Wednesday, August 17, 2011

JE, WAFANYABIASHARA WANAJUA UMUHIMU WA "BAR CODE"

Mfano wa bar code

Kwa hali ya kawaida watu wengi wamekuwa wakijiuliza nini maana ya mistari iliyopangika kwa wingi nyuma ya bidhaa nyingi, hususani zinazouzwa kimataifa.
Kwa mataifa ya Ulaya na Marekani, na kimataifa kiujumla hutumia mistari hii maarufu kama "bar code"
Bar Code ni mistari inayogundua ubora wa bidhaa, kampuni iliyotengeneza, bei ya bidhaa hiyo na pia tarehe iliyotengenezwa. GS1 ni taasisi rasmi inayotoa kibali cha "bar code", ambayo makao yake makuu yapo nchini Uswiss. Kwa Tanzania GS1 TZ ilianzishwa mwka 2008, ingawa harakati za kuianzisha ilianza 2005 ikishilikiana na shirika la utafiti na maendeleo ya viwanda Tanzania (TRIDO). Hiyo ndio BAR CODE, ili bidhaa yako iuzike kimataifa bila ya wasisi kwa watumiji wote Duniani lazima iwe na "bar code".  

0 comments:

Post a Comment

CHANGIA MAWAZO YAKO HAPA

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...