Tuesday, May 15, 2012

NJEMBA AFUMWA AKIMCHUNA MBWA!

-Ilikuwa ni kwa ajili ya mishikaki, supu ya kuuza
 UKISTAJABU ya Musa utaona ya firauni, hali hiyo iliwatokea wakazi wa Ubungo Kibangu pale mkazi mmoja aliyetajwa kwa jina la Rajabu aliponaswa na wananchi akimchuna mbwa.
Baada ya Rajabu kufumwa akifanya kitendo hicho Jumamosi ya wiki iliyopita, alipewa kibano na wananchi wenye hasira kali akakiri kwamba mbwa huyo alikuwa akimuandaa ili akamuuzee kama mishikaki na supu kwa wateja wake.
Shuhuda wetu aliliambia gazeti hili kuwa baada ya wananchi kumtilia shaka anapopata nyama ya kuuza kutokana na hali yake ya kiuchumi kuwa duni, waliunda kikosi kazi cha kumchunguza ndipo arobaini yake ikatimia.
Mtoa habari huyo alisema baada ya wananchi kuchukizwa na kitendo hicho waliamua kumfikisha kijana huyo Kituo cha Polisi cha Kibangu.
“Kijana huyo alipohojiwa na polisi alikiri kufanya biashara hiyo kwa muda mrefu,” kilisema chanzo chetu.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alisema kuwa taarifa juu ya tukio hilo hajazipata na akaahidi kuzifuatilia na kusisitiza kuwa kama ni kweli kijana huyo alifanya kitendo hicho atachukuliwa hatua za kisheria.]
www.globalpublisher.com
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...