajabu kufumwa akifanya kitendo hicho Jumamosi ya wiki iliyopita, alipewa kibano na wananchi wenye hasira kali akakiri kwamba mbwa huyo alikuwa akimuandaa ili akamuuzee kama mishikaki na supu kwa wateja wake.
Shuhuda wetu aliliambia gazeti hili kuwa baada ya wananchi kumtilia shaka anapopata nyama ya kuuza kutokana na hali yake ya kiuchumi kuwa duni, waliunda kikosi kazi cha kumchunguza ndipo arobaini yake ikatimia.
Mtoa habari huyo alisema baada ya wananchi kuchukizwa na kitendo hicho waliamua kumfikisha kijana huyo Kituo cha Polisi cha Kibangu.
“Kijana huyo alipohojiwa na polisi alikiri kufanya biashara hiyo kwa muda mrefu,” kilisema chanzo chetu.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alisema kuwa taarifa juu ya tukio hilo hajazipata na akaahidi kuzifuatilia na kusisitiza kuwa kama ni kweli kijana huyo alifanya kitendo hicho atachukuliwa hatua za kisheria.]
www.globalpublisher.com

SPIKA MAKINDA AWASILI JAPANI KWA ZIARA YA SIKU 6 YA MWALIKO BUNGE LA JAPAN

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika mazungumzo maalumu na Naibu Meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta (kushoto) mara baada ya kuwasili katika mji huo kwa lengo la kujionea uharibifu ulitokana na mafuriko ya tsunami yaliotokea machi mwaka jana ambapo zaidi ya watu 911 walipoteza maisha na wengine 53 kutopatikana katika mji huo. Mhe. Spika na ujumbe wa wabunge 5 wapo katika ziara nchini Japani kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japani.
 Naibu Meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta akimuonesha katika ramani Mhe. makinda sehemu kubwa ya Maeneo yalioathirika na mafuriko hayo katika Mji wa natori.
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkabidhi zawadi Naibu Meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta (kushoto) mara baada ya kufanya nae mazungumzo baada ya kuwasili katika mji huo kwa lengo la kujionea uharibifu ulitokana na mafuriko ya tsunami yaliotokea machi mwaka jana ambapo zaidi ya watu 911 walipoteza maisha na wengine 53 kutopatikana katika mji huo.
 Mhe. Spika akiangalia baadhi ya Mabaki ya wahanga wa Mfuriko hayo katika Shule ya awali ya YORIAGE ambapo picha na nguo za wanafunzi waliofariki zimehifadhiwa.
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiweka shada la maua katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya wahanga wa Mafuriko ya Tsunami yaliyoikumba nchi ya Japan Mwezi Machi mwaka jana alipotembelea Mji wa NATORI, Uliopo mkoa wa MIAGA ikiwa ni mojawapo ya miji iliyokumbwa na mafuriko yaliyoikumba Japani Mwaka jana. Mhe. Spika na ujumbe wa wabunge 5 wapo katika ziara nchini Japani kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japani.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Spika wa Tanzania Mhe. Anne Makinda wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta (Kulia) mara baada ya kuweka shada la Maua katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya wahanga wa Mafuriko ya Tsunami yaliyoikumba nchi ya Japan Mwezi Machi mwaka jana alipotembelea Mji wa NATORI, Uliopo mkoa wa MIAGA ikiwa ni mojawapo ya miji iliyokumbwa na mafuriko yaliyoikumba Japani Mwaka jana. Mhe. Spika na ujumbe wa wabunge 5 wapo katika ziara nchini Japani kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japani. Kushoto ni Mhe. Tundu Lissu, Mhe. Anne Makinda, Mhe. Rukia Ahmed, Mhe. James Lembeli, Mhe Anne Kilango Malecela, Naibu meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta na Mhe. Godfrey Zambi.

Thursday, May 3, 2012

A-Z BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

                                                              Rais Jakaya Kikwete.
Na Elvan Stambul

RAIS Jakaya Kikwete amekasirishwa na utendaji mbovu wa baadhi ya mawaziri wa serikali yake hivyo kuamua kulivunja baraza lake la mawaziri.
Habari kutoka chanzo chetu ndani ya Ikulu zinasema Rais Kikwete amehuzunishwa na ubadhirifu uliofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali, hali iliyomfanya aseme wazi kwamba hakufurahishwa na watu ambao wanachukua fedha za umma ili kunenepesha matumbo yao.


