Sunday, December 30, 2012

FUNGA MWAKA NA TAMADUNIMUZIK: KILINGE CHA MWISHO KWA MWAKA 2012

Siku ya jana lebo ya muziki wa hiphop Tanzania ijulikanayo kama TAMADUNIMUZIK ilifunga mwaka kwa show ya aina yake pale New Msasani Club.Nadiriki kusema kilinge cha jana kilikua tofauti sana na vilinge vyote vilivyopita kwani kulikua na darasa la kutengeneza mdundo kwa staili ya kukata au kuchop au kwa lugha rahisi kusample kutoka katika nyimbo ZA ZAMANI na madarasa haya yaliendeshwa na watayarishaji wa midundo (producers) wawili tofauti wa kwanza akiwa ni pala.
                     Producer Pala akiwa na Duke kwa pamoja wakielzea na kuhamasisha watayarishaji wa mziki na wale wanaopenda fani hiyo kua kuna uwezekano pia wa kukata au kusample kutoka katika nyimbo za zamani za hapa hapa nyumbani


Masabiki wa tamadunimuzik wakifatilia kwa makini maelezo ya Procucer pala na Duke juu ya ukataji wa midundo(Beats)
 
Darasa la pili lilitolewa na producer Teknohama ambae yeye alionyesha moja kwa moja kupitia projector ambayo iliwezesha wanatamaduni wote kushuhudia kile kilichokua kinafanywa na TEKNOHAMA.Kwa kukadiria teknohama alitumia km dk 20 kusample beat kutoka kwenye nyimbo ya jazz ambayo iliimbwa zamani na hatimae beat hiyo ilikamilika na baadae mtayarishaji mwingine ambae ni MUJWAHUKI kutoka M lab aliijalizia beat hiyo na SONGA akakaribishwa kufree style kwa kutumia beat hiyo.
 Producer Ray teknohama akionyesha sayansi ya ukataji wa midundo


 SONGA Akichana juu ta mdundo huo
Producer Mujwahuki a.k.a Kanye
 
Kilinge hakikuishia hapo,wasanii pamoja na watayarishaji ambao wapo chini ya lebo ya TAMADUNIMUZIK walipta nafac ya kuelezea historia fupi ya maisha yao kimziki na pale walipofikia mpaka
Mtayarishaji wa midundo kutoka m lab mujwahuki a.k.a Kanye akielezea historia fupi ya fani yake ya utayarishaji midundo mpaka alipofikia sasa
 Msanii kutoka lebo ya tamaduni FEISAL
 Songa ni moja kati ya wasanii ambao walipagawisha sana mashabiki siku ya jana
 DUKE TOUCHEZ A.K.A FATHER CHRISTMAS mtayarishaji midundo kutoka m lab ndie alikua Mc
 P THE MC pia alipiga show kali sna iliyoambatana na utambulisho wa track yake mpya
 KIMBUNGA pia alikuja kuunga mkono harakati kitamaduni zaidi


DUKE,NASH MC MPALESTINA PAMOJA NA SONGA
 One The Inredible alisasabisha watu wote kusimama na kuvisaliti viti vyao

 ONE na  SONGA
 
Ni utaratibu wa kawaida wa lebo ya TAMADUNIMUZIK kuonyesha wanachokifanya kwa mashabiki wao kila siku ya jumamosi pake New Msasani Club,hivyo basi kama wewe ni shabiki wa kweli wa hiphop ni vizuri ukiwa unakwenda kuwaunga mkono ili kuufikisha miziki wa hiphop tanzania pale unapotakiwa ufike.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...