Kwa maeneo yaliyopo mabondeni inasemekana kuwa ni tatizo sugu kwa wakazi wa maeneo hayo kuto taka kuhama hususani kwenye mabonde ya jangwani ambalo limebainishwa kuwa eneo la wazi, hayo yamesemwa na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka alipokuwa anafanya mahojiano na waandishi wa habari.
Kwa upande mwingne kuna ripoti za kuharibika kwa Daraja la Kawe bondeni ambako kumesabishwa na mvua hizo hivyo usafiri wa kutoka Tegeta kwenda maeneo ya mjini kuwa tatizo na baadhi ya magari kulazimika kukatisha ruti za kwenda maeneo ya mjini kwa kusingizia kuwa na foreni kubwa.
Kwa tathimini ya haraka mvua hizi zimesababisha Watu wengi kupoteza maisha, kuharibikiwa na nyumba kutokana na kujaa maji, kuanguka kwa nguzo za umeme na kuripuka kwa transfoma kwa baadhi ya maeneo ya Jiji.