Habari zaidi zinasema kuwa kutokana na ulaji wa fedha za umma ambao Kikwete alisema ni kama wa mchwa, uliofanywa na baadhi ya viongozi wasiokuwa na huruma na wananchi, kuna uwezekano mkubwa wa watuhumiwa kupandishwa kizimbani.

“Hawa watu watachukuliwa hatua za kisheria ili kulinda heshima ya chama chake (Chama Cha Mapinduzi) na serikali yake. Nakuhakikishia kuwa hili limemkera sana rais na hata kile kitendo cha mawaziri kubishana hadharani,” kilisema chanzo hicho. Hadi wakati tunakwenda mitamboni kulikuwa na tetesi kwamba Rais Kikwete angetangaza baraza lake jipya la mawaziri wakati wowote.

Bunge katika kikao chake kilichopita lilipendekeza kwa serikali kuwa mawaziri wanane watimuliwe na wakatishia kuwa wasipotimuliwa watampigia kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutokana na ubadhirifu wa fedha ulioainishwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovic Utouh.

MALI ZA KANUMBA ZAANZA KUUZWA


Na Shakoor Jongo

SIKU ishirini na sita zimekatika tangu nyota wa sinema Tanzania, Steven Charles Kanumba ‘The Great’ afariki dunia, kuna taarifa kwamba mali zake zimeanza kuingia kwenye mauzo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa anasaka mteja wa kulinunua gari aina ya Toyota Lexus lenye namba za usajili T750 AER lililoachwa na staa huyo mkubwa ndani na nje ya Bongo.
CHANZO CHAMWAGA SIRI
Chanzo hicho kimesema gari hilo limeingia sokoni likisimamiwa na mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa) ambaye amekabidhiwa ‘dokumenti’ zote.
“Jamani gari la marehemu Kanumba lile ambalo alikuwa anatambiana na Ray (mwigizaji Vincent Kigosi) linauzwa. Yupo mwanamke mmoja amepewa kazi hiyo na amekabidhiwa makaratasi yote yenye maelezo,” kilisema chanzo.
Kikaendelea: “Mama wa marehemu ndiye aliyeamua hivyo, tayari siku ya Jumanne (juzi) kuna wateja walijitokeza, lakini baada ya makubaliano walitaka kujiridhisha kwa kwenda kwenye ‘yadi’ ambayo Kanumba alipolinunua gari lile, pale Sozmy maeneo ya Kijitonyama, Dar.”
Inadaiwa lengo la wanunuzi hao kwenda yadi ni kutaka kujua kama marehemu Kanumba hakuwa akidaiwa na waliomuuzia gari hilo.
Kuhusu bei, chanzo kilisema kwa mteja anayelitaka anatakiwa kuweka mezani Sh. milioni 45 ili akabidhiwe gari hilo.
Awali, marehemu Kanumba alisema alilinua gari hilo kwa Sh. milioni 78 hivyo kuuzwa kwa bei ya mama ni pungufu ya Sh. milioni 33.
MALI NYINGINE ZIKAE TAYARI
Hata hivyo, kwa mujibu wa habari za ndani, kuuzwa kwa gari hilo ni mwanzo wa maandalizi ya kuendelea kupigwa bei kwa mali nyingine za marehemu ili kuweka sawa maisha ya familia kufuatia kifo cha msanii huyo.

KWA WENZETU WA NJE
Kule majuu nchi za Ulaya na Marekani, utaratibu wa mali za marehemu kama alikuwa supastaa hupigwa mnada hadharani ambapo bei huwa juu kupita ya manunuzi ya awali.
Kama familia ya Kanumba ingeamua kupiga mnada gari hilo kuna uwezekano lingenunuliwa kwa zaidi ya Sh. milioni 100.

KUNA USIRI?
Haijajulikana mara moja sababu za kuuzwa kwa gari hilo ndani ya kipindi cha kuelekea 40 ya marehemu Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwake, Vatican City Hotel, Sinza, Dar.
Taratibu za jamii ya Kitanzania, mali za marehemu hujulikana hatima yake kwenye 40 ambapo hutafutwa mrithi wake.

Ziko pia habari kwamba baba mzazi wa marehemu Kanumba, Mzee Charles Kusekwa Kanumba anayeishi Shinyanga amepanga kupata mgawo wa mali za marehemu huku akisema anajua kila kitu kilichoachwa na mwanaye.
Mzee huyo alipovutiwa simu na paparazi wetu kuulizwa kama ana habari yoyote kuhusu mali za marehemu kuuzwa alijibu atafuatilia.
“Sina taarifa yoyote ila nitafuatilia ili nione hilo likoje,” alisema.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